Menu
RSS

Tanzania na Brazil,zaingia makubaliano kilimo cha Pamba

MWANZA

Tanzania na Brazil zimeingia makubaliano ya kuinua kilimo cha zao la pamba ili kiwe na tija kwa wakulima nchini, wakati Brazil ikiwa katika hatua kubwa za kimageuzi ya kilimo.

Naibu Waziri wa Kilimo, INNOCENT BASHUNGWA ameyasema hayo, baada ya kutembelea na kukagua mashamba ya mfano wa kilimo cha pamba, katika Kituo cha Utafiti-TARI, Ukiriguru mkoani Mwanza.

Naibu Waziri BASHUNGWA amesema kuwa, mradi wa kuinua kilimo cha pamba unaotekelezwa na Brazil katika katika nchi tatu za Burundi, Kenya na Tanzania, utajielekeza zaidi katika kuwahakikishia wakulima, pamba mbegu bora.

 Amesema kuwa, kupitia mradi huo, uzinduzi wa utafiti wowote utakaofanywa kwa ajili ya mageuzi ya kilimo cha pamba nchini, ni lazima utamfikia mkulima ili aweze kuongeza tija.

Naibu Waziri BASHUNGWA amesisitiza kuwa, Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dakta JOHN POMBE MAGUFULI, imedhamiria kwa kauli moja, kuimarisha sekta ya kilimo, likiwemo zao la pamba.

 

Na. Martin Kuhanga

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,Kuomba zabuni mabasi yaendayo haraka

DAR ES SALAAM

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam linakusudia kuomba zabuni ya kutoa huduma ya kusafirisha abiria kupitia mabasi yaendayo haraka kati ya Gerezani, Kariakoo na Mbagala.  Mstahiki Meya wa Jiji, ISAYA MWITA, amebainisha hayo baada ya kumalizika kwa kikao cha Baraza la Madiwani, kilichofanyika leo, katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.

 Meya Mwita amesema kuwa tayari Wakala wa mabasi yaendayo haraka wameshatangaza zabuni ya ujenzi wa awamu ya pili ya miundombinu ya mabasi itakayoanzia Kegerezani hadi Mbagala hivyo kama jiji limeona kunahaja ya kuomba zabuni hiyo ilikutoa huduma hiyo ya usafiri.

Amefafanua kuwa jiji linania ya kuomba zabuni hiyo kutokana na kuwa wanaweza kutoa huduma hiyo ili kusaidia adha ya foleni iliyopo kwa sasa katika maeneo ya Mbagala.

“ Tunatarajia kuomba zabuni ya kutoa huduma ya kusafirisha abiria hapa jijini ,iwapo tutakubaliwa basi kama jiji nalo litakuwa miongoni mwa watoa huduma hiyo” amesema Meya Mwita.

Tunajua kwamba pesa tunazo, nauwezo wakutoa huduma hiyo tunao,kwahiyo wakazi wa jijini hapa wafahamu kuwa kama tutakubaliwa tutatoa huduma hiyo, ndio mana leo nimewaeleza madiwani kwamba uliangalie jambo hili kwa umuhimu wake ilitujiandae” ameongeza.

Katika hatua nyingine baraza hilo limepitisha kwa kauli moja taarifa mbalimbali za utendaji na miradi mbalimbali zilizotolewa na wenyeviti wa kamati  mbalimbalimbali za jiji.

Mwishoo.

Imetolewa leo Machi 12 na Christina Mwagala .Afisa habari ofisi ya meya wa jiji.

***

 

Frida Manga

VYOMBO VYA KANISA,TANZANIA TIMIZENI WAJIBU

DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania-TEC, Padri CHARLES KITIMA, amevitaka vyombo vya habari vya Kanisa nchini kuhakikisha vinatimiza wajibu wake wa kuinjilisha.

Padri KITIMA ametoa wito huo jana wakati akifunga mafunzo ya waandishi wa habari wa vyombo vya Kanisa Katoliki yaliyohusu masuala ya utafiti wa wasikiliza yani Audience Research, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa baraza hilo, Kurasini, Dar es Salaam.

Amesema kuwa pamoja na kzi nyingi zinazofanywa na vyombo hivyo katika upashanaji habari, lakini vaina budi kuhakikisha vinatimiza majukumu yake ya msingi  ya kulitangaza Neno la Mungu.

Padri KITIMA amesema vyombo vya habari vya Kansia katika ulimwengu huu wa wa sayansi na teknoloji, ni muhimu kufanya tafiti za mara kwa mara ili kuboresha vipindi na usiku wake.

Mafunzo ya utafiti kuhusu wasikiliza kwa Redio za Kanisa, yaliwahusisha waandishi wa habari kutoka Redio Tumaini, Redio SAUT-ya Chuo Kikuu cha SAUTI, Mwanza, Redio Mwangaza Dodoma, Redio Huruma Tanga, Redio Maria Tanzania, Redio Chemichemi ya Sumbawanga na Redio Habari Njema ya Jimbo Katoliki la Mbulu.

***

Alex Kachelewa

 

SIKU YA WANAWAKE MUSOMA,TANZANIA YAFANA

MUSOMA.

Umoja wa wanawake wakristo Jimbo Katoliki la Musoma wamefanya kongamano lao la siku ya wanawawake Duniani katika parokia ya Nyamiongo humo na kuhudhuriwa na wanawake wa makanisa mbalimbali ikiwemo wa KKKT, Aglikana, Wakatoliki, Morovian, AIC na Menonite.

Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma Mhashamu MICHAEL MSONGANZILA ameungana na wanawake hao katika kongamano hilo la siku ya wanawake duniani na kuwafundisha mbinu za kuimarisha ndoa zao.

Askofu MSONGANZILA amesema kuwa ili kusumisha  ndoa yapo masuala mbalimbali ya kuzingatia ambayo yanaweza kuchochea kuimarisha ndoa ikiwemo kuitana mama na baba.

Amewaambia wanawake hao kuwa wanapaswa kuwa waaminifu na kuwaamini waume zao kwani kukosekana kwa uaminifu na kutoaminia kumekuwa kukisababisha ndoa nyingi kusambaratika na matokeo yake baba anamuachia mama mzigo wa kulea familia.

 

Ashura Kishimba.

Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.