Menu
RSS
Tanzania

Tusilazimishe wanafunzi kusoma wasichopenda.

 

 

Na Joyce Sudi

 

Kipaji  ni kitu cha pekee ambacho Mungu  ameweka ndani ya mtu kufanya jambo la pekee kabisa.kitu hicho kinamfanya mtu huyo kuipenda kazi yake, kujituma na kuwa mbunifu zaidi na kuifanya katika mazingira yoyote.

 

Kila mmoja wetu anapozaliwa katika dunia hii kuna kitu ambacho Mungu   anakuwa amemuwekea, kwa ajili ya kuweza kusaidia wengine kwa namna moja ama nyingine hali inayopelekea wote kuishi kwa kutegemeana.

 

Kumbe kila mmoja ana umuhimu wake katika dunia hii ikiwa atatumia  vizuri kipaji chake kinachoimarika zaidi  kupitia taaluma aliyosomea kwa moyo, kwa maana kipaji pasipo elimu ni sawa na maji kumimina katika ndoo iliyotoboka.

 

Mara zote huwezi kujenga nyumba pasipo kuanza na msingi ,hii namaanisha kwamba kipaji cha mtu yoyote kinaanza kuonekana tangu akiwa mdogo na endapo wazazi au walezi watachukua hatua madhubuti kusimamia vema kipaji cha watoto wao hatimaye kinachipuka na kuwa manufaa kwao, jamii na  Taifa kwa ujumla.

 

Walimu na wazazi wakishirikiana na Serikali wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha kila mmoja anatumia vema talanta aliyopewa na Mungu, kwa kuwa endapo mtoto atakoseshwa kuimarishwa katika kipajichake  moja kwa moja atakuwa amekoseshwa kufika kwenye njia ya mafanikio na kila kukicha atalalamika maisha ni magumu .

 

Hapo ndipo linapoonekana tatizo sehemu nyingi sasa ukipita mitaani utakuta kijana anakwambia yeye alitamani sana kuwa Daktari au Mwalimu au Karani na fani nyinginezo lakini ufaulu haukumuwezesha kwa hiyo imebidi aende akasomee fani ambayo hakuipenda.

 

Swali linakuja ni kwamba mtu kama huyuataitendea vema hiyo fani aliyoisemea ambapo watoto wa mjini wanaita kishingo upande ,kwa sababu tu alifaulu masomo ya michepuo hiyo? vipi kuhusu talanta yake imekufa ? je mtu huyu atakuwa ametendewa haki?

 

Majibu ya maswali hayo yanakuja kuonekana katika matokeo ya utendaji kazi ,kwa maana tumeshuhudia mambo mengi yakitokea namengine yanayomalizika kimnyakimnya katika sekta mbalimbali nchini, achilia mbali mtu aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya goti, mwalimu kumpiga mwanafunzi kipigo cha mabondia n.k.

 

Hatuna sababu ya kushangaa kwa maana inaonekana watu wako kimaslahi zaidi sasa  na wameweka kando talanta zao,hali inayopekea mtu hata kufoji cheti ili akasomee masomo ambayo anaona kwake yatamuwezesha kupata ajira chapuchapu  ya kumkidhi kimaisha.

 

Wengine wanaishi kwa kuigiza mitindo ya mafanikio yawengine, pasipo kujali mambowaliyoyafanya  kwa urahisi  na upekee yakawaletea mafanikio ,kwa kuona mafanikio yake yanachelewa anaona aingie kwenye mafanikio ya talanta ya mwingine na kuishia kuifanya kazi hiyo ambayo siyo fani yake kwa ugumu sana tofauti na mwenye talanta yake.

 

Ingawa wapo waliopata neema ya Mungu kwa kutambua vipaji vyao na kurudi kwenye mstari ,ambapo unaweza kukuta mtu alikuwa mwalimu akaona ualimusiyo talanta yangu akajiendeleza na akasomea talanta yake husika ,au mtu alisomea uuguzi baadaye akaona haikuwa talanta yake na akasomea uandishi wa habari ,n.k mtu kama huyu atakuwa ametimiza haja ya kile alichowekewa moyoni na Mungu kukifanya na kwake kazi iatakuwa rahisi hata kama atafanya katika mazingira magumu kiasi gani.

 

Kimsingi kijana hakuwa na sababu ya kulalamika maisha magumu lakini kwa kuwa mfumo wa maisha yake umeharibiwa tangu akiwa mdogo basi  kwa kusomea fani ambayo haikuwa ndoto ya maisha yake lazima ataongea maisha ni magumu hata kama anafanya kazi yenye hela kiasi gani.

 

Tatizo lingine linakuja katika mfumo wa elimu ambapo hautazami talanta ya mtu bali unaangalia michepuo aliyofaulu hali inayopelekea mtu mbeleni kufanya kazi asiyoipenda, wakati mwingine mtu huyu huenda aligezea kwa mwenzake akafaulu vizuri masomo husika na akaenda nayo hadi chuo yakampatia kazi ,ambapo tatizo linakuja katika utendaji.

 

Lakini pia serikali imekuwa ikilalamika kuwa na uhaba wa watalamu wa fani mbalimbali wakati wapo ambao wana moyo wa kufanya fani hizo lakini hawakupewa nafasi ya kuengaliwa tangu utoto talanta zao hata kama walifeli darasani lakini ukiwaweka kivitendo uwezo wao wa kuitendea haki kazi husika ni mkubwa  kuliko yule aliyefaulu.

 

Inapaswa sasa tubadilike kwa kutokuangalia ufaulu wa cheti pekee,bali tuangalie ufaulu na uwezo wa mtu , kwa maana hata ukienda katika usaili mbalimbali wa kazi mtu anaambiwa umefanya vizuri lakini cheti chako hakionyeshi ufaulu mzuri kuliko wa mwenzako,Swali ni kwamba anayefanya kazi ni cheti, stashahada, shahada au mimi?.

 

Huku ni kuudanganya ubongo kwamba mwenye ufaulu mzuri ndiyo ana akili na anakiwezea fani hiyo kuliko aliyefeli ,jambo linalotugharimu sasa mtu  anashindwa kuelewa wajibu wake kwa sababu haoni umuhimu wa kujifunza kitu ambacho hana kiu nacho katika maisha yake  zaidi ya  kuonyesha ufaulu katika  cheti pekee.

 

Wenzetu katika Nchi  zilizoendelea wanaheshimu sana talanta ya mtu kwa sababu wanaelewa ndiyo inayobeba mustakabali wa maisha yake na Nchi yake kwa ujumla ndiyo maana wanatoa fursa kwa wananchi wao kujaribu mambo yao kwa kumuendeleza mtoto kipaji chake tangu akiwa mtoto kwa sababu uhalisia wa kitu huanza mwanzo ndiyo maana mtoto anafatiliwa jinsi anavyoishi mwingine tangu mtoto utaona anapenda kufundisha,kuhudumia wagonjwa anakaa kama hakimu,muhudumu n.k.

 

Tunahitaji na sisi siku moja tuwe na wavumbuzi kutoka Nchini Tanzania na sio kuwasikia wenzetu wakivumbua vitu mbalimbali kila kukicha kana kwamba kwetu watu hawana akili ya uvumbuzi ,la hasha,!tatizo kipaji chake hakikuchochewa tangu kilipoonekana na kumuwezesha mtoto huyo awe na fikra nyingi za kufanya mambo makubwa kadiri kila siku anavyokuwa.

 

Kuni zinakuwa ziko tayari pale zinapowashwa moto kwa ajili ya kutumiwa na kutoa moto mkali na mzuri kwelikweli,lakini kuni hizi zisipochochewa moto unakuwa hauna nguvu  na hatimaye kutawanyika,ndiyo sawa sawa kinachomaanishwa endapo mtoto huyo hakuchochewa kipaji chake ,ndipo hapo zinapoibuka labda nyingi na fikra zake zinatawanyika na kujikuta anasomea fani kwa kujaribu tu kama ataiweza na si kwanza ndiyo lilikuwa chaguo lake.

 

Katika mfumo wa elimu ushirikiano unahitajika kupatikana kwa taarifa ya msomi tangu shule ya chekechea hadi sekondari ili kupata kitu halisi atakachoweza kufanya katika maisha yake na kikawa msaada kwake ,jamii na Taifa nah ii pia itaweza kuweka uwiano sawa wa wataalamu katika Nyanja mbalimbali na kuepuka kila kukicha serikali kulalamika wana uhaba wa watu wa taaluma fulani.

 

Basi kama tunafahamu kwamba mara nyingi mtoto hadanganyi kwamba ushahidi atakaotoa mtoto ni wa kweli, kwa hivyo ni rahisi sana kupata ukweli wa talanta ya mtu kwa kuweka rekodi yake ya matamanio yake tangu akiwa mdogo na hata kuoanisha kwamba kile alichokuwa anakitamania kina uwiano na hicho alichosoma.

 

Haidhuru mtu huyo kama mtihani wa kidatocha nne au shule ya msingi alifeli masomo,lakini bado kuna kitu ndani yake ambacho akiendelezwa kitaaluma kitakuwa msaada mkubwa sana, kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeuenzi vema ule usemi wa tajiri maarufu sasa Bill Gates aliwahi kusema kwamba .

 

“Mimi nilifeli baadhi ya masomo yangu kwenye mitihani lakini rafiki yangu alifaulu yote, Sasa yeye amekuwa mhandisi kwenye kampuni yangu ya Microsoft na mimi nimekuwa mmiliki wa kampuni ya Microsoft”.

 

End

 

 

 

Read more...

Jamii Tanzania yatakiwa kuacha mtazamo hasi kuhusu magereza

 

Na Bruno Bomola

 

Tukiwa bado tupo katika jubilee ya huruma ya mungu alhamisi ya 6/102016 ilikuwa ni siku ya huruma ya mungu kwa wafungwa na mahabusu ambapo adhimisho hilo lilifanyika katika magereza saba tofauti katika jimbo kuu la dare s salaam.

 

Wafungwa na mahabusu hao walipata nafasi ya kufundishwa mafundisho na tafakari ya mungu pamoja na kupatiwa sakramenti ya kitubio na baadae kufuatiwa na adhimisho la misa takatifu.

 

Askofu msaidizi wa jimbo kuu katoliki la Dar es salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwaaliadhimisha huruma ya mungu kwa wafungwa na mahabusu katika gereza la segerea .

 

Askofu Nzigilwa amewataka wafungwa na mahabusu kuwa na moyo wa huruma na  msamaha pamoja na kuwasaidia wao kwa wao ikiwemo kutendeana matendo mema.

 

“tumekuja kuwaambia ndugu zetu walioko magerezani mungu bado ana wapenda mungu bado ana wa hurumia haijarishi wapo katika mazingira gani ikumbukwe kwamba hata kristu mkombozi wetu naye katika historia yake ya maisha alikuwa mfungwa mtakumbuka kwamba yesu alikamatwa na askari wa kirumi akawekwa gerezani na akahukumiwa na alihukumiwa kufa adhabu kubwa kabisa ambayo binadamu anaweza kupewa na mamlaka ya kidunia”

 

Tunataka kuwapa ujumbe huu ndugu zetu walioko magerezani wasikate tamaa kristu alishiriki hali zote hizo wale wote walioko magerezani wamkumbatie mungu na kumrudia kama mwana mpotevu alivyorudi nyumbani kwa baba watubu na kuanza maisha mapya alisema Muhashamu Nzigilwa.

 

Aidha askofu Nzigilwa ametoa shukrani kwa uongozi wa magereza kuruhusu zaidi ya mapadri ishirini kuzunguka katika magereza yaliyopo ili kuhakikisha wanatoa huduma hiyo kwa wafungwa na mahabusu.

 

Hata hivyo amebainisha kuwa huduma hizi za kiroho zinazotolewa zimekuwa ni sehemu muhimu ya kurekebisha tabia na mienendo ya ndugu zetu walioko magerezani kwani huduma za magereza peke yake bila huduma ya kiroho pengine hazita harakisha mageuzi ya kitabia wanayoyatarajia kutoka kwa wafungwa na mahabusu.

 

Upendo walionesha wafungwa na mahabusu nilitamani kunendelea kubaki lakini kamishna asingeniruhusu kwani wafungwa walikuwa wachangamfu na kuonesha upendo mkubwa mpaka nikajiuliza kweli hawa wanamakosa alieleza Askofu Nzigilwa

 

 Aidha amebainisha taswira ambayo jamii imekuwa nayo katika watu walioko magerezani sio kile ambacho kinafanyika na kutendeka ndani wafungwa na mahabusu wanaishi kwa upendo na amani.

 

Kwa upande wake paroko wa familia takatifu mburahati na mkurungezi wa utume walei jimbo kuu la Dar es salaam amesema kuwa shughuli waliyo ifanya ni ya huruma ya mungu na nikama tumekuja kumuona kristu kwani naye alikuwa mfungwa kama maandiko yanavyosema.

 

“siku hii tumejifunza mengi tumeona wafungwa walivyo na mahusiano mazuri na wafungwa lakini zaidi tunahitajika kuwasamehe ili watakavyo rudi huku waone kama wamepokelewa na jamii”

 

Kama wafungwa wana nafasi kubwa pia ya kujirekebisha tabia zao ndiyo neno la mungu linasema kumpokea mwana mpotevu ni kumsamehe unapomsamehe basi anarudi katika familia ya mungu na sisi tuwasamehe  na kuwaombea zaidi alibainisha paroko wa mburahati.

 

“ufungwa tunaouzungumzia hapa ni ufungwa wa kimwili kwamba unakosa uhuru  lakini pia tuna ufungwa wa kiroho  ambao ndio mkubwa zaidi cha msingi ni kujua mungu hataki nini na wanadamu awataki nini kwahiyo ukiongozwa na maneno ya mungu kila mmoja anaweza kwenda gerezani lakini gareza kubwa ni la kiroho”

 

Katika adhimisho hilo la huruma ya mungu kwa wafungwa na mahabusu lakini pia walei walishiriki kikamilifu pamoja na viongozi wengine wa dini katika magereza mbalimbali ikiwamo gereza la Segerea,Ukonga,Keko,Wazo,Mvuti na Kimbiji.

 

 

 

 

 

Read more...

MONSINYORI MBIKU- WAKATOLIKI TANZANIA ISHINI KWA UMOJA NA UPENDO

 

Na Bruno Bomola

 

Monsinyori deogratius mbiku amewataka waamini wa kanisa katokiki  kuishi imani ya kikristu na kupendana na kuwa na mshikamano na kuimarishana kiroho.

 

Amesema kuwa sakramenti ya kipaimara ni pentekoste  nani njia ya kuwaimarisha waamini kiroho na kumkiri yesu kristu hivyo kila aliyepata sakramenti ya kipaimara ana deni la kumtangaza kristu.

 

Monsinyori deogratius mbiku ameyasema hayo katika adhimisho la misa ya kipaimara katika parokia ya yombo vituka ambapo zaidi ya vijana 69 waliweza kuimarisha ikiwa ni idadi ndogo ikilinganishwa na roho mtakatifu alivyo washukia wafuasi wa yesu 120 wakati wa pentekoste.

 

“mapaji yale yale nguvu ile ile ya roho mtakatifu aliyowashukia wafuasi wa yesu ndi leo wana vituka roho mtakatifu anawashukia na mapaji yake saba lakini leo hata kuja kwa ishara ya nje ya ndimi za moto”

 

Monsinyori mbiku amewataka waimarishwa hao kuwa askari hodari wa kanisa katoliki kwani wanatakiwa kutenda yale yanayompendeza mungu na kuwa dira katika maisha ya kila siku.

 

Rais wetu anasema hapa kazi tu kauli hiyo sio ya mchezo mmempokea roho mtatifu mnatakiwa kufanya kazi mungu atakuja kuwauliza mlitumiaje karama na mapaji niliyo wapa alisema monsinyori

 

Katika adhimisho hilo la misa takatifu lililopambwa na utoto wa mtakatifu walio valia nadhifu mavazi ya malaika wakiwa na mwonekana kama malaika kuonesha kwamba siku hiyo ni ya kipekee katika parokia hiyo na kuonesha kwamba upendo upo ndani yao.

 

Sanjari na hayo katika adhimisho hilo la kipaimara kwaya ya sharikisho iliyozijumiuisha kwaya zote za parokiani vituka ili kuwa ikifanya kazi ya uinjilishaji kwa kuimba nyimbo mbalimbali za kusifu na kumshukuru mungu huku kinanda kikipigwa na yohane limilah.

 

Kwa upande wa mmoja wa waamini walioudhuria katika misa hiyo aliyejitambulisha kwa jina la joyce amesema kuwa wazazi wasizembee kuwaongoza vijana hao katika safari ya kumtumikia mungu.

 

“wazazi tulio wengi tukihakikisha mtoto amepata kipaimara basi tuna mwacha ajiongoze mwenye hapo ndipo tunapokosea na watoto ndipo wanapoli hasi kanisa jukumu la mzazi ni kumlea mtoto katika njia ipasayo”

 

Aidha joyce amewataka pia wasimamizi wa vijana waliopata sakrameti hiyo kuhakikisha wanaacha kazi na kuwalea vijana hao ili kuweza kutimiza malengo na makusudi ya mungu kwa kuwalea ndani ya kanisa la kristu.

 

“wazazi wamekuwa wakichagua wasimamizi wa kuwasimamia watoto wao ila bado awajatafakari je msimamizi yupi sahihi kila mtu akifata kile alichoitiwa na mungu hata swala la vijana kukosekana kanisani halitakuwepo”

 

 Kupata kipaimara siyo kuhitimu ukristu bali ni moja ya safari ya kumtangaza kristu hivyo kipaimara ni silaha ya kupambana na shetani kwa kusali na kumuomba roho mtakatifu.

 

Read more...

Ukweli na Hija ni Muhumu

 

Na Editha Mayemba

 

Kukiri udhaifu kuna maana kubwa sana. Unapokiri una maana kuwa upo tayari kubadilika na kuacha yale uliyokuwa ukiyafanya awali, iwe ulikuwa ukiyafanya kwa makusudi, kwa kujua au kutokujua ukweli au pengine kwa mazoea.

 

Inapotokea tukio la kukiri udhaifu wa kiutendaji kufanywa na kiongozi wa Kanisa ina kuwa na maana zaidi kwa mwamini kwa kuwa wengi wanaamini viongozi wa Kanisa, hawakosoi, na hata wakikosea hawakosolewi na wakikosolewa basi wanarekebisha kwa siri siri bila kukiri waziwazi.

 

Hii imetokea hivi Karubuni wakati Mkurugenzi wa Uchungaji Jimbo Kuu la Dar es Salaam Padri Joseph Matumaini alipokiri kuwa, mwamko duni wa waamini kufanya hija katika maeneo matakatifu unatokana na idara yake kuwa na upungufu.

 

Padri Matumaini anakiri udhaifu huo wakati Tumaini Letu lilipotaka kujua yeye kama kiongozi wa Idara ya uchungaji anadhani ni kwa nini waamini wengi hawahamasiki kwenda hija licha ya wengine kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha na nafasi wanayo na anadhani nini kifanyike kuwahamasisha.

 

Anasema moja ya upungufu katika idara hiyo ya kichungaji ni kutovitumia vema vyombo vya habari vya Kanisa kama Radio, Televishen na gazeti kutoa taarifa za kuwepo kwa hija pamoja na kutozitumia vizuri Parokia ili zihamashishe.

 

Padri Matumaini anasema amebaini kuwa siyo kwamba waamini hawana fedha za kuwawezesha kwenda hija katika maeneo matakatifu kama vile Nchi Takatifu, Lurds, Roma, na maeneo mengine ila sababu ni kutopata taarifa au kupata taarifa kwa kuchelewa.

 

Anasema kwa muda mrefu Idara imekuwa haitumii vyombo vya habari kuhamashisha kuwepo kwa hija, hali iliyosababisha watu wachache kupata taarifa hizo huku wengine.

 

Anakiri kuwa kwa mfano Hija ya Israel, Roma na Lurds iliyofanywa hivi karibuni na baadhi ya waamini wamepata taarifa za kuwepo kwa hija siku tatu kabla ya safari kufanyika huku wengine wakiwa hawana taarifa kabisa.

 

Katika mazingira ya namna hiyo hata kama mtu anao uwezo wa kifedha wa kugharamia safari yake ya Hija, hawezi kwenda kwa kuwa amechelewa kitu ambacho kinaweza kisimuhamsishe wakati mwingine kufanya hivyo.

 

Hata hivyo, Padri Matumaini, baada ya kukiri udhaifu huo anasema Idara yake inajipanga kuweka mkakati maalum kwanza kuhakikisha vyombo vya habari vya Kanisa vinatumika ipasavyo lakini pia kuhakikisha maparoko katika Parokia zote wanapata taarifa za kuwepo kwa hija mapema ili wawe wahamasishaji wa kwanza.

 

Anasema kwa kuanzia, idara hiyo itavitumia vizuri vyombo vya habari vya Kanisa kutoa matangazo ya Hija katika nchi Takatifu inayofanyika Mwezi Desemba kila Mwaka ili kila atakayesikia, kutazama na kusoma ahamasike na idadi ya mahujaji iongezeke.

 

Anasema kutokana na udhaifu uliokuwemo licha ya kambwa Hija iliyofanyika Roma, Lurdi na Israel, ilikuwa ni wazi kwa kila mwamini kutoka majimbo yote ya Kanisa Katoliki, ni mahujaji 59 pekee ndiyo waliojitokeza.

 

Kundi la kwanza la Mahujaji hao lilijumuisha Mahujaji 37 akiwemo Askofu Msaidizi wa Jimbo hilo Mhashamu Eusebius Nzigilwa, ambapo limehiji huko Roma, Italia na Lurdi, Ufaransa.

 

Kundi hilo lililojumuisha watawa watatu lilikuwa na Mapadri watano ambao ni Padri Joseph Matumaini, Padri Paul Haule, Padri Vitalis Kasembo, Padri Timothy Nyasulu na Padri Nicholaus Masamba wote wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

 

Anasema pamoja na nia kuu ya kufanya hija, lilipelekwa ombi maalum la kushiriki Misa takatifu pamoja na Baba Mtakatifu Fransisko iliyopangwa kufanywa Septemba 4 ikiwashirikisha Askofu Nzigilwa pamoja na Mapadri hao.

 

Kundi la pili lilokwenda Israel limepata mahujaji 21 tu, wakiwemo watawa wawili na Mapadri watatu ambao ni Padri Edwin Kigomba aliyekuwa Mkuu wa Msafara pamoja na Padri George Mkonogumo kutoka Jimbo la Rukwa, Padri Phocas Masawe-OSS.

 

Read more...

Watoto wa kike wanaohitimu elimu ya msingi wasiozeshwe

 

Na Frida Manga

Wanafunzi wa darasa la saba nchini wamefanya mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi, ikiwa ni kujiandaa na masomo ya kidato cha kwanza.

 

Bila sahaka ni hatua nzuri na ndefu waliyopitia watoto wetu na hatimaye hii leo watakamilisha ungwe hiyo na kujiweka tayari kwa elimu zaidi kwani bado wanasafari ndefu ya maisha katika kupata elimu.

 

Licha ya kwamba hatua hiyo inaweza kuonekana ndogo machoni pa watu kwa kuwa kile walichokipata hakiwasaidii katika kujitegemea kimaisha lakini ukweli utabaki kwamba vijana hawa wamepitia changamoto mbalimbali hasa kwa upande wa watoto wa kike.

 

Ni dhahiri kwamba wanahitaji pongezi kwa hatua hiyo na sasa ni jukumu la wazazi na walezi kuwaanda kwa ajili ya kwenda kidato cha kwanza hapo mwakani.

 

Nasema hivi kwa kuwa tumeshuhudia mabinti wanaomaliza darasa Saba wakikatishwa masomo yao ya juu na wazazi ama walezi kwa sababu mbalimbali lakini kubwa ikiwa ni kuwapeleka kutumika katika majumba ya watu kama wadada wakazi ama kuwafanyia mila na desturi potofu na kisha kuwaozesha katika umri mdogo.

 

Tumeshuhudia idadi ya wanahitimu kuwa nyingi kinyume na ile wanaokwenda kunza kidato cha kwanza, na kisingizio kikubwa kwa wazazi ni kwamba watoto wao wamefeli jambo ambalo binafsi si kubaliani nalo kwani naaishi katika imani kwamba kufeli darasa la saba si kwamba kunamzuia mtoto kwenda sekondari.

 

Pia naamini kwamba katika kuhitimu elimu ya msingi wapo wanaopata bahati ya kuchanguliwa kwenda kidato cha kwanza na wapo wanaokosa nafasi hiyo hivyo haiileti maana kwamba wakipelekwa shule binafsi watashindwa kuendelea na masomo yao ama kufikia malengo yao ya baadae isipokuwa ni nikuwanyima haki ya kupata elimu na kufikia malengo yao ya baadaye.

 

Mtazamo wangu ni kwamba huu ni muda muafaka kwa wazazi na walezi kukaa chini na kuzungumza na watoto wao kuona ni namna gani wanajianda kwa ajili ya masomo ya juu.

 

Zipo baadhi ya mila potofu ambazo licha ya makatazo mbalimbali ya Serikali zimeendelea kufanyika kwa siri ambazo wazazi ama walezi hupenda kufanya mambo hayo katika kipindi hiki ambacho wamemaliza elimu ya msingi.

 

Wengine wamewajengea watoto wao kwamba hawatafanya vema katika masomo yao na hivyo kuwajenga kisaikolojia kwamba ajiweke tayari kwenda kufanya kazi za ndani majumbani kwamba anaonekana hana uwezo wa akili hivyo hawezi kuendelea na Elimu ya juu.

 

Waswahili wanamisemo mingi yenye kujenga na kutuonyesha kwamba licha ya kwamba njia hii imeshindikana basi tunaweza tafuta njia nyingine kwa ajili ya kupata ufumbuzi na ndiyo maana wanasema “Kuvunjika kwa Jamvi Siyo Mwisho wa Mazungumzo”.

 

Wazazi na walezi wanapaswa kujipanga sasa na si kusubiri matokeo yatoke ndipo waaze kuhangaika, mkazo uwe kwamba lazima Watoto wanaohitimu darasa la saba wanapata nafasi ya kuendelea na masomo ya juu hata kama si kwenda Sekondari lakini vipo vyuo vya ufundi ambavyo ikiwa mzazi atazungumza na mwanae anaweza famu mapema upi mwelekeo wa mtoto wake.

 

Nionavyo mimi si muda wa wazazi au walezi kupanga namna ya kuwaozesha mabinti zao bali ni muda wakukaa na kujipanga kuona ni njisi ngani wanavyoweza kuwasaidia kuwenda mbele katika masomo yao hata kama watakuwa hawakuchanguliwa kwenda shule za Serikali.

 

Umaskini unatajwa kuwa kigenzo cha wazazi ama walezi kuwakatisha watoto wao masomo na kuwaozesha kwa madai kuwa hawana uwezo wa kuwapeleke Kidato cha Kwanza na hivyo wanakila sababu ya kuwaozesha jambo ambalo si kubalini nalo hata kidogo.

 

Nasema kuwa si kubaliani nalo kwani sera ya Elimu bure imetoa fursa kwa wazazi kuhakikisha kuwa watoto wanakwenda shule kwani jukumu lao ni kuchangia mahitaji muhimu kwa mtoto si kuwaza swala la Karo.

 

Pia suala la ndoa za utotoni mara nyingi linahusishwa na sababu za kiuchumi kwani binti anapoozeshwa inakuwa tayari amepunguza mzigo wa matumizi ndani ya familia.

 

Kwa mujibu wa taarifa ya umoja wa Afrika kiasi cha mabinti milioni 14 barani humo huolewa kila mwaka wakiwa na umri mdogo na nyingi ya ndoa hizo zikiwa ni za kulazimishwa na wazazi wao.

 

Ndoa za utotoni zinakwenda kinyume na haki za binadamu na kumnyima haki ya kuwa na afya bora mtoto wa wa Kike ikiwa ni pamoja kumnyima haki ya kupata elimu na kuwa na uhuru wa maisha yake ya baada.

 

Mbali na kwamba serikali imeweka mkazo wa kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wanaomaliza Darasa la Saba wanapata fursa kwenda Kidato cha kwanza, lakini ikiwa kama hatapata fursa ya kuchanguliwa ni vema ikaeleweka wazi kwa Wazazi kutafuta njia nyingine na kuhakikisha  kuwa watoto wao wanakwenda Kidato cha Kwanza.

 

Ni vema visingizio vya kuwa hakufanya vyema kwenye masomo yake au hakuchanguliwa vikawekwa pembeni na badala yake ni wakati mzuri kwa wazazi na walezi kutumia kipindi hiki kwa maandalizi ya kuwaweka watoto wao tayari kiali kwenda kidato cha kwanza.

 

Mazazi anatajwa kuwa Mwalimu wa tatu kwa mtoto wa Kwanza akiwa Mwalimu wake wa shule wa pili mtoto mwenyewe na watutu ni mzazi, sasa wakati umefika kwa Wazazi kutumia nafasi hiyo kumjenga mtoto kisaikolojia hata kama anaonekana hana mlengo kwa kwenda shule unaweza mtayarisha kwa ajili ya Elimu ya Ufundi.

 

Wazazi na walezi wenye watoto wanaohitimu shule msingi tumieni kipindi hiki kuwatayarisha watoto kwa ajili ya Elimu ya Sekondari na si vinginevyo.

 

End

 

Read more...

Kard. Pengo ataka waamini kumzawadia Kristo Parokia mpya tano

Na Gaudence Hyera

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar Es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka Waamini wa Jimbo hilo kumzawadia Bwana Yesu  Kristo Parokia mpya tano ili Jimbo lifikishe Parokia 105 kabla hajastaafu mwaka 2019. 

Alisema hayo katika mahojiano maalum na Kituo hiki kuhusu siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake itakayofanyika Ijumaa hii Agosti 5 ambapo atakuwa anafikisha umri wa miaka Sabini na miwili(72).

Kardinali Pengo alibainisha kuwa miaka mitatu ijayo atakuwa na umri wa miaka sabini na mitano na kwa mujibu wa sheria za Kanisa Katoliki anatarajia kuandika barua ya kuomba kustaafu kwa Baba Mtakatifu.

Alisema atakuwa mwenye furaha zaidi endapo Jimbo hilo litamwongezea Mwokozi zawadi ya Parokia tano katika kipindi cha miaka mitatu ijayo kabla hajastaafu madaraka ya Askofu Mkuu.

Alimshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai na baraka ya kuwa kati ya Makuhani hata kufikisha miaka 45 ya Upadri, miaka 32 ya Uaskofu, Miaka 26 Askofu Mkuu na miaka 18 ya Ukardinali.

Kardinali Pengo aliwashukuru Mapadri, Watawa, Waamini na watu wote wenye mapenzi mema ambao kutokana na ushirikiano wa kwa Neema na huruma ya Mungu ameweza kufikia umri huo.

Aliongeza kuwa Mwenyezi Mungu anapotoa baraka anakuwa na madai kwa yule aliyemjalia baraka hivyo anamshukuru sana kwa kumwezesha kutekeleza majukumu yake ya kuliongoza Jimbo hilo.

Kardinali Pengo alizaliwa Agosti 5, 1944 katika Parokia ya Mwazye, Jimbo Katoliki la Sumbawanga, aliingia Seminari ya mwanzo ya Karema mwaka 1959 hadi 1964 na baadaye Seminari ya Kaengesa 1959 hadi 1964.

Alijifunza Falsafa katika Seminari Kuu ya Kipalapa, Tabora Mwaka 1965/67, Teolojia 1968/71 na elimu ya Dini kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda.

Alipewa Daraja Takatifu ya Upadri na Hayati Askofu Karolo Msakila katika Parokia ya Mwazye Juni 20, 1971 na kuteuliwa kuwa Katibu wa Jimbo hadi Julai mwaka 1973 alipotumwa Roma kwa Masomo ya Juu ya Teolojia ya Maadili.

Desemba mwaka 1977 hadi 1983 alitumwa na Maaskofu kuwa Gombera mwanzilishi wa Seminari Kuu ya Mtakatifu Karoli Lwanga, Segerea Jimbo Kuu Katoliki la Dar Es Salaam.

Aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Nachingwea Novemba 11, 1983 na kuwekwa Wakfu Januari 6,1984 na Baba Mtakatifu mwenyewe(Mtakatifu YOHANE Paulo IIII) Roma na kusimikwa Februari 19, 1984.

Oktoba 17, 1986 aliteuliwa kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo la Tunduru-Masasi hadi Januari 22,1990 alipoteuliwa kuwa Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam akiwa na haki ya kurithi.

Baada ya kustaafu kwa aliyekuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo hayati Kardinali Laurian Rugambwa, alisimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Julai 22, 1992.

Januari 18, 1998 saa 8:00 adhuhuri alitangazwa kuwa Kardinali wa Kanisa Katoliki ambapo Februari 21 mwaka huohuo alitawazwa kwenye adhimisho lililoongozwa na Mtakatifu Yohane Paulo  II katika Kanisa Kuu la Mtakatifu PETRO, huko Roma. 

Wakati huo  huo, Umoja wa Marafiki wa Tumaini Media-UMTUME umempongeza Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar Es Salaam Mwadhama POLYCARP Kardinali PENGO kwa kutimiza miaka 72 ya kuzaliwa Agosti 5, 2016.

Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Baraza anzilishi la Umoja huo PETER SAKIA MACHA alipokuwa akisoma risala ya UMTUME wakati wa hafla ya Upashanaji habari iliyofanyika Dominika ya Agosti 7, katika Parokia ya Mtakatifu PETRO,Oysterbay.

MACHA alisifu jitihada kubwa zilizofanywa na Kardinali PENGO katika kipindi chote tangu alipoanza kuwa mchungaji mkuu wa Jimbo hilo hadi hivi sasa.

Aliongeza kuwa uwepo wa marafiki wa Tumaini Media pia ni tunda la juhudi za Mwadhama ili kuhakikisha Vyombo vya habari vya Tumaeini Media vinafikia malengo yaliyokusudiwa.

Historia fupi ya Alipoanzia Kardinali Pengo

Kumbukumbu zinaonesha kuwa Kardinali PENGO alisimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo Julai 22 Mwaka 1992 baada ya kustaafu kwa mtangulizi wake Hayati Kardinali LAURIAN RUGAMBWA.

Wakati huo Jimbo lilikuwa na Mapadri wazalendo wafuatao; Monsinyori DEOGRATIAS MBIKU, Marehemu Padri VALERIAN FATAKI na JUVENALIS MUBA, Padri STEFANO NYILAWILA na Padri CAMILLIUS LUAMBANO.

Wengine ni Padri VENANCE TEGETE, Padri GEORGE SAYI, Padri Padri BENEDICT SHAYO na Padri PAUL HAULE ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Tumaini Media.

Mapadri wengine wakati huo walikuwa ni kutoka Majimbo mbalimbali likiwemo Jimbo la Bukoba na wamisionari kutoka mashirika mbalimbali waliokuwa wakiwezesha kazi za kichungaji Jimboni humo.

Parokia zilizokuwepo wakati Kardinali Pengo anaanza kazi ya Mchungaji Mkuu wa Jimbo hilo ni pamoja na Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosef(1889), Mtakatifu Fransisko wa Asisi Pugu(1889), Bikira Maria wa Fatima, Msimbazi(1952) Mt. Antoni wa Padua, Mbagala(1954), Mt. Petro,Oysterbay, Mt. Fransisko Ksaveri Chang’ombe(1960) na Wat. Mashahidi wa Uganda, Magomeni(1965).

Parokia nyingine ni Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu, Kawe(1968), Maria Imakulata, Upanga(1968), Mt.Agustino, Chuo Kikuu(1968), Mt.Maurus, Kurasini(1970), Mt. Agustino, Ukonga(1971), Mt. Martin de Pores Mwananyamala na Mt. John Bosco,Kibaha(1972).

Nyingine ni Mt. Paulo Mtume,Ubungo(1973), Mt.Gaspar, Tegeta(1973), Bikira Maria Consolata,Kigamboni(1973), Familia Takatifu, Mburahati(1974), Moyo Mt. wa Yesu,Manzese(1978), Mt.Maximilian Maria Kolbe,Mwenge(1985), Kristo Mfalme, Tabata na Bikira Maria Mapalizwa, Kibiti(1987).

Ikumbukwe kwamba kati ya Parokia hizo zipo zile zilizoanzishwa na Maaskofu wamisionari waliotangulia akiwemo Hayati Cassian Spies, Ofm Cap, Askofu Mkuu wa kwanza wa Jimbo hilo Hayati Edgar Marantha na baada ya mwaka 1969 Hayati Kardinali Rugambwa.

 

Read more...

Waziri azindua mpango kuboresha elimu Ngara

Na Mwandishi Wetu, Ngara

WANANCHI wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera waishio jijini Dar es Salaam na kwingineko wameshiriki harambee ya kwa ajili ya kuboresha elimu ya msingi kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa ujumla.

Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Walemavu, Jenester Mhagama ameshiriki harambee hiyo kama mgeni wa heshima ilifanyika Julai 30 mwaka huu katika Ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo walihudhuria Mkuu wa Wilaya hiyo, Luteni Kanali Michael Mntenjele, na Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Aidan Bahama.

Viongozi wengine wa wilaya hiyo waliohudhuria ni Mbunge wa  Jimbo la Ngara, Alex Kashaja, Mwenyeki wa Halmashauri ya Wilaya, Eric Ntamachumu na Afisa Elimu wa Shule ya Msingi katika wilaya hiyo, Gedion Mwesiga.

Harambee hiyo ilizinduliwa na Waziri Mhagama kwa kauli mbiu ya “Ondoa Jiwe Darasani na Weka Dawati” na kupelekea kufanikiwa kuchangisha fedha taslimu kiasi cha Shilingi  3,410,000 na hundi mbili zenye thamani ya Shilingi 2,000,000 na pia kupata jumla ya madawati 631.

Hata hivyo, mafanikio ya harambee hiyo yalitokana na Kamati ya Umoja wa wana Ngara waishio nje ya Ngara na marafiki wapenda maendeleo ya wilaya hiyo iliratibu harambee ya uchangiaji wa madawati, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mabamba Tumaini, Makamu Wenyeviti, Prophetess Adriana Batakanwa na Meshack John, na Katibu wake, Asheri Majanja, pamoja na wajumbe wake, Philotea Ruvumbagu, Pius Kaheshi, Adace Semitende, Peter Ngoti na Eddie Komeza.  

Katika kuzindua operesheni hiyo, Mhagama alitoa wito kwa wananchi wote wa Ngara wanaoishi nje ya wilaya hiyo kushiriki katika kuboresha elimu ya shule ya msingi wilayani humo kwa kuchangia madawati. Kwani alisema madawati ni moja ya nyenzo muhimu katika kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi kujifunza masomo vizuri.

“Kama kauli mbiu inavyosema ondoa jiwe darasani na weka dawati ndivyo nanyi wana wa Ngara mnavyotakiwa kufanya leo katika kuondoa upungufu wa madawati 3,000,” alibainisha mgeni rasmi wa harambee ya kuchangia madawati.

Akitoa ufafanuzi wa upungufu wa madawati hayo, Mwesiga alieleza kuwa mahitaji ya madawati kwa shule zote za msingi ni 240,606 ambapo thamani ya kila dawati ni Shilingi 70,000.00.

Afisa elimu huyo alidokeza wananchi walihamasika kuchangia na kupelekea kubakia madawati 3,669 hadi mwishoni mwa Juni mwaka huu.

“Taarifa nilizopata punde, idadi hiyo imeshuka na sasa tuna upungufu wa madawati 2,119 ambapo kila dawati ni Shilingi 70,000,” alibainisha Mwesiga.

Katika harambee hiyo, Mhagama alichangia madawati 15 na pia Waziri wa Elimu na Ufundi, Dk. Joyce Ndalichako akachangia madawati 15, huku Mbunge Kashaja akiahidi kuchangia madawati 30 na fedha taslimu kiasi cha Sh. 1,500,000.00.

Katika kutoa mchango wake, Kashaja alieleza kuwa Wilaya ya Ngara ina changamoto nyingi kutokana na kupakana na nchi mbili za Rwanda na Burundi.

Alipendekeza kuwepo Kamati ya Ushauri yenye wajumbe kumi katika kukabili changamoto hizo na uwezekano wa kuwa na ofisi ndogo ya Jimbo la Ngara jijini Dar es Salaam. 

Pg 13 Falsafa, Dhana na umuhimu wa mbio za Mwenge nchini

Na Mwandishi Maalum

Historia ya nchi yetu ni pana na ya kuvutia kwa namna ya pekee ukilinganisha na nchi nyingi za Afrika na Duniani kote.

Upekee huu unatokana na uwezo wa kujenga hoja na uadilifu wa viongozi wetu, hasa mwasisi wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipochaguliwa kuwa mjumbe kwenye Baraza la kikoloni la kutunga Sheria (Tanganyika Legislative Council) mwaka 1958.

Kwa kuwa Mwalimu alikuwa na ndoto ya kuiona Tanganyika na Afrika iliyo huru, mwaka 1958 katika hotuba yake ya kwanza alitamka maneno ya kifalsafa kwa wajumbe na Spika wa Baraza la kikoloni la kutunga Sheria kwa kusema:

 “Sisi tunataka Uhuru wa Tanganyika, Mkitupatia tutauwasha Mwenge wa Uhuru na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike ndani na nje na mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki na heshima palipojaa dharau”.

Maneno haya aliyarudia tena mwaka 1959 alipohutubia kikao cha 35 cha Baraza la Umoja wa Mataifa kama Mbunge mwakilishi pekee wa Tanganyika.

Falsafa hiyo ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilikuwa ni kiashiria kikubwa kwa Waingereza kwamba watu wa Tanganyika wamechoka kutawaliwa. Siku Tanganyika ilipopata Uhuru tarehe 09 Desemba, 1961.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliuwasha Mwenge wa Uhuru na akamkabidhi Luteni Alexander Ngwebe Nyirenda na kikosi cha Vijana wenzake wakaupeleka Mwenge wa Uhuru juu ya Mlima Kilimanjaro.

Mwalimu wakati akitoa hotuba ya siku ya Uhuru; aliwatangazia Watanganyika, Afrika na Dunia kwa ujumla kwa kusema:

 “Sisi tumekwisha uwasha Mwenge wa Uhuru na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike ndani na nje ya mipaka yetu, ulete matumaini pale ambapo hakuna  matumaini, ulete upendo mahali penye chuki na heshima mahali palipo jaa dharau”.

Luteni Alexander Nyirenda alipandisha Bendera na Mwenge wa uhuru juu ya mlima Kilimanjaro usiku wa kuamkia tarehe 9 Desemba mwaka 1961 ambapo baada  ya  Uhuru wa Tanganyika na kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru,  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na viongozi wenzake wa awamu ya kwanza walielekeza juhudi zao katika kuwaunganisha Watanzania na kuweka misingi imara ya kulijenga taifa huru la Tanganyika; kudumisha amani, upendo, umoja, mshikamano na kuweka sera za kukabili  maadui ujinga, umaskini na maradhi.

Awamu hii  ilitafsiri falsafa ya Mwalimu aliyoijenga katika Mwenge wa Uhuru kwa kuweka  misingi madhubuti ya uhusiano wa nje, sera ya kutofungamana na siasa za upande wowote, na kuweka msisitizo mkubwa katika ukombozi wa Bara la Afrika na mapambano dhidi ya ubeberu na vibaraka wao. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Azimio la Arusha lililosisitiza siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, na kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni matunda ya utelekezaji wa Falsafa ya Mwenge wa Uhuru.

Mara baada  ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964, Tanganyika iliungana na Zanzibar na kupata Taifa moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Haya ni mafanikio makubwa katika kutekeleza falsafa ya Mwenge wa Uhuru kwani Wazanzibar walirejeshewa matumaini yaliyokuwa yametoweka chini ya utawala wa Kisultani.

Hata baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964, falsafa yaMwenge wa Uhuru iliendelezwa kwa kuukimbiza Mwenge wa Uhuru katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kujenga na kuimairisha misingi ya amani, umoja, uzalendo, upendo, mshikamano na kuhamasisha shughuli za maendeleo katika jamii zetu na kupeleka kwa Watanzania wote ujumbe maalum uliokusudiwa na Serikali kila mwaka.

Aidha, Mwenge wa Uhuru ni chombo pekee tulichonacho kama taifa cha kuwaunganisha Watanzania na kuwa wamoja kwani haufungamani na itikadi za kisiasa, makabila yetu wala Dini zetu. Mwenge wa Uhuru ni mali ya Watanzania wote.

Kwa nini Mwenge wa Uhuru husimamiwa na Serikali

Hadi mwaka 1992, Mbio za Mwenge wa Uhuru zilikuwa zikisimamiwa na kuratibiwa na Chama Tawala.   Baada ya nchi yetu kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992; mwaka 1993 Mbio za Mwenge wa Uhuru zilianza kusimamiwa na Serikali chini ya Wizara yenye dhamana na Maendeleo ya Vijana. 

Mabadiliko hayo yalikuwa ni kiashiria kikubwa kwa watanzania wote kwamba Mwenge wa Uhuru hauna Chama, hauna kabila na hauna dini isipokuwa ni  kwa ajili ya kujenga na kudumisha umoja wa kitaifa. Kwa sasa Mbio za Mwenge wa Uhuru zinaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Zanzibar.

Aidha, rasilimali fedha kwa ajili ya uendeshaji wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa hutolewa na Serikali na hutengwa na Wizara zenye dhama na kupitishwa na Bunge la bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwaka wa fedha husika.

Tangu Mbio za Mwenge wa Uhuru ziasisiwe hadi leo, misingi na madhumuni ya Mwenge wa Uhuru na Mbio zake zimeendelea kuwa zenye manufaa makubwa na zitaendelea kurithishwa vizazi hadi vizazi katika taifa letu.

Faida na Mafanikio ya Mwenge wa Uhuru Kitaifa na Kimataifa.

I.  Mwenge wa Uhuru umekuwa ni chombo muhimu cha kujenga undugu, umoja, mshikamano na kudumisha amani pote unapopita bila kujali itikadi zetu za kisiasa, dini wala makabila yetu. Umuhimu huu unatokana na ukweli kwamba, leo hii tunahitaji kujenga Taifa lenye amani, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa kuliko wakati wowote ule ikiwa ni pamoja na kujenga taifa lisilokuwa na dhuluma, unyonge, rushwa, ubaguzi, ukabila, udini wala vitendo vya kifisadi.

II.  Mbio za Mwenge wa Uhuru zimeendelea kuhamasisha wananchi kwa kushirikiana na Serikali yao katika kubuni na kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo katika nyanja za kilimo, ufugaji, Uvuvi  endelevu, uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya, elimu, maji, umeme na huduma za jamii katika maeneo yote nchini na hasa katika maeneo yasiyofikika kiurahisi.

Kwa mfano, kwa mwaka 2015 pekee, miradi 1,342 yenye thamani ya Shilingi 463,519,966,467.77 ilizinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi. Kati ya fedha hizo, Shilingi 73,462,492,473. 62 zilitokana na nguvu za wananchi. 

Hata hivyo, michango yote inayotolewa na wananchi ni ya hiari na hutolewa baada ya wananchi kuhamasishwa na kufahamu umuhimu na matumizi yake ambayo ni kugharamia kwa miradi yao wenyewe.

III. Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa zikitumika kuelimisha wananchi katika maeneo yote nchini jinsi ya kupambana na maradhi yanayotishia ustawi wa watu wetu kama vile UKIMWI, Malaria na kupambana na matumizi ya Dawa za kulevya. Pamoja na njia nyingine tunazotumia kuwahamasisha wananchi wetu. Bado Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa ni njia sahihi ya kufikisha taarifa na elimu sahihi ya changomoto hizi kwa watanzania wote.

IV. Mbio za Mwenge wa Uhuru pia, zimeendelea kuhamasisha na kuimarisha umuhimu wa Muungano kwa watanzania wa pande zote mbili za nchi yetu.

V. Kimataifa, Mwenge wa Uhuru umeendelea kusimamia dhana ya na maudhui yake ya kumulika hata nje ya mipaka yetu. Kwani umeendelea kuhamasisha amani ndani ya Afrika Mashariki, Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika na Duniani kwa ujumla. Tanzania imeendelea kuwa msuluhishi wa Amani Afrika na mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine Duniani kote na imeshiriki ukombozi wa Bara la Afrika hasa kusini mwa Afrika na kusisitiza juu ya umoja, mshikamano, upendo na amani kwa mataifa hayo.

 VI.  Mwenge wa uhuru umeendeleza falsafa ya kumulika ndani ya mipaka ya taifa letu kwa kumulika uovu katika jamii ikiwemo uzembe, kutowajibika, vitendo vya rushwa na ufisadi katika miradi mbalimbali ya maendeleo na huduma za kijamii nchini.

VII.  Mbio za Mwenge wa Uhuru pia hutumika katika kuratibu na kutathimini shughuli mbambali za maendeleo zinazofanywa na wadau wa maendeleo na kukusanya taarifa zinazohusu kero za  wananchi ambazo husaidia Serikali katika upangaji na utelezaji wa mipango ya  maendeleo kwa wananchi wake.

 Dhana Potofu dhidi ya Mwenge wa Uhuru.

Pamoja na maono ya Baba wa Taifa, falsafa ya Mwenge wa Uhuru , faida na umuhimu wa Mwenge wa Uhuru ambao umeelezwa hapo juu, wapo watu wachache ambao huenda kwa sababu zao za kisiasa au maslahi yao binafsi wameamua kutumia nafasi zao na ushawishi wao kuupotosha umma wa Watanzania kwamba Mwenge wa Uhuru haufai kwa kutoa hoja  nyepesi (Cheap arguments). Hoja hizo hizo ni pamoja na:-

(i)      Falsafa ya Mwenge wa Uhuru haihitajiki sasa kwa Watanzania

Serikali kama ilivyoeleza hapo juu, inaendelea kusisitiza kuwa falsafa ya Mwenge wa Uhuru na maono ya Baba wa Taifa juu ya taifa hili bado yanaendelea kuishi japo yeye hatupo naye tena kwani ni dhahiri kuwa chombo hiki kinasaidia sana katika jitihada za kuwaunganisha Watanzania, kujenga umoja wa kitaifa, upendo, mshikamano, amani, uzalendo na kuchochea shughuli za maendeleo kote nchini. Kwa sasa Mbio za Mwenge wa Uhuru zinahitajika zaidi kwa lengo la kuhamasisha watu wetu kufanya kazi na kujiletea Maendeleo kama silaha ya kupambana na adui ujinga na umaskini.

(ii)     Michango wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.

Serikali ingependa ifahamike kwa wananchi kuwa, Mbio za Mwenge wa Uhuru zinaendeshwa kwa rasilimali fedha za serikali zinazopitishwa na Bunge. Aidha, pale inapohitajika, wadau kwa hiari yao, husaidia katika kugharamia machapisho ya ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru uliokusudiwa kama jitihada zao katika kuisaidia Serikali kufikisha ujumbe kwa wananchi wengi zaidi. 

Mbio hizi pamoja na dhana nyingine zilizofafanuliwa hapo awali, unawahamasisha wadau mbalimbali kushiriki na kuchangia kwa hiari shughuli za Maendeleo katika maeneo yao.

Michango ya wadau katika Halmashauri zetu hujumuisha nguvu za wananchi, Vifaa na fedha taslimu ambazo hutumika katika miradi wanayoibuni na kuitekeleza wenyewe. 

Lengo la kuwashirikisha wananchi katika miradi yao ya  maendeleo ni  kujenga  moyo wa kujitolea, uzalendo na utaifa kwa wananchi wetu ili  waweze kumiliki miradi inayoanzishwa na kujenga misingi ya uendelevu wa Miradi hiyo.

Mara nyingi, asilimia ishirini ya kila mradi unaowekewa jiwe la msingi, kuzinduliwa, au kufunguliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru ni sharti itokane na nguvu za wananchi. Serikali inaendelea kusisitiza kuwa, michango hiyo ni ya hiari na matumizi yake huwekwa wazi kwa wanachi kila mradi wakati wa kuzinduliwa au kuwekewa jiwe la msingi.

(iii) Mikesha ya Mbio za Mwenge wa Uhuru na maambukizi ya VVU/UKIMWI

Baadhi ya watu wachache wamekuwa wakidai kuwa, mikesha ya Mbio za Mwenge wa Uhuru inachochea vitendo vya ngono zembe vinavyopelekea maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI katika maeneo mbalimbali nchini. Serikali inapenda kufafanua jambo hili kuwa, Suala la mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI ni jambo linalopewa kipaumbele kikubwa katika Mbio za Mwenge wa Uhuru.

Tangu mwaka 2000 hadi sasa, ujumbe wa mapambano dhidi ya UKIMWI umefanywa kuwa ujumbe wa kudumu na uandaliwa kwa kushirikiana na Tume ya taifa ya kuthibiti UKIMWI (TACAIDS) na kisha kutolewa kwa ufasaha na vijana wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa kila mwaka katika Halmashauri za Wilaya zote zote nchini.

Lengo likiwa ni kuhakikisha maambukizi mapya ya VVU yanafikia asilimia sifuri katika jamii yetu. Katika kufanikisha azma hii, Mbio za Mwenge wa Uhuru huwafikishia wananchi wote nchini, taarifa sahihi kukusu VVU/UKIMWI kwa njia ya machapisho, sanaa kama vile maigizo, mashahiri na nyimbo, ushuhuda (testimony) kutoka kwa waathirika na hotuba za wakimbiza Mwenge kitaifa ambao huandaliwa na mamlaka husika kabla ya kunza mbio hizi.

Mbio za Mwenge wa Uhuru pia huhamasisha wananchi kupima VVU kwa hiari na kila siku, wastani wa watu 200 hadi 600 hujitokeza kupima VVU jambo ambalo ni nadra sana kutokea kwa watu wengi kujitokeza kupima VVU kwa wingi  katika program nyingine zinazolenga kuhamasisha upimaji wa VVU.

Mbio za Mwenge wa Uhuru pia hukemea tabia za unyanyapaa katika jamii, huhamasisha juu ya matumizi sahihi ya ARVs na kuwaelekeza wananchi jinsi ya kujikinga na maabukizi ya VVU. Hivyo siyo kweli kuwa mikesha ya Mbio za Mwenge wa Uhuru inachangia katika maambukizi ya VVU.

Ni vyema tukafahamu kuwa UKIMWI upo na tabia zetu hatarishi hasa za kufanya ngono zembe ndizo changamoto kubwa tunayotakiwa kuijadili kama Watanzania katika kupambana na ugonjwa huu wa UKIMWI na sio Mwenge wa Uhuru.

Mwenge huu unatusaidia kupambana na tabia zetu hatarishi ambazo ndizo zimekuwa kikwazo kikubwa katika jitihada za Serikali za kupambana na VVU/UKIMWI.

 Kutokana na umuhimu, dhana na falsafa ya Mwenge wa Uhuru kama ilivyoelezwa :-

· Serikali itaendelea kujenga mshikamano, umoja, upendo na kudumisha amani miongoni mwa Watanzania kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru.

· Serikali itaendelea kuutumia Mwenge wa Uhuru kuwahamasisha wananchi kupambana na maadui ujinga, maradhi na umaskini kwa watu wetu.

· Serikali itaendelea kuutumia Mwenge wa Uhuru kumulika, kufichua na kuchukua hatua dhidi ya watu au kundi la watu wanaojihusisha na vitendo vyote vinavyolihujumu Taifa ikiwa ni pamaoja na vitendo vya kibaguzi, rushwa, ufisadi, ubadhirifu, uzembe na chuki.

 Serikali inapenda kutumia nafasi hii kuwaomba watanzania wote kutambua kuwa, kila taifa lina chimbuko lake, utamaduni wake, na taratibu zake. Mwenge wa Uhuru utabaki kuwa ni chombo muhimu na alama ya Taifa letu.

Kama Taifa tutaendelea kushirikiana na kuenzi kazi na fikra za waasisi wa Taifa hili. Tushiriki katika shughuli za maendeleo kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru, tuusikilize ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru unapopita katika maeneo yetu, tuutafakari na kuufanyia kazi kwa vitendo kwa maendeleo ya Taifa letu.

Tujiepushe na biashara na matumizi ya Dawa za kulevya, vitendo vinavyosababisha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na tufanye kazi kwa bidii huku tukiendeleza mshikamo, umoja, upendo, amani na undugu wetu.

Serikali inatoa wito kwa Vijana ambao ndiyo nguzo ya Taifa, kudumisha chombo hiki kwa faida yetu sote na vizazi vijavyo. Hapa Kazi tu.

Read more...

Pg 2. Tamasha Tumaini Jipya laibua mazito

·       Serikali yapongeza, yaahidi kusimamia maadili mema nchini

·       Waamini, Wananchi wamiminika, waguswa na ujumbe mzito

Na Gaudence Hyera

Waamini na watanzania kwa ujumla wametakiwa kuendeleza moto wa maadili mema kwa maneno na matendo na kurekebisha mwenendo mbaya na maovu katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa jana na Balozi Mstaafu Paul Rupia aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye Tamasha la Tumaini Jipya lililoandaliwa na Kituo cha Tumaini Media na kufanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Aliwahakikishia watu wote, wazazi, Vijana na watoto walioshiriki Tamasha hilo kwamba yeye atakuwa Mhashasishaji mkubwa wa maadili bora kwa watu wote atakaokutana nao katika maeneo mbalimbali nchini.

Balozi Rupia  ambaye dhehebu lake ni la Anglikana amesema Taifa la Tanzania kwa sasa linapita katika wakati mgumu wa mmomonyoko wa maadili tofauti na ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.

Aliongeza kuwa wale waliopata bahati ya kuwa viongozi katika ngazi ya Taifa wanatokwa machozi wanaposikia ujumbe wa maadili mema unaotolewa na watoto na vijana kwa njia ya nyimbo.

Balozi Rupia alikipongeza Kituo cha Tumaini Media kwa kuwasha moto huo na wote walioshiriki kuandaa Tamasha hilo wakiwemo watoto na vijana ili kurekebisha maadili ya Taifa.

Aliwataka vijana na watoto kueneza moto uliowashwa kwa kuanza sasa kuyaishi maadili mema kwa kuwa wao ni Taifa la kesho hivyo wajiandae tangu sasa kuwa viongozi waadilifu wa Taifa lao.

Balozi Rupia aliwakumbusha vijana kuhusu Utandawazi na kwamba ndiyo umekuwa chanzo kikubwa cha kupotosha maadili mema hivyo wajiepushe na kuiga matendo yasiyofaa.

Amesisitiza kuwa amefarijika na ujumbe uliotolewa kwenye Tamasha hilo kwa njia ya nyimbo kuwa ni mzuri na amemtaka kila aliyeusikiliza aendelee kuueneza kwenye jamii anakoishi kwa manufaa ya Taifa.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel, katika ujube wake uliosomwa kwa niaba yake kwenye Tamasha hilo, amelipongeza Kanisa Katoliki kwa kushirikiana na Serikali kukemea vitendo viovu.

Alitoa pongezi hizo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa, Utamaduni na Maadili Hajaati Shani  kwenye Tamasha la Tumaini jipya.

Profesa Elisante alikishukuru Kituo cha Tumaini Media kwa ubunifu wa kuandaa Tamasha ambalo lengo lake ni kuhakikisha maadili mema na bora yanajengwa kwa manufaa ya watanzania wote.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Godfrey Ngereza aliwakumbusha waimbaji na Kwaya mbalimbali nchini kuhakikisha wanasajili kazi wanazorekodi kwa mujibu wa sheria za nchi.

Amekumbusha pia kwamba suala la maadili mema ni mtambuka na kwamba hata Bwana Yusu Kristo alilelewa na kukua Kiroho na Kimwili akimpendeza Mungu na Wanadamu.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Muleba-Kusini Mheshimiwa Profesa Aanna Tibaijuka alimshukuru Mkurugenzi wa Tumaini Media Padri Paul Haule kwa mwaliko wa Tamasha hilo.

Aidha aliongeza kuwa maadili mema ni lazima kwa kila Mtanzania na kwamba kila mmoja anatakiwa kusema ukweli ili kuyaenzi maadili mema kwa kuwa mtu hawezi kuwa mwadilifu kama ni muongo.

Profesa Tibaijuka alinukuu andiko la Mtakatifu Paulo kwamba “ Asiyefanya kazi na asile na kuwasihi Watanzania wapende kufanya kazi halali ili waweze kuishi maisha yenye maadili kimwili na kiroho.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini Media Padri Dk. Joseph Matumaini alimshukuru Mungu kwa ajili ya Tamasha la Tumaini Jipya na kuwatakia wote walioshiriki Afya ya mwili na Roho.

Amesema hayo jana wakati akifunga Tamasha hilo maalum kwa ajili ya kuhuisha maadili lililofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar Es Salaam na kuhudhuriwa na Watanzania wa Kada mbalimbali.

Padri Matumaini alishukuru Mgeni rasmi Balozi Paul Rupia, Viongozi wa Serikali, Mapadri na Watawa, Dini na Madhehebu, Waamini na watu wote wenye mapenzi waliounga mkono Tamasha hilo.

Aidha amezishukuru Kwaya, Vikundi na Waimbaji Binafsi ambao walikuwa tayari kwa maandalizi yao na jinsi walivyoweza kushiriki kuhamasisha kwa nyimbo zao ujumbe wa Maadili kwa Watoto na Vijana.

Awali akifungua Tamasha hilo Mkurugenzi wa Tumaini Media Padri Paul Haule alitoa shukrani za dhati kwa Serikali, Kamati ya maandalizi na Jumuiya ya Watanzania waliounga mkono Tamasha hilo.

Alisema lengo la Tamasha hilo ni ufunguzi na kuwa mlango wa Programu endelelevu yenye Kauli Mbiu “Maadili bora kwa Watoto na Vijana ni Faida kwa Taifa” itakayoendeshwa na Kituo cha Tumaini Media kupitia Redio,Televisheni na Gazeti Tumaini Letu.

Baadhi ya Kwaya zilizoshiriki ni Mtakatifu John Bosco kutoka Jimbo Katoliki la Bukoba, Mtakatifu Secilia kutoka Jimbo Kuu la Arusha, Mtakatifu Kizoto -Makuburi na Mtakatifu Maria Goreth -BMMH.

Waimbaji wengine ni Uinjilisti Kijitonyama, Canaan KKKT- Keko, Moyo Mtakatifu wa Yesu -Oysterbay, Ebeneza Karismatiki-Emaus, Utoto Mtakatifu-Mwenge, Evelyne Muthioka kutoka Kenya, Atosha Kisava na Joshua Mlelwa.

 

Read more...

Serikali yatenga mil. 900/-kuzalisha Dawa nchini • Idadi wagonjwa wa upasuaji waongezeka MOI

Na Ally Daud.

Serikali imetenga Shilingi milioni 900 kuzalisha dawa za binadamu katika viwanda vya ndani ili kufanya asilimia 80 ya dawa zinazoagizwa nje zipatikane nchini.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri ya Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA).

Ummy alisema kuwa Serikali imetenga fedha hizo kuhakikisha viwanda vya ndani vinatengeneza dawa hapa nchini na kupiga hatua katika uchumi wa viwanda.

 

 “Serikali kupitia wizara yangu tumetenga Shilingi milioni 900 kuzalisha dawa za binadamu katika viwanda vya ndani ili kufika uchumi wa kati kwa kutumia viwanda vyetu”,alisema Ummy.

Aidha Ummy alisema kuwa TFDA kwa kushirikiana na Serikali wanapaswa kuhakikisha viwanda vya ndani vinatengeneza dawa zenye ubora kwa matumizi ya binadamu ili kupunguza magonjwa yanayotokana na sumu za kemikali zitokananzo na dawa hizo.

 

Ummy aliongeza kuwa TFDA inatakiwa ishirikiane na Taasisi ya viwango nchini (TBS) ili kuzuia na kupiga marufuku bidhaa zisizokizi viwango na ubora unaopaswa kutumiwa na Watanzania.

Aidha Waziri Ummy alisema kuwa TFDA inatakiwa kutoa elimu ya kutosha kwa umma ili kuwawezesha watanzania kuepuka kutumia bidhaa zisizo na ubora kwa matumizi ya binadamu.

Mbali na hayo Ummy alisema TFDA inatakiwa kukusanya mapato kwa wingi zaidi ili kuendana na kasi ya Rais John Pombe Magufuli na kupiga hatua kiuchumi ili isaidie wananchi katika shughuli za maendeleo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TFDA, Balozi Dk. Ben Moses, alisema kuwa wamepokea maagizo yote yaliyotolewa na Waziri Ummy na watayafanyia kazi kwa haraka na ufanisi ili kuendana na kasi ya “Hapa Kazi tu”.

“Tumepokea maagizo ya Waziri na nataka kumuhakikishia kwamba tutaendelea na kasi yetu ili kuifikisha nchi yetu kwenye kilele cha maendeleo na Afya bora”, alisisitiza Dk. Moses.

 

Katika hatua nyingine, Lilian Lundo wa Idara ya Habari Maelezo anaripoti kuwa, idadi ya wagonjwa wa upasuaji katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) imeongezeka kutoka wagonjwa 20 mpaka wagonjwa 40 kwa siku.

Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa taasisi hiyo, Jumaa Almas aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya tuhuma zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa taasisi hiyo inabana matumizi na kusababisha msongamano wa wagonjwa taasisi hiyo.

Alisema asilimia 80% ya wagonjwa walio katika taasisi hiyo wanahitaji upasuaji wa dharura jambo ambalo limeilazimu taasisi hiyo kufungua wodi nyingine ya upasuaji ili wagonjwa wote wanaohitaji huduma hiyo waweze kufanyiwa ili kuokoa maisha yao.

“Msongamano wa wagonjwa MOI hausababishwi na kubana matumizi bali ni kutokana na kuongezeka kwa wagonjwa kutoka wagonjwa 20 mpaka wagonjwa 40 kwa siku ambapo kumesababishwa na ongezeko kubwa la ajali hasa za pikipiki katika jiji la Dar es Salaam,” alisema Almas.

Alifafanua kuwa wagonjwa wa upasuaji wa kichwa na ubongo hulazimika kusubiri kwa muda kutokana na pindi wanapopelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi mara baada ya upusuaji na kuongeza kuwa vyumba vya wagonjwa mahututi ni vichache ikilinganishwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wanaohitaji upasuaji huduma hiyo.

Amesema Taasisi hiyo inategemea kuongeza vyumba vingine zaidi kwa ajili ya wagonjwa mahututi ili kukidhi idadi ya wagonjwa ambao wamekuwa wakiongezeka kila siku. 

 

Akifafanua kuhusu usitishwaji wa kambi za upasuaji (surgical camps) zilizokuwa zikifanyika siku za mapumziko alisema kuwa kambi hizo zimesitishwa kwa muda mrefu kufuatia uamuzi wa Bodi ya wadhamini ya MOI baada ya bajeti ya kuendesha kambi hizo kuwa kubwa ikilinganisha na mapato na kuigharimu Taasisi hiyo kiasi cha shilingi milioni tano hadi sana kwa wiki.

End 

Read more...
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.