Menu
RSS
Tanzania

Unywaji viroba waathiri Watoto Kondoa

Na Mary Yuda, Kondoa

Askofu wa Jimbo Katoliki la Kondoa, Mhashamu Bernadine Mfumbusa amesema kuwa watoto wa Jimbo hilo wanakabiliwa natatizo la unywaji wa pombe aina ya viroba.

Aidha amesema kuwepo kwatabia hiyo ni changamoto kubwa inayowamaliza watoto wa Jimbo la Kondoa na hivyo kushindwa kutimiza ndoto zao.

Askofu Mfumbusa alibainisha hayo hivi karibuni katika Ibada ya MisaTakatifu yaKongamano la UtotoMtakatifuKanda yaMasharikina Kati, lililofanyikakwenyeViwanjavyaKanisa la Kiaskofu la RohoMtakatifuKondoa.

AlisemawatotowaJimbo la Kondoawanashindwakutimizandozozaokutokananakuanzakunywapombewangaliwadogo, haliinayorudishanyumamaendeleoyawatotohao.

KutokananahalihiyoAskofuMfumbusaamewatakawazazi na walezi na watoto wa Utoto Mtakatifu kuwa ombea watoto wa Kondoa ili waweze kuondoka na hali hiyo inayohatarisha maishayao.

Naye Askofu wa Jimbo Katoliki la Mahenge, Mhashamu Agapiti Ndorobo amewataka wazazi na walezi nchini kuhakikisha wanawalea vema watoto wao kwani watoto huchangia kuleta neema na Baraka ndani ya familia.

AskofuNdoroboalisemahayohivikaribuniwakatiakifunguaKongamano la UtotoMtakatifu Kanda yaMasharikina Kati lililofanyikakwenyeJimbo la Kondoa.

Alisemakuwa kuna haja wazazi nawalezi nchini kuwafundisha watoto wao fadhila  mkristo kwa kuwa neemana Baraka zinatokana nafadhila za mkristo.

AskofuNdoroboalizitajafadhilahizokuwanipamojanauvumilivu, upendo, kusameheananakusaidiana.

“Mtotoanapokuwanauvumilivunineemakatikafamilianatunatimizafadhilazakimungukwaniwakatimwinginehaliinawezakuwangumukatikafamiliakutokananamatatizondaniyafamilia”,alisemaAskofuNdorobo.

Alisemakuwakatikakutimizafadhilamambo yoteyanawezekanaendapowazazinawatotohaowatajikabidhimbeleyaMwenyeziMungu.

AidhaAskofuNdoroboaliwatakawatotohaokutambuawajibuwaokatikafamiliaikiwanipamojanakufuatafadhilazakikristokwakuwandiouinjilishajikwasababuukristounaonekanakadiriyamaishawanayoishinakumuombaMungu.

AskofuhuyoaliwatakawazazinawalezikuimarishaupendokwawatotowaoikiwemokuwatimiziamahitajiyaonakuyashiriishakatikaJumuiya, Parokianajamiikwaujumlailikuruhusu Baraka zaMungu.

KongamanohilolilifunguliwanaAskofuNdoroboJulaiMosimwakahuu, likiambatananaseminambalimbalikwawatotopamojanawaleziwaonalinatarajiwakufikiakilelechakeJulai 3, mwakahuu.

Kongamanohilokwamwakahulimebebwanakaulimbiuya ‘Haki ya Mtoto ni Malezi’.

 

Read more...

Mnyika adia ofisi ya waziri Mkuu yawakingia kifua mafisadi

  • Published in Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

 

Mbunge wa Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amedai kuwa ofisi ya Waziri Mkuu inawalinda watendaji wa halmashauri wanaotuhumiwa kuhusika na vitendo vya kifisadi kwenye halmashauri zao.

 

Mnyika alitoa madai hayo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa anauliza swali la nyongeza kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

 

Alidai kuwa hali hiyo ndiyo inawafanya baadhi ya watendaji hususan wa Jiji la Dar es salaam kuwa na viburi pindi wanapoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo zilizoainishwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG.

 

Aliongeza kuwa hata Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa ikiondoa mashauri yanayofikishwa Mahakamani.

 

Hata hivyo akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya TAMISEMI, Kassimu Majaliwa aliliambia Bunge kuwa hakuna mtuhumiwa yeyote anayelindwa na Serikali na badala yake Ofisi hiyo inachukua hatua mara baada ya tuhuma kuchunguzwa na vyombo vinavyohusika.

 

Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju alisema kuwa Ofisi yake ndiyo yenye jukumu la kuondoa mashitaka Mahakamani kwa kuzingatia sababu za msingi za kufanya hivyo.

 

End 

Read more...

SIDO yawapa somo Watanzania

  • Published in Tanzania

Na Mwandishi Wetu

Kutokana na hamasa ndogo iliyopo katika ushiriki wa wananchini kwenye maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, Shirika la Kuendeleza Viwanda Vidogo vidogo (SIDO), limewataka wananchi kuhamasika na kwenda kulitembelea banda lao ili kujionea watanzania wenzao waliothubutu.

 

Akizungumza na Tumaini Media kwenye maonesho hayo Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Mhandisi Omari Bakari alisema kuwa katika banda hilo wapo wajasiriamali wengi waliothubutu kujiendeleza, kutumia teknolojia na ubunifu kwa kutengeneza vitu mbalimbali.

 

Mhandisi Bakari alisema kuwa hiyo ni fursa kwa watanzania wengine hususan vijana waliomaliza vyuo kwenda kujionea ni kwa namna gani na wao wanaweza kujifunza kuzitumia fursa za mafunzo, ushauri wa kibiashara na ushauri wa teknolojia ya kisasa ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali Kutoka SIDO na kwa wajasiriamali wenyewe badala ya kuendelea kusubiri ajira Serikalini au katika Mashirika na taasisi binafsi.

 

Akizungumzia mwamko wa wajasiriamali kushiriki matika maonesho hayo Mhandisi bakari amesema kuwa,umekuwa mkubwa kwani maombi ni mengi kutoka mikoa yote ya Tanzania lakini mwamko wa wananchi kutembelea maonesho hayo kwa mwaka huu ni mdogo.

 

Wakizungumza katika maonesho hayo kwenye Banda la SIDO wajasiriamali kutoka mipakani Noela Gachuma kutoka Boda ya Silari, Edran Mwaku kutoka boda ya Rusumo,

 

Aisha Kisoki kutoka mpaka wa Horohoro na Rose Mlay kutoka mpaka wa Horiri Moshi wamekishukuru Chama cha wafanyabiashara Wanawake (TWCC) kwa kuwawezesha kufanya biashara na kujikwamua na unyanyasaji wa kijinsia kwenye mikoa yao.

 

Wajasiriamali hao wamesema licha ya TWCC kuwawezesha bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kutozwa ushuru mkubwa kwa mizigo wanayoisafirisha kwenye mipaka ya Tanzania na Kenya na Tanzania na Rwanda na hivyo kuwadidimiza kibiashara.

 

 

Read more...

Kanisa lililotumika Zahanati kwenye Vita Kuu ya Dunia lawa kivutio -Tanzania

Na  Mary Yuda

Kondoanimiongoni mwa miji yenye Historia kubwa katika ukanda wa kati nchini Tanznaia.Wilaya ya Kondoa inapatikana mkoani Dodoma ambapo nimakao makuu ya Serikali ya Tanzania.

Wilaya  ya Kondoa iliyo katika mkoa wa Dodoma wakati wa enzi za biashara ya utumwa mji huo ulitumika  kama kituo cha kupumzikia watumwa waliyokuwa wakipelekwa Pwani.

Kwa kipindi hicho eneo hilo lilikuwa likitumika kama njia moja kuwapitisha watumwa hao inayoitwa mtaa wa ubembeni,jina linalotokana na kukaliwa na kabila  laWabemba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambayo zamani ilikuwa ikifahamika kamaZaire ambayo 1900, ilipiga marufuku biashara ya utumwa.

Asili ya neno Kondoa linatokana na Mto unaopita karibu na mji huo ambao watu wa kabira la Warangi waliuita mwairangi Koondo na wakati huo Kondoa ikijulikana kama ula, kikiwa ni soko la biashara  iliyokuwa ya kuuziana  na kununuliana vitu, mahali hapo kwa warangi paliiitwa “wula”ikiwa na maana ya nunua.

Mitaa ya mji wa Kondoa ina majina ya matukio au watu maarufu wa zamanai  ikiwemomtaa wa Bembeni ambapo walikaa kabila la Wabemba kutoka DRC mara baaada ya biashara ya utumwa kufungwa na mabaki ya kabila hilo wapo hadi sasa katika mji huo wa Kondoa.

Mtaa mwingine ni Chemchem ambao unatokana na chemchem isiyokauka inayotoa maji ya moto nyakati za asubuhi, Iboni ni mtaaa mwingine ambao unatokana mtu maaarufu sana na mtawala wa eneo hilo aliyehemishika kwa hekima na busara zake na mtaa wa kwa Pakacha uliotokana na jina la mtawala ambaye alikuwa Mwanangwa wa eneo hilo.

Wakati mtaa wa bomani  unatokana na neno Boma  lilokuwa jengo la watawala wa Kijerumani kwa kuendeshea shughuli  zote za utawala na kwa sasa jengo hilo ni ofisi ya Mkuu wa Wilaya, mtaa wa Mningani umetokana na kuwepo na miti ya mninga na upo karibu na uwanja wa ndege.

Mtaa wa maji ya Shamba, umetokana na kuwepo kwa bwawa linalotumiwa kwa kilimo na kumwagilia mbogamboga na Mnarani, mtaa huu ndipo  mahali palipojengwa  mnara wa kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961. Kondoa ina makabila mengi ikiwemo Warangi,Wasandawe,Waalawi,Wagogo, Wanyaturu na Waberbeig.

Baada ya kuifahamu Kondoa, hebu tuangalie historia ya uinjilishaji katika Jimbo hilo, nikianzia katika Parokia ya Kondoa ya Roho Mtakatifu ambayo ni Parokia mama yenye kiti cha Kiaskofu ambapo ni makao makuu ya Jimbo katoliki la Kondoa.

Kijografia Jimbo Katoliki Kondoa lipo nyanda za kati mwa Tanzania ambapo kwa upande wa Kusini limepakana na Jimbo Kuu la Dodoma, Kaskazini limepakana na Jimbo la Mbulu, kwa upande wa Magharibi limepakana na Jimbo la Singida na  Mashariki limepakana na Jimbo Kuu la Arusha.

Jimbo Katoliki la Kondoa liliundwa Machi mwaka 2011 likiwa Jimbo katoliki la 31 nchini ambalo ni sehemu ya mpango wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania(TEC).

Ukristu ulianza kuingia Kondoa kwa mara ya kwanza mwaka 1907 kupitia Mmisionari wa Shirika la Roho Mtakatifu  Padri Andrea Krieger aliyeitwa “kafefe ambaye alikuwa Mmisionari wa kwanza kupanda mbegu ya Injili katika Jimbo hilo.

Kwa mujibu wa Katibu wa jimbo hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa PMS jimboni humo, Padri Pascal Kilongo, Inasemekana jina la kafefe lilitokana na neno la kirangi “afafa”yaani mgumu au “Kufyefya”  mkali kutokana na kufanya utume wake katika mazingira magumu.

Jimbo hilo lina ukubwa wa kilomita za mraba 13,210, likiwa na idadi ya watu 541,345 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2000 na kwamba ina idadi ya wakatoliki Jimboni humo ni 50,000 wakiwa na Parokia 12 na Mapadri wa Jimbo 18, Mapadri watawa wawili, Mashirika ya Kitawa ya wanawake mawili na Shirika la Mtakatifu Jema wa Dodoma na Shirika la habari njema Babati.

Wakati Mashirika ya watawa wa kiume yanayofanyakazi katika jimbo hilo ni moja ambalo ni Shirika la Mateso la Bwana Yesu Kristo na kwamba lina jumla ya Waseminari wakubwa tisa.

Safari ya Padri Andrea Krieger kuja Kondoa  ilianzia Kibosho Moshi ambapo alifuatana na Bruda Timoteo na makatekista wanne wa kabila la Kichaga  akiwemo Katekista Oktavian (Otto),Albert, Petri na Zefrin, ambaye aliadhimisha Misa ya kwanza kisese Agosti 18  mwaka 1907  na kwamba Ukristu ulipofika Kondoa Uislamu ulikuwepo miaka mingi iliyopita.

Padri Kafefe alihubiri sehemu za Choray, Bubu,Chaangaa na Wisi , hatimaye alipata eneo la ambapo kanisa la Parokia ya Kondoa lipo  hadi sasa.

Ujenzi wa kanisa hilo ulikamilikamwaka 1910na kwamba alifanikiwa kuwabatiza wakristo wa kwanza 60 katika Kanisa la Kondoa katika sikukuuya Krismasi mwaka 1910.

Imani kabla ya vita Kuu ya kwanza yaani kuanzia  mwaka 1907 -1913, mwanzoni Padri Kafefe aliwaandaa Makatekista  11 wenyeji wakuchukua nafasi ya wale aliofuatana nao kutoka Moshi.

Aidha alifanikiwa kuanzisha vigango 13 vya Parokia ya Kondoa ikiwemo Kigango cha Kolo,Tumbelo,Changaa, Loo, Ausia, sega,Dalai,Kwancharai, Bolisa, Muluwa, Baura, Ihalala na Haubi, na baadae Haubi ilikuwa Parokia chini ya Mapadri wa Mateso( Passions Fathers).

Hali ya uinjilishaji wakati wavita Kuu ya kwanza 1914- -1918 haikuwa nzuri kwani shughuli za kichungaji ziliathirika ambapo wakati huo Padri Kafefe alikuwa likizo Ulaya naye Bruda aliyekuwa Parokiani Kondoa alijiunga na Wajerumani wenzake kupigana na Waingereza.

Wakati wa vita hiyo ikiendelea jengo la Kanisa la Kondoa liligeuzwa kuwa zahanati  ya kutunzia na kutibu majeruhi wa vita jambo lililosababisha Kanisa kupigwa mabomu yaliyobomoa paa na kuua majeruhi waliolazwa kwenye kanisa hilo na kwamba iliwalazimu wakristu wa Haubi kwenda kusali Kurhio ambapo ni mbali kutoka Haubi.

Desemba 24, mwaka 1920 Padri Andrea Krieger alirudi na alilazimika kufufua upya imani katoliki  hasa kwa wakristo wachanga waliokosa mchungaji kwa muda mrefu.

Aidha miaka ya 30 Dodoma liligawanywa katika sehemu Kuu tatu  ambapo Kondoa ilikuwa chini ya Vicariate ya Kilimanjaro, Kurio, Bahi na Farakwa  zilikuwa chini ya vicariate ya Bagamoyo na Bihawana  ilikuwa chini ya Vicariate ya Iringa.

Mwaka 1935 Dodoma ilifanywa kuwa Prefecture Apostolic na Padre Disma Giannotti aliyeteuliwa  kuwa Prefect wa kwanza.

 Miaka miwili baadaye Novemba 23 mwaka 1937 Monsinyori StanslaoAmbrozini aliteuliwea kuwa “Prefect Apostolic” wa pili na baada ya kufariki nafasi yake ilichukuliwa na Padre Teodoro Mateo  na Jimbo la Dodoma lilifanywa kuwa Vicario Apostolic Desemba 23 mwaka 1951 chini ya uongozi wake Askofu Jeremia Pesce, Cp alipowekwa wakfu  kuwa Askofu  Desemba 3 mwaka 1951.

Mwaka 1972 Askofu Mathias Isuja Joseph alikuwa Askofu wa Kwanza mzalendo wa Jimbo la Dodoma wakati Mhashamu Yude Thadeus Ru’waichi  alikuwa Askofu wa Jimbo hilo mwaka 2005 – 2011 na Askofu Gervas John Mwasakhabile Nyaisonga kutoka machi 17, 2011.

Jimbo la Kondoa liliundwa Machi 12, mwaka 2011 kwa tamko la Baba Mtakatifu Benedict XVI na Askofu wa kwanza wa Jimbo hilo ni Askofu  Bernadine Mfumbusa ambaye mpaka uteuzi wake alikuwa mkufunzi Mwandamizi katika Idara ya Mawasiliano na makamo Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Mwanza.

Binafsi nimeyafurahia mazingira ya uinjilishaji Kondoa, kwani Kondoa ni Jimbo lililo na Wakristu wachache kuliko Waislamu lakini watu hawa wa imani tofauti wamekuwa wakishirikiana vema bila kujali tofauti zao kama ilivyo katika baadhi ya Majimbo ambayo yana idadi ndogo ya Wakristu.

Jimbo hilo limebarikiwa kupata Maaskofu wazawa watatu akiwemo Askofu Mstaafu Mhashamu Matthias Isuja  wa Jimbo la Dodoma, Askofu Bernadine  Mfumbusa Jimbo la Kondoa na Askofu Agapiti Ndorobo wa Jimbo la Mahenge.

 

 

Read more...

TAHARIRI

 

Serikali iwe makini na uandikishaji Wapigakura

ZOEZI la uandikishaji wapigakura katika daftari la kudumu la wapigakura kwa mfumo wa kieletroniki wa Biometric Registration Voter (BVR), linaendelea nchini.

Hivi karibuni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema katika taarifa yake kwamba inakusudia kuwafikisha mahakamani wananchi zaidi ya 100 wa Mkoa wa Njombe kwa madai ya kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura.

Naibu Katibu wa Tume hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Daftari na Tehama, Dk. Sisti Cariah alisema wananchi hao wamebainika kwa kutumia teknolojia ya BVR na uhakiki huo utaendelea katika maeneo yote nchini.

Alisema picha na majina ya watuhumiwa hao vimepelekwa kwenye idara zinazohusika huku akiwaonya wananchi ambao hawajaandikishwa kuacha kudhani kwamba wanaweza kujiandikisha zaidi ya mara moja bila kubainika.

Haki hii ni jambo la baya ambalo linaweza kuleta shida katika uchaguzi hasa endapo katika baadhi ya maendeleo ikishindikana kubainika kutokana na changamoto mbalimbali.

Lakini pia lipo suala la raia wasio watanzania hasa katika maeneo ya mipakani ambapo bila ya Serikali kuweka udhibiti mkali na kutilia mkazo suala la umakini hakika wataandikishwa watu ambao sio watanzania.

Tuoonavyo sisi ni vema  licha ya kazi hiyo ya uandikishaji kukamilika katika Mikoa mitano nchini ikiwemo ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa na Njombe, bado juhudi za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa na serikali kudhibiti wasio raia kuandikishwa hasa katika mikoa ambayo bado zoezi hilo halijafanyika.

Hali ya wananchi kujiandikisha zaidi ya mara moja na wengine kudai kusahaulika kuandikishwa kwenye daftari hilo hasa katika mikoa ambayo tayari zoezi hilo limekamilika inaweza kuleta shida na kuzusha mijadala ikiwemo kuibua hofu wananchi kuona uwepo wa uchakachuaji kufanyika katika Uchaguzi Mkuu.

Lakini pia jambo lingine ambalo linaonekana kwamba huenda zoezi hilo lisifike kweye mikoa yote ni kutokana na muda unavyozidi kwenda zaidi ikilinganishwa na kasi ya zoezi hilo huku NEC, ikitangza kusogeza mbele uandikishaji wapigakura kwenye mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga na Morogoro kutokana na marekebisho ya mipaka ya kiutawala ya kata, mitaa, vijiji na vitongoji yaliyofanywa na Tamisemi.

Sisi tunawasihi wananchi katika mikoa ambayo zoezi hilo linatarajiwa kuendelea wajitokeze kwa wingi na kujiandikisha, tena mara moja ili waweze kupata haki yao msingi kushiriki Uchaguzi Mkuu badaye mwaka huu na kumchagua kiongozi wanayeona anafaa.

Mungu Ibariki Tanzania.

 

Read more...

Watendaji Wizara zilizotumia vibaya fedha za bajeti wawajibike-Askofu

Na Alex Kachelewa

IMEELEZWA kuwa watendaji wa Serikali na Mawaziri ambayo Wizara zao hazikufanya vizuri katika matumizi ya fedha za bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo wanatakiwa kuwajibika kwani wametumie vibaya fedha za umma.

Kauli hiyo imekuja wakati huu ambapo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilikualikiendelea na vikao vyake vya bajeti mjini Dodoma, ambapo tayari Wizara mbalimbali zimekwisha pitisha bajeti zake.

Kutokana na hali ya kisiasa kuelekea ucuaguzi mkuu bajeti hizo zimepitishwa na  idadi kidogo ya wabunge hasa wa viti maalum huku idadi kubwa ya wabunge wakiwa hawapo kwenye vikao hivyo.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Mhashamu Method Kilaini, wakati akizungumza na Tumaini Letu katika mahojiano maalumu kuhusiana na bajeti ya fedha zinazotolewa kwa Wizara mbalimbali nchini ikiwemo ya mwaka wa fedha 2014/2015 na 2015/2016.

“Bajeti hata kama inapitishwa na wabunge wachache lakini jambo la msingi inatakiwa iwe imetengenezwa vena na hasa wale technical Staff, maana wale ndio wanaoendesha serikali kuanzia Katibu Mkuu wa Wizara”,alisema Askofu Kilaini na kuongeza kuwa:

Lakini kama hao watafanya vibaya katika kutengeneza bajeti hiyo hakika inakuwa shida kubwa kwani Waziri yeye ni kiongozi wa kisiasa na sio mtaalam anaweza kuhamishwa wizara moja kwenda nyingine”,alisema.

“Hivyo kwa Wizara ambazo zilipokea fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo kwa bajeti zilizopita na hakuna utekeleza wowote fedha zile zimeliwa kwa namna moja ama nyingine Mawaziri wanatakiwa kuwajibika na hata kujiuzulu”,alisema Askofu Kilaini.

Alisema kuwa na ndio maana ikapendekezwa kwenye Katiba mpya kupo kwa kipengele kinachoeleza Waziri asiwe mwanasiasa kwa sababu akiwa mtaalam ama wa Maji na nyingine atafanya kazi yake katika wizara husika kama mtaalama na hivyo kuondoa masuala ya kupiga siasa katika mambo ya msingi.

Kwa mujibu wa Askofu Kilaini kwa sasa bajeti nyingi zimepitishwa na idadi ndogo ya wabunge hali inayoweza kutia mashaka kwa wanachi, endapo hazikutengenezwa vema kwani wabunge wengi wa kuchaguliwa wamerudi majimboni kwa ajili ya kujipanga na kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu badaye mwaka huu.

Alisema zipo wizara ambazo kwa namna moja ama nyingine zimeomba fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo lakini zinashindwa kutekelezwa kutokana na ufinyu wa bajeti hasa kwa kutopatiwa fedha zote zilizoombwa huku Wizara zingine zikitumia vibaya fedha hizo za miradi.

Akizungumzia hali ya kisiasa nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu, Askofu Kilaini alisema hatua ya sasa ni ya vyama vya siasa ambapo watu mbalimbali wenye nia wanachukua fomu za kuomba kuteuliwa, lakini bado uhalisia wa nani atakuwa Rais haujafajamika hadi mchujo utakapofanyika ndipo wananchi wataelekezwa namna ya kufanya kumpata kiongozi bora.

“Kwa sasa hii ni inaonesha wazi kwamba demokrasia imekua na kila mtu anaweza kwenda kuchukua fomu hata kama ni darasa la saba ama la pili si kinachotakiwa ni fedha bwana…wakati ukifika itajulikana anayewania Urais ni nani na wananchi wafenye nini ili kumchagua kiongozi bora”,alisem Askofu Kilaini.

Alisema kuwa jambo la msingi kwa wananchi ni kujiandaa na kujipanga ili wapate muda wa kuwauliza maswali watu watakaoteuliwa na vyama vyao jinsi ya kufanikisha ahadi zao baada ya kupata nyadhifa mbalimbali za uongozi.

Kwa sasa Watu wengi waliojitokeza kutangaza nia na kuchukua fomu kwa upande wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaendelea na harakati za kusaka wadhamini katika Mikoa mbalimbali nchini wakisubiri hatua ya mwisho za mchujo ndani ya chama chao.

Hivi karibuni wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walipinga vikali bajeti ya Wizara ya Maji wakidai fedha za miradi ya maji katika kipindi cha mwaka jana ambayo miradi yake haikutekelezwa kama ilivyokusudiwa wakida fedha hizo zimeliwa.

Wabunge hao walisema kuwa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maji haikuweka bayana namna ya utekelezaji wa miradi ya maji vijijini.

Wakichangia bajeti hiyo wabunge hao walidai kuwa hotuba hiyo imetoa taarifa za uwongo kuwa miradi ya maji vijijini imetekelezwa kwa kiwango kibwa jambo walilosema halina ukweli wowote.

Mbunge wa Rungwe Mashariki Profesa David Mwakyusa aliitaka Wizara hiyo kuweka takwimu wazi ni vijiji vingapi vimefikiwa na miradi hiyo ya maji kuliko kutaja kwa jumla ya asilimia.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ether Bulaya aliitaka Wizara hiyo, kutowakumbatia wakandarasi wazembe wanaochelewesha na kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maji vijijini.

Bulaya alisema wakandarasi hao wamekuwa na utendaji mbovu na hawana sifa zinazostahili hivyo wamekuwa wakileta taarifa za uwogo kwa wananchi na kuwalazimisha wananchi kupokea miradi isiyokamilika.

Aidha kwa upande wake David Silinde Mbunge wa Jimbo la Mbozi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEDMA) na Mbunge wa Nkasi, Ally Mohamed Kesi walilalamikia taarifa walizodai ni za uwongo zilizoko kwenye hotuba hiyo kuhusu  utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji vijijini.

Read more...

‘Vyombo vya habari Jimbo Kuu Dar vyenu Waamini’

  • Published in Tanzania

·        Parokia Kipawa yanyakua tena Mbuzi

Na Mwandishi Wetu

Waamini wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wametakiwa kuviona vyombo vya habari vya jimbo hilo vyao na hivyo wanapaswa kuvisaidia kwa hali na mali.

Changamoto hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Tumaini Media, Padri Paul Haule, alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi ya mbuzi kwa washindi wa promosheni ya shinda mbuzi iliyoendeshwa na Gazeti Tumeini Letu.

Alisema kuwa vyombo hivyo ni vya waamini na kwamba watendaji wake wako kwa ajili ya kuwezesha kazi ya uinjilishaji.

Aidha aliwataka mawakala wanaouza gazeti la Tumaini Letu kuendelea kujitolea na kuliwezesha gazeti hilo kuwafikia wasomaji wengi na kurahisisha kazi ya uinjilishaji.

Alisema kazi inayofanywa na mawakala ni ya uingilishaji kwani wanasambaza gazeti lenye kubeba mambo mbalimbali ikiwemo habari za kanisa kwa ajili ya kuwafikishia wengine.

Katika shindano hilo Parokia ya Kipawa imeibuka mshindi kwa mara ya pili mfulululizo ikifuatiwa na Parokia ya Luhanga huku Parokia ya Mbagala ikishika nafasi ya tatu.

Mbali na Parokia hizo tatu Parokia 20 zilizofanya vizuri kwenye promosheni hiyo ni pamoja na Parokia za Mbezi Louis, Yombo Kiwalani, Msewe, Chang’ombe, Salasala, Kimanga, Mbezi Beach, Tabata, Livuvia na Kijichi.

Zingine ni Parokia ya Kizinga, Kilungule, Chanika, Tegeta, Mwananyamala, Oysterbay, Kibaha, Segerea, Hananasifu na Parokia Kuu ya Mtakatifu Yosefu.

Read more...

Mrema akana kutafuna fedha za Jimbo

  • Published in Tanzania

Na Mary Yuda

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) Agustino Mrema amekanusha tuhuma za kutumia vibaya fedha za mfuko wa Jimbo la vunjo na kusema hizo ni hujuma zakutaka kumuondoa katika jimbo hilo.

Hatua hiyo ya Mrema imekuja kufuatia kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulaahman Kinana hivi karibuni katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Jimbo la Vunjo na kusema Mrema anafuja fedha za mfuko wa Jimbo hilo.

“Wanataka kuvuta TLP ili ipoteze Jimbo la Vunjo na kwamba hakuna yeyote atakayeweza kunishinda katika Jimbo la Vunjo”, alisema Mrema.

Akizungumza katika mkutano Mkuu wa Chama hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mrema alidokeza kuwa mfuko huo unakusanya kiasi cha shilingi milioni arobaini na mbili kwa mwaka na si milioni mia kama ilivyosema na Kinana.

Katika hotuba yake iliyojaa malalamiko Mwenyekiti huyo wa TLP amemuomba Rais Jakaya Kikwete  amuagize Kinana  akamuombe radhi katika Jimbo la Vunjo katika mkutano wa hadhara kama alivyofanyawakati akimchafua.

Akizungumzia hali ya usalama nchini, Mrema alieleza kusikitishwa na migogoro mbalimbali inayoendelea nchini  ikiwemo migomo, migogoro ya dini na hivyo kuwaomba viongozi wa Serikali kujitokeza kukemea hali hiyo ili kuiepusha nchi katika hali machafuko.

Katika hatua nyingine mgombea mtarajiwa wa urais kupitia TLP Maximiliani Lyimo alidokeza kuwa uamuzi wake umekuja kufuatia sera za chama hicho na kwamba lengo la TLP ni kuondoa umaskini kwa Watanzania endapo watapata nafasi hiyo.

“Chama chetu ndicho chenye sera nzuri  kushinda vyama vyote na kwama Agenda Yetu Kuu Katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba tutaomba iwe Futa umaskini kwa Tanzania”,alisema Lyimo.

Hata hivyo ameyataja mapendekezo ya TLP kwa uchaguzi Mkuu ujao  kuwa ni pamoja na wagombea watakaopitishwa rasmi na vyama vyao kutafuta muafaaka wa kitaifa wa wa kutazama manmboo mbalimbali ikiwemo suala la katiba .

Suala lingine ni klutafuta Siku maaalum ya kufanya maombi ya kitaifa kumuomba Mungu awavushe salama katika magumu yote ndani ya Taifa la Tanzaniana kwamba maonmbi hayo yashirikishe watu wa dibni zote.

“ Nina muomba Rais wa nchi  kuona umuhimu wa kufanya maombi maaana penye hitaji kubwa na zito kama hali ilivyo kwa sasa ni kiongozi Mkuu wan chi tu ambaye huweza kuita maombi na Mungu akasikia na kujibu kwa haraka  na kwa usahiii”,alisema Lyimo.

End

Read more...

Miaka 51 ya Muungano

  • Published in Tanzania

 

Umoja na amani nguzo imara kwa Taifa

Na Gaudence Hyera

 

MUUNGANO wa Tanganyika na Zanzibar umefikisha miaka 51 tangu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume walipchanganya udongo wa ardhi ya Bara na Visiwa vya Zanzibar Aprili 26, 1964.

 

Viongozi hao watukuka, viongozi wenye upendo na uzalendo mkubwa kwa nchi zao walikubaliana kwa moyo wa dhati kuunganisha nchi zao walizozipenda kuwa Taifa moja chini ya Serikali moja yaani jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Viongozi hawa wasio na mfano pamoja na wenzao wengi walioshirikiana nao kwa sasa wametangulia mbele ya haki ambapo Aprili 7, 1972 Mzee Abeid Karume aliouawa kwa kupigwa risasi akiwa kazini Ofisini kwake Kisiwandui, Zanzibar.

 

Naye Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliaga dunia baada ya kuugua ugonjwa wa Kansa ya damu, pamoja na jitihada kubwa za serikali na madaktari wa hospitali Mtakatifu Thomas huko London alikopelekwa kwa matibabu, alifariki Oktoba 14, 1999.

 

Japokuwa kwa nyakati tofauti tumewapoteza wapendwa wetu hao na wenzao wengi wakiwemo baadhi yao tunaowakumbuka kama Rashid Mfaume Kawawa(Simba wa Vita) na Sheikh Thabit Kombo tutaendelea kuwaenzi. Mungu awarehemu wote.

 

Tunawaenzi  hawa wote kwa sababu walijitoa kwa dhati ya mioyo yao yote, akili zao zote na nguvu zao zote kuiletea Uhuru nchi yao na kuwapenda watu wao waliowaongoza bila ubaguzi wa aina yoyote.

 

 

Tanganyika na Zanzibar ambazo sasa ni Taifa moja la Tanzania linaloendelea kusonga mbele bila kuwepo kwa wazee hao waasisi wa Taifa letu lakini Fikra zao zitaendelea kudumishwa na kukumbukwa daima.

 

Jambo hili linanikumbusha maandiko matakatifu katika Kitabu cha Dini ya Kikristo yaani Biblia Takatifu yasemayo “ Mwenyehaki japokuwa amekufa, atakumbukwa milele.” Maana yake yu hai.

 

Tunayo sababu ya kusema hivi; Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume hakika tutawakumbuka kila wakati unapowadia tunapoadhimisha kumbukumbu ya Muungano na nyingine nyingi za kitaifa ambazo ninyi mlisababisha ziwepo, hatutasahahu kamwe juhudi zenu njema.

 

Miaka hamsini na mmoja ni mingi kwa uhai wa binadamu kwani hapa ni nusu ya karne ambayo tunajivunia na kwamba ni nadra sana kwa binadamu kumaliza karne nzima ingawa wengi wamevuka umri wa kuishi ambao ni miaka sabini, hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alijaaliwa miaka 77.

 

Kuna mambo mengi ambayo leo inawezekana ni chanagamoto na yana tufanya tuwakumbuke waasisi hawa wa Taifa na kubwa zaidi ni kitendo cha kuwafanya watanzania waungane na kuwa kitu kimoja kiasi kila upande  pamoja na changamoto nyingi bado haujathubutu kujitenga.

 

Jambo la Umoja na Mshikamano limekuwa ni sababu kubwa ya kuifanya Tanzania yetu itambulike ndani ya ukanda wa Afrika mashariki na kuheshimika katika bara mama la Afrika na kwingineko Ulimwenguni kote.

 

Dhana ya pili ni Amani na Utulivu miongoni mwa Watanzania ni nyenzo muhimu ambazo zimelifanya Taifa letu kuwa la kupigiwa mfano na hata kuitwa Kisiwa cha amani kutokana na udugu kati ya watanzania wenyewe na kwa wageni na wahamiaji kutoka mataifa mbalimbali.

 

Jambo la ajabu kabisa ni kwa waasisi hawa hawakuwa wabinafsi wa kujali nchi yao pekee bali pia walifanya jitihada kubwa wakati huo Mwalimu Nyerere akiwa Rais na Mzee Karume akiwa Makamu wa Rais, walishirikiana na viongozi na wanaharakati wa kudai uhuru katika mataifa mengine, hivi leo tunashuhudia Afrika yote ipo huru.

 

Tunaposherehekea Muungano wetu na kuadhimisha kumbukumbu ya miaka hiyo zaidi ya hamsini tuone fahari kubwa na tusifanye ajizi na kudhani kwamba tumeifikia kirahisi tu bila jitihada au miongozo makini ya viongozi wa Taifa.

 

Kwa nyakati tofauti umoja na amani vimesisitizwa na viongozi wetu kwa awamu zote tangu awamu ya kwanza ya waasisi Nyerere na Karume, awamu ya pili ya Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi na wenzake.

 

 Pia awamu ya tatu ya Benjamin William Mkapa na awamu ya sasa ya nne ambayo bado ipo madarakani ya Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete wamesisitiza umuhimu wa jambo hilo kwa ajili ya  usalama wa nchi na Watanzania kwa ujumla.

 

Zipo changamoto nyingi, zipo tofauti mbalimbali za Kiitikadi, kisiasa, kiimani{msukumo wa udini na kudharau uhuru wa kuabudu} na ukabila zikomeshwe, zisipewe nafasi na kila mmoja aweke mbele utanzania na kauli mbiu ya kila mmoja iwe “Tanzania kwanza.”

 

Muungano wetu miaka hamsini na mmoja unasherehekewa wakati tukiwa tunaelekekea uchaguzi Mkuu wa Serikali yaani Rais, Wabunge na Madiwani Mwezi Oktoba. Pia bado kura ya maoni ya Katiba iunayopendekezwa inatusubiri.

 

Katika mambo yote haya Mwelekeo wa Viongozi wa Serikali, Vyama vya Siasa na Taasisi mbalimbali msisitizo uwe Tanzania kwanza. 

 

 

Hii ina maana kwamba japokuwa kila mmoja anatamani kuwa kiongozi katika ngazi yoyote ile, au chama cha siasa kimoja kinajiandaa kukishinda kingine na lolote litakalofanyika lengo na nia iwe ni kuendeleza Tunu za umoja na amani.

 

Nakumbuka Tungo nzuri iliyoghaniwa vyema na kundi la sanaa za maonesho la Tanzania one Theatre-TOT chini ya Kepteni John Damian Chimtetemo Komba {sasa marehemu Mungu amrehemu} inabeba maneno haya:  walau shairi moja na kiitikio.

(bila shaka yoyote Mwalimu  alimshirikisha mwenzake Mzee Karume akashauriana waasisi wenzake na wakakubaliana)

 

Shairi: Tumejaliwa sana sisi Tanzania,Ngao yetu umoja tumeshikilia, heri tujiulize nyi watazania, vipi malengo yetu tumezingatia.

 

Kiitikio: Mawazo ya Mwalimu yameshatimia, kudumisha umoja ndiyo yetu nia, ni wajibu kumshukuru baba Nyerere (Karume), kwa furaha kumsifu wingi wa hamu, mwalimu ndugu yetu tunamfahamu, mwalimu ndugu yetu tunamshukuru; Ni yeye ameleta umoja wa Taifa, ni yeye ameanzisha Taifa letu change Nyerere(Karume).

 

Kwa hiyo tunapoadhimisha miaka hii hamsini na mmoja bila ubinafsi tufanye tathmini ya kina na kurejea tulikotoka. Tulipo na tunakoelekea kwa dhati kabisa ya kuulinda Muungano na kuendelea kuishi katika nchi nzuri yenye  umoja, amani, utulivu na maendeleo endelevu.

 

end

Read more...

Askofu Sangu atikisa Shinyanga

  • Published in Tanzania

Na Alex Kachelewa, Shinyanga

ASKOFU mpya wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Mashamu Liberatus Sangu amesimikwa rasmi kuliongoza jimbo hilo, huku akitakiwa kuongoza kwa kuzingatia misingi ya haki na upendo mkuu.

Aidha askofu Sangu ametakiwa kuwarejesha katika zizi la Bwana kondoo wote waliopotea ili kustawisha uinjilishaji jimboni humo.

Hayo yamesemwa na Maskofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, jimbo Kuu la Mwanza na Rais wa Baraza la Maskofu Katoliki Tanzania (TEC), Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwaambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa, wakati wakiwasilisha salamu za kichungaji kwenye Misa Takatifu ya  kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu mpya Sangu, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Kanisa Kuu la Mama Mwenye Huruma, Ngokolo.

Kwa upande wake Rais wa TEC, Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa, amesema Askofu mpya Sangu anatakiwa kuzingatia misingi na kanununi za Baraza la Maaskofu katika kutekeleza majukumu yake ya utume na kutotoka nje ya sheria hizo.

Alisema Askofu Sangu nini mtu mwenye uzoefu katika masuala ya kichangaji, hivyo atumie vema uzoefu huo katika kuliendeleza jimbo hilo.

“Ni muhimu sana kuliongoza jimbo hilo kwa uadilifuli na upendo Mkuu na pia chunga kondoouliokabidhiwa kwa nyaNyanjate kwani waamini hawa wanahitaji sana msaada wako”,alisema Askofu Ngalalekumtwa.

Alisema kuwa ni vema Askofu Sangu katika ut umishi wake wa uinjilishaji ajitahidi kwa kiasi kikubwa kusimamia haki miongoni mwa jamii hasa yaw a Jimbo la Shinyanga.

Aidha amesema TEC, inampongeza Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi kwa kulisimamia vema jimbo la Shinyanga hadi anapolikabidhi kwa askofu mpya Sangu.

Amewataka Mapadri, Watawa na waamini wa Shinyanga kujitoka na kumpa ushirikiano askofu huyo mpya ili kumwezesha kutekeleza vema majukumu yake ya kuinjilisha.

BALOZI WA PAPA ATOA RAI

Naye Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Mkuu, Fransisco Padilla, amemtaka Askofu Sangu kuhakikisha anakabiliana na changamoto mbalimbali za uinjilishaji jimboni humo.

Amesema waamini wa Shinyanga wamevumilia kwa kiasi kikubwa hasa kwa kukaa bila ya Askofu kwa kipindi cha miaka mitatu, hivyo ujio wa askofu huyo mpya utasaidia kwa kiasi kikubwa kuendeleza imani katoliki.

Aidha amemtaka ajenge dhamiri ya kuwafundishi waamini hao imani katoliki kwa kupeleka upendo palipo na chuki ili kulata maendeleo ya kiuinjilishaji.

Hata hivyo Askofu Mkuu Padilla amewataka waamini hao kumpokea Askofu Sangu na kumpa ushirikiano na kufanikisha vema utume wake.

KARD. PENGO ATAKA ASKOFU SANGU KURUDISHA KONDOO WALIOPOTEA

Aidha naye Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ambaye alikuwa akiongoza Misa hiyo ya daraja ya uaskofu, katika humilia yake, amesema kuwa Askofu Sangu anatakiwa kuwatumikia watu na sio watu wamtumikie yeye.

“Nawe ndugu mpendwa uliyeteuliwa na bwana  uzingatie moyoni kuwa umechaguliwa kati ya wanadamu na ukawekwa kwa ajili ya wanadamu katika ambo yamhusuyo Mungu, maada uaskofu ni jina linalomaanisha utumishi wala si adhama na askofu hupaswa kutumikia katika kutawala kwa sababu kadiri ya maagizo ya mwalimu wetu aliye mkubwa na awe kama aliye mdogo na mwenye kuongoza kama yule atumikaye”,alisema Kardinali Pengo.

Alisema kuwa Askofu Sangu anatakiwa kulihubiri neno la Mungu wakati unaofaa na usiofaa kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho na kutoacha kuomba neema mbalimbali kwa ajili ya watu aliokabidhiwa.

Kwa mujibu wa Kardinali Pengo pia askofu huyo awapende  wote aliokabidhiwa na Mungu kwa upendo wa kibaba  na kindugu  kwanza kwa Mapadri na mashemasi  washiriki wake katika  katika utumishi wa Kristo.

“Lakini pia wapende walio maskini na wadhaifu, wasafiri na wageni wahimiza waamini wote washirikiane nawe  katika kazi za kitume na wala usikatae kuwasikiliza  kwa radhi”,alisema na kuongeza kuwa:

“Kuhusu wale ambao hawajaingizwa bado kwenye zizi lile moja  la Kristo nao uwashughulikie  bila kuchoka maana hao nao wamekabidhiwa kwako na Bwana”,alisema Kardinali Pengo.

RAIS KIKWETE ATAKA SEHEMU ZA IBADA ZIHESHIIWE

Kwa upande wakeRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, amewataka viongozi wa dini nchini kukataa kuwapa nafasi wanasiasa kuyafanya makanisa na misikiti majukwaa ya kisiasa kwani kunaweza kuwagawa Watanzania.

Rais Kikwete alisema hayo mjini Shinyanga alipokuwa akitoa salama za Serikali kwenye sherehe za kumweka wakfu na kumsimika Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Mhashamu LIBERATUS SANGU.

Rais Kikwete alisema, kazi iliyo mbele ya viongozi wa dini kwa sasa nchini ni kuziba nyufa zilizopo za tofauti za kidini, ukabila na itikadi za kisiasa.

“Ni wajibu wa viongozi wa dini kuwaelimisha waumini wenu kuhusu madhara ya migogoro ya kidini ili kudumisha amani, upendo na mshikamano baina ya Watanzania kwani inapotokea migogoro ya kidini moto wake kuuzima ni kazi kweli”,alisema Rais Kikwete.

Alisema kuwa, kwa hali ilivyo sasa, ya kuanza kuibuka kwa tofauti hizo za kidini katika jamii, viongozi wa Dini wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha hali hiyo inadhibitiwa na hairuhusiwi kuendelea.

Alifahamisha kuwa endapo viongozi wa dini watatimiza vema majukumu yao ya kuwaelimisha wananchi khusu madhara ya migogoro ya dini,kuacha vitendo vya wizi na mauaji ya albino itakuwa kazi raisi hata kwa Serikali  kuongoza nchini kwani taifa litakuwa na watu waadilifu.

“Kasi inayofanywa na viongozi wa dini na serikali ni moja, ya kuhakikisha watu wanakuwa waadilifu, viongozi wa dini kazi yenu ni kuwalea watu kiroho ili waachane na vitendo vya wizi, kufumaniwa, kuua albino na sisi kaka Serikali tunawakamata na kuwafunga gerezani matokeo yake naambiwa magereza mzee yamejaa lakini watu hao wakielimisha vema kazi ya serikali nayo inakuwa rahisi”,alisema Rais Kikwete.

Alisema kuwa kupatikana kwa Askofu Sangu kutasidia askofu huyo kuwaelimisha wananchi wa Shinyanga, ambao mara nyingi wamekuwa na imani potofu za mauaji ya vokongwe na albino.

Rais Kikwete alisema kuwa serikali itaendelea kushiriiana vema na Kanisa Katoliki katika Nyanja mbalimbali kwani tangu awali ushirikiano huo umekuwa ukifanyika zaidi ikiwemo ujenzi wa hospitali ya Bugando.

“Serikali na Kanisa katoliki tumekuwa tukishirikiana vizuri na kwa ushirikiano huo maendeleo yameonekana”,alisema Rais Kikwete.

Aidha alisema Serikali itaendelea kusimamia na kuimarisha uhuru wa kuabudu kwani hata katika Katiba inayopendekezwa jambo hilo limezungumzwa vizuri.

Alisema viongozi wa iwaelimishe waamini wake ili watu waweze kuishi kwa upendo, umoja bila ya kujali tofauti zao za kidini, rangi na itikadi za kisiasa.

Amewataka viongozi hao kuhakikisha hawato nafasi kwa wanasiasa ambao wamekuwa wakiyatumia majumba ya ibada kama majukwa ya siasa kwani kufanya hivyo kunaweza kuleta shida katika taifa.

“Nyingi wanasiasa wakija kwenye misikiti, na makasani waondoeni waambieni hapa si mahali pake wakafanya kazi hiyo kwenye majukwaa ya kisiasa nyumba hizo ziachwe zitumike kwa kazi iliyokusudiwa”,alisema Rais Kikwete.

Alisema katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu viongozi wa dini wanatakiwa kuwa makini zaidi kwani wapo wanasaisa wanaoajali maslahi binafsi wanaweza kufanya uchochezi kwa utumia mgongo wa dini na hivyo kuliweka mahali pabaya taifa.

 

ASKOFU SANGU: NITAENDELEA KULINDA YALIYOASISIWA

Naye Askofu Sangu, alitoa salam zake, alisema kuwa atajitahidi kusimamia na kuendeleza yote yaliyoanzishwa na mtangulizi wake, mrehemu Askofu Aloysius Balina.

“Nitafanya yazi yangu ya uinjilishaji kwa kuzingatia utume wa Kristo mtumishi mwema kutumikia waamini na si kutumikiwa”,alisema Askofu mpya Sangu.

Askofu Sangu alizaliwa   Februari 19, mwaka 2963 katika kijiji cha Mwazye Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa. Alibatizwa Februari 19, mwaka 1963.

ELIMU YA MSINGI

Alipata elimu ya msingi katika shule ya Mamba Chiwanda na Tunduma kati ya mwaka 1970  hadi mwaka 1976.

Baada ya kumaliza elimu ya msingi alijiunga na  suhle ya Sekondari Iyunga mkoani Mbeya  na kuhitimu kidato cha nne  mwaka 1982.Aliendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Shinyanga kuanzia mwaka 1983 hadi mwaka 1984.

Kwa mujibu wa taratibu za nchi kwa wakati huo, kila mtanzania aliyemaliza kidato cha sita alilazimika kujiunga na mafunzo ya Kujenga Taifa (JKT),ambapo alijiunga na mafunzo hayo kuanzia mwaka 1985 hadi mwaka 1986 huko Mafinga.

ELIMU YA SEMINARI

Mwaka 1978 Askofu Sangu alijiunga na Seminari Kuu ya Kibosho iliyopo mkoani Kilimanjaro, jimbo la Moshi kwa ajili ya masomo ya falsafa na kumaliza mwaka 1989.

Badaye mwaka 1989 alijiunga na Seminari Kuu ya Mtakatifu ya Mtakatifu Caroli Lwanga Segerea Jimbo Kuu la Dar es Salaam, kwa ajili ya masomo ya TaaliMungu na kuhitimu mwaka 1992.

Baada ya majiundo yake seminarini alirudi jimboni kufanya mwaka wake wa kichungaji kati ya Juni mwaka 1992 hadi Juni 1993.

USHEMASI NA UPADRISHO

Baada ya kumaliza mwaka wake wa kichungaji alipewa daraja la ushemasi Junuari 9, mwaka 1994 katika Parokia ya Tunduma. Badaye alipewa daraja takatifu ya upadri Juni 3, mwaka 1994 katika Parokia ya Sumbawanga.

UTUME WA ASKOFU SANGU

Katika maisha yake ya upadri, Askofu Sangu Sangu amewahi kuwa Mwalimu na Mlezi wa Seminari ndogo ya Kaengesa  Jimbo la Sumbawanga kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka 1995.

Badaye aliteuliwa kuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Matai kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 1996.

Kati ya mwaka 1996 hadi mwaka 1999 alikwenda mjini Roma  kwa masomo ya juu  na kujipatia Shahada ya Uzamili katika masuala ya TaaliMungu  ya Sakramenti za Kanisa  kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa c ha Mtakatifu Anselmi kilichopo mjini Roma.

Kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2000 aliteuliwa kuwa Msimamizi wa Parokia ya Mwazye.

Mwaka 2007 hadi 2008 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa miito Jimbo la Sumbawanga, Katibu wa elimu Jimbo, Gombera mwaka wa malezi na Mkurugenzi wa utume wa Vijana Jimbo la Sumbawanga.

Ndani ya muda huoalihudumu pia kama Paroko wa muda wa parokia ya Sopa. Kuanzia mwaka 2008 hadi uteuzi wake amekwua akitekeleza utume wake akiwa mjumbe wa senate, mjumbe wa SADC kitengo maalum cha walemavu na afisa mwandamizi Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu mjini Vatican.

Ambapo Februari 2, mwaka 2015 Baba Mtakatifu Faransisko alimteua Monsinyori Liberatus Sangu kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Shinyanga, ambalo lilikuwa wazi tangu Novemba 6, mwaka 2012 kufuatia kifio cha Askofu Aloysius Balina, na akawekwa wakfu na kusimikwa rasmi kuongoa Jimbo Shinyanga, Aprili 12, 2015.

End

 

 

Read more...
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.