• Kard. Pengo aunda mfumo mpya utambuzi wa vigango
• Ulongoni sasa Parokia Padri Amadori Paroko wake
• Arudisha Historia ya Pugu kwa Mapadri Wabenediktini
• Apangua vituo vya kazi kwa Mapadri Jimbo Kuu Dar
Na John Liveti
WAKATI Watananzia wakiendelea kukuna vichwa juu ya Rais gani anayefaa kuwaongoza katika kipindi kingine cha miaka mitano ijayo kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu, Viongozi wa Kanisa Katoliki nchini wamekata mzizi wa fitina na kueleza kiongozi anayefaa kuiongoza Tanzania.
Aidha Viongozi hao wametoa angalisho kubwa kwa wananchi kuhusu taifa linapoelekea kwenye uchaguzi huo likiwatahadharisha waamini kusali ili kulinusuru Taifa na kudumisha amani.
Kauli hiyo ya Maasofu hao imetolwa katika Ibada ya Misa Takatifu ya Sherehe ya Tokeo la Bwana iliyokwenda sanjari na utoaji wa Daraja za Upadri na Ushemasi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.
Kwa upande wake Askofu Msaidizi wa Jimbo hilo, Mhashamu Eusebius Nzigilwa alisema kiongozi anayefaa kuliongoza Taifa la Tanzania nia mwenye hofu ya Mungu na mwadilifu.
Alisema mambo mengi yanayotokea nchini ikiwemo vitendo vya ufisadi yanatokana na kutowepo kwa viongozi waadilifu na kwamba chanzo kikuu cha uvunjifu wa amani nchini kimetona viongzo wasipotenda haki na kutumia madaraka kwa ajili ya maslahi yao binafsi jambo ambalo halifai kwa viongozi waliopewa madaraka kuongoza nchi.
Kwa mujibu wa Askofu Nzigilwa katika Historia ya Kanisa ilionekana kuwa wakati wa kuzaliwa kwake Bwana Yesu Kristo watawala wa wakati huo walikuwa hawakukubali kuwa Kristo aliyezaliwa ni mfalme kutokana na hila ya watawala hao na chuki na ndio maana Herode alipopata taarifa ya kuzaliwa kwake Kristo alifadhaika na kuamuru wale wataaalmu wa Nyota wamletee taarifa kuwa huyo aliyezaliwa aanafananaje ili yeye aweze kufahamu lakini kutokana na ufikiri wake ulikuwa umegawanyika katika sehemu mbili katika utawala kisiasa na utawala kiuflme hakuweza kufanikiwa hivyo aliweza kuamuru mauaji ya watoto wa kiume walio chini ya miaka miwili kuuawa lakini lego lake halikufanikisha kuuawa kwa Yesu Kristo.
“Hali hiyo iliyoonekana kuwa kuna chuki za kidini katika jamiii na ilizua taharuki kubwa tunaiona hadi leo kuwepo kwa chuki baina ya dini moja na nyingine hiyo yote ni hali ya viongozi na wenye mamlaka kujichukulia maaamuzi bila ya kutafakari kwa kina”,alisema Askofu Nzigilwa.
Askofu Nzigilwa alisema katika kutafakari kwa kina sakata hilo la hila za Herodi ni lazima kutafakari kwa kina zaidi na zaidi kwa kila Mtanzania katika kipindi cha mwaka huu ambapo taifa linapoelekea katika Uchaguzi Mkuu kwani hila kama za Herodi zipo kwa viongozi wengi wa taifa letu ambao hawastahili kuchaguliwa.
Alisema wapo ambao wanatumia nguvu za fedha kwa ajili ya kuwaangamiza wengine ili waweze kumiliki madaraka pasipo kustahili jambao ambalo linaleta ukakasi kwa wananchi na hata wakati mwingine kutishia machafuko katika jamii kutokana na utawala wa pesa.
“Ni jambo kwa kila mwanasiaasa ana watawala kujiuliza kama kweli wanatenda haki wanayopaswa kuitenda pasipo kumgandamizi raia yoyote kwa kutumia pesa au madaraka”,alisema Askofu Nzigilwa.
Alisema kuwa awali Mfalme Herodi alifahamu kuwa Kristo alizaliwa kwa ajili ya mpango wa Mungu wa kuwakomboa binadamu na ndio maana alizaliwa katika mazingira Duni ambayo alishuhudiwa na watu duni wenye dhiki ambao daima hukesha huko mabondeni kwa ajili ya kulinda mifugo yao.
Askofu Nzigilwa alisema inatupwa kila kiongozi kufikiri kwa umakini juu ya utawala wake katika sehemu yake kama anaongoza kwa maslahi yake au ya wengi na sio kufuata nyayo za Mfale Herode.
Alibainisha kuwa hali hiyo imejitokeza haya kwa viongozi wa sasa ambao wanadiriki kuwaaangamiza wengine bila ya hatia ikiwemo kuwatupa gerezani bila kosa lolote kwani Mungu alimuumba mwanadamu akiwa na mpango naye na wala si kumgandamiza.
Akizungumza juu uongozi wa kisiasa Askofu Nzigilwa alisema kuwa kwana namna nyinginne watawala wa wakati ule walifikiri pia kuzaliwa kwe Kristo kutaweza kuwasaidia kufanikiwa kiuchumi katika kupandisha thamani ya Dola kwa wakati ule kwani Kristo alizaliwa katika Betrehemu ya Uyahudi wakidhani ataimarisha utawala wa kiyahududi kuwa na nguvu ya kiuchumi zidi ya nchi za Isarael ambazo zilikuwa na nguvu ya kiuchumi jambo lililokwenda kinyume na matarajio yao.
Askofu Nzigilwa alifahamisha kuwa ni vema jamii ikajengwa na hofu ya Mungu hasa katika madaraka na kuacha kutumia njia haramu za kujipatia madaraka kama vile rushwa na wizi wa kura ambao unajitokeza mara nyingi katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika nchini kwani hali hiyo inaweza kuleta machafuko na kumwaga damu.
Askofu Nzigilwa alisema kazi kubwa kwa viongozi wa Kanisa ni kusisitiza kusali kwa ajili ya kuombea amani ya taifa jambo linalotakiwa kufanywa na kila mwaamini hasa katika kipindi Taifa linapoekekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Aidha Askofu Nzigilwa alitakwa Waamini wanotaka kugombea nafsi mbalimbali za uongozi katika ngazi mbalimbali ikiwemo Urais, Ubunge na Udiwani kujitokeza na kuchukua fomu ila wawe waangalifu wasifuate nyayo za Mfalme Herode na wala wasiwe watu wa kugandamiaza na kuwaaangamiza wengine.
KARDINALI PENGO ATANGAZA MFUMO MPYA WA VIGANGO
Aidha uwa upande wake Askofu Mkuu wa wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizungumza wakati wa Misa hiyo ya daraja la Upadri na Ushemasi alitangaza mabadiliko na kuwapangia kazi Mashemasi na Mapadri na kukitangaza Kigango cha Ulongoni kuwa Parokia mpya ya 86 ya jimbo hilo.
Kardinali Pengo alitangaza pia mfumo mpya wa utambuzi wa Vigango ambapo katika kuanza mfumo huo amevitangza vigango vitatu vya jimbo hilo kuwa Parokia Teule huku kurudisha Historia ya Pugu amewarudishia wamisionari wa Shirika la Wabenedictini kuendea na utume katika Parokia hiyo na Kituo cha Hija.
Pamja na hayo Kardinali Pengo amefanya mabadiliko madogo baada ya kuhamishia katika Parokia ya Pugu Padri Melkiol Kayombo kuwa Paroko wa Pugu na Padri Leonardo Amadore kuwa Paroko wa Parokia ya Ulongoni.
AVIPANDISHA HADHI VIGANGO VITATU
Katika kuanza kuutumia mfumo huo mpya wa Kigango ili kiweze kuwa Parokia lazima kipitia ngazi ya Parokia Teule, Kardinali Pengo alikitangza Kigango cha Ununio kilchopo Parokia ya Boko kuwa Parokia Teule na kitakuwa chini ya Mapadri wa Shirika la Watawa wa Matkatifu Vicenti kutoka Jimbo Katoliki la Mbinga.
Vigango vingine ni pamoja na Kigango cha Mtakatifu Yohane Mtumme ambacho awali kilifahamika kama Mtakatifu Petro kuwa Parokia Teule kikiwa chini ya Wamisionari wa Shirika la Maria Imakulata na Kigango cha Thomas More kuwa Parokia Teule kikiwa chini Mapadri wa Jimbo chini ya Padri Girlbert Makuru.
Kardinali Pengo alisema Mapadri waliopangiwa katika vigango hivyo wanatakiwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa juhudi ili ifikapo Julai mwaka huu vitangazwe kuwa Parokia kamili.
Kardinal Pengo aliwashukuru waamini kwa moyo wao wa upendo hasa kwa kuwatoa vijana wao kuingia katka miito mitakatifu na kumtaka Padri Joseph Mapunda kwenda katika kituo chake cha kazi alichopangiwa hapo awali ili kutekeleza kazi ya utume katika Kanisa la Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwani Padri Joseph Mapunda ni Paroko wa Parokia ya Kibangu nafasi alipangiwa tangu Julai 7, mwaka jana.
Awali Askofu Msaidizi wa jimbo hilo, Mhashamu Titus Mdoe akitoa humilia yake kwenye Ibada ya Masifu ya jioni aliwaasa walipewa daraja Takarifu ya Ushemasi, Shemasi Mmoja alipewa Daraja Takatifu ya Upadri kuhakikisha wanakiishi kiapo cha useja kwani ni muhimu sana kwa Yule anaingia katika maisha ya ukasisi kwa sababu Kasisi kujitoa sadaka na sadaka yenyewe ndiyo hiyo ya kuacha yote na kumfuasa Kristo na kutenda kazi yake.
Aidha Askofu Mdoe aliwataka waamii kutofikiri vibaya kuwa wana mapungufu bali hiyo ni sadaka na katika kufanya kazi wasiwe watu wa majivuno wala kufanya kazi kwa sifa bali watende kwa sifa na utukufu wa Mwenyezi Mungu.
Askofu Mdoe alisema ni vema watumishi hao wa Mungu wakaacha ubinafsi na kutokuwa na tabia ya majigambo kwa kuzitumia akili zao na usomi walioupata kueneza Neno la Mungu.
Waliopata Daraja ya Ushemasi ni Shemasi Raymond Mbaula wa Parokia ya Kigamboni ambaye kwa sasa amepangiwa kufanya kazi katika Parokia ya Ikwiriri, Shemasi Meinrad BigirwaMungu ambaye amepangiwa kufanya kazi ya kichungaji katika Nyumba ya Askofu Msaidizi Masaki na Parokia ya Mtakatifu Petro Oyesterbay na Shemasi Dainiel Matungwa anayekwenda kufanya kazi ya uchungaji Parokia ya Roho Mtakatifu Kitunda.
Na aliyepewa Daraja takatifu ya Upadri Padri Tito Rwegoshora amepangaiwa kufanya kazi ya kichungaji katika Parokia ya Ukonga akiwa ni wakili Paroko wa Parokia hiyo, Padri Asisi Mendosa aliyekuwa masomoni Roma amepangiwa kufanya utume kwenye Parokia ya Mtakatifu Yosefu kama Paroko Msaidizi na kumfamisha Padri Ladislaus Kapinga aliyekuwa Paroko Msaidizi Parokia ya Mt. Yosefu na kuwa Paroko Msaidizi kwenye Parokia ya Mtakatifu Martha Mikocheni.
Aidha Kardinali Pengo amempangia Padri Theophil kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC}, kuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Yosefu na kufanya Parokia hiyo kuwa na Maparoko wasaidizi wawili.