Menu
RSS

Wauguzi Mweka waula

Na Celina Joseph 

WAHITIMU wa mafunzo ya wauguzi wasaidizi katika Chuo cha Mweka, wamepewa ahadi ya kusaidiwa kupata sehemu ya kufanyika kazi katika baadhi ya hospitali zilizoko kwenye Kata ya Kigogo jijini Dar es Salaam.

Ahadi hiyo ilitolewa na  Afisa Mtendaji  kata hiyo Anthony Ngonyani, hivi karibuni  aliyekuwa mgeni rasmi akimwakilisha Diwani wa kata hiyo, alipozungumza nao kwenye mahafali ya 10 yaliyofanyika Kigogo.  

Alisema waanguzi wasaidizi wanahitajika sana, ili kuongeza nguvu kwa madaktari  na manesi wanaofanya kazi hiyo.

Ngonyani alisema wahitimu wa kazi ya uuguzi wanapaswa pia kuzingatia maadili ya kazi yao ili kuepusha madhara na vifo kwa wangojwa na kutenda kazi kwa huruma na upendo. 

 Naye Mkuu wa Chuo cha uuguzi cha Mweka Kigogo Dk. Mlangwa, alisema kila mhitimu anapaswa kuzingatia mafunzo kwa umakini na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya uuguzi. 

Alisema huruma kwa wangonjwa inahitajika zaidi bila kusahau upendo licha ya kumpatia matibatu  mgonjwa kwani kufanya hivyo kutamsaidia mgonjwa kupata afuaeni hata kabla ya matibabu. 

Dk. Mlangwa alisema kwa mafunzo waliyoyapata ikiwa ni pamoja na mafunzo kwa vitendo katika hospitali mbalimbali wauguzi hao watakuwa wamepata elimu ya kutosha kumhudumia mgonjwa kama wauguzi wasaidizi. 

Aidha Mkuu huyo alikemea tabia ya baadhi ya wauguzi kuwanyanyasa wagonjwa na kuwatolea lugha zisizo rasmi kuwa haifai katika kazi yao kwani wanakiuka maadili ya uuguzi.

Alisema Muuguzi mwenye maadili daima anazingatia, kazi yake na kuwaheshimu watu wote wanaofika kwa ajili ya matibabu kwa kuwa wao ndio wataalamu wa masuala ya afya badala ya kuwakejeli na kutaka rushwa , kuwa tabia hiyo sio nzuri hata kidogo. 

Mkuu huyo wa chuo pia aliwataka waunguzi hao kutokuridhika na elimu waliyoipata bali watafute muda ili kujiendeleza zaidi katika ujuzi huo. 

Alisema elimu waliyoipata sio kwamba haifai bali iwe tiketi ya kwenda mbele kwa mfunzo zaidi ili kuwafanya wagojwa wafurahie huduma itakayokuwa ikitolewa kwa kiwango cha hali ya juu na watu wenye taaluma iliyobobea. 

Alisema vinginevyo badala ya kuhudumia wagonjwa watabaki kutoa lugha zisizo rasmi, kutokuwajibika wakati wa saa za kazi na pengine kutoroka ofisini kwa sababu ya kutokuwa makini.

Kwa upande wake mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo, Sista Issabela Mdam wa Shirika la Mtakatifu Vincent wa Paulo wa Mbinga, aliwataka wahitimu wenzake kufanya kazi kwa uadilifu na kufuata kanuni za uuguzi. 

Sista Issabela alisema kazi itakuwa ni rahisi ikiwa wauguzi hao wakifuata kanuni za kazi yao, ikiwa ni pamoja na kumshirikisha Mungu kwa kuwa kazi bila Mungu haiwezi kuwa na mafanikio. 

Alisema mafanikio ya kazi yoyote hayawezi kuja kuwa na juhudi za mtu binafsi hasa katika suala la kujiendeleza kimasomo zaidi na kwamba iwapo muuguzi atakuwa na ujuzi wa kutosha itamsaidia kutoa huduma kwa wagonjwa bila hofu kwa kuwa atakuwa anafahamu nini anafanya, tofauti na ujuzi wa kubabaisha wajue kwamba kosa moja linaweza kugharimu uhai wa Mtu. 

Sista huyo alitoa wito pia kwa jamii inayokuwa ikiwahudumia wagonjwa kwenye hospitali kuwa na moyo wa uvumilivu badala ya kuwalaumi na kugombana na wauguzi jambo linaloweza kuwafanya wagonjwa kukosa imani na waunguzi. 

Alisema kazi hiyo ni nzuri ila inahitaji umakini mkubwa, moyo wa huruma na upendo bila kusahau kumuomba Mwenyezi Mungu mafanikio kila siku.

Katika mahafari hayo wahitimu walipewa zawadi mbalimbali kwa mshindi aliyeongoza kwa nidhamu, masomo, mazoezi kwa vitendo, uuguzi na ukunga, ambapo miongoni mwao alikuwa ni Sista Issabel Mdam, Mwasi Sostenes na Hadija Suleiman waliochukua ushindi wa jumla.

Jumla ya wahitimu 176 wametunukiwa vteti vyao katika mahafali hayo ya 10 tangu Chuo cha Uuguzi cha Mwika kilipoanzishwa.  

 

 

Read more...

Maaskofu wamtaja Rais ajaye

 • Kard. Pengo aunda mfumo mpya utambuzi wa vigango

• Ulongoni sasa Parokia Padri Amadori Paroko wake

• Arudisha Historia ya Pugu kwa Mapadri Wabenediktini

• Apangua vituo vya kazi kwa Mapadri Jimbo Kuu Dar

Na John Liveti

WAKATI Watananzia wakiendelea kukuna vichwa juu ya Rais gani anayefaa kuwaongoza katika kipindi kingine cha miaka mitano ijayo kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu, Viongozi wa Kanisa Katoliki nchini wamekata mzizi wa fitina na kueleza kiongozi anayefaa kuiongoza Tanzania.

Aidha Viongozi hao wametoa angalisho kubwa kwa wananchi kuhusu taifa linapoelekea  kwenye uchaguzi huo likiwatahadharisha waamini kusali ili kulinusuru Taifa na kudumisha amani.

Kauli hiyo ya Maasofu hao imetolwa katika Ibada ya Misa Takatifu ya Sherehe ya Tokeo la Bwana iliyokwenda sanjari na utoaji wa Daraja za Upadri na Ushemasi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu  Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.

Kwa upande wake Askofu Msaidizi wa Jimbo hilo, Mhashamu Eusebius Nzigilwa  alisema kiongozi anayefaa kuliongoza Taifa la Tanzania nia mwenye hofu ya Mungu na mwadilifu.

Alisema mambo mengi yanayotokea nchini ikiwemo vitendo vya ufisadi yanatokana na kutowepo kwa viongozi waadilifu na kwamba chanzo kikuu cha uvunjifu wa amani  nchini kimetona viongzo wasipotenda haki na kutumia madaraka kwa ajili ya maslahi yao binafsi jambo ambalo halifai kwa viongozi waliopewa madaraka kuongoza nchi.

Kwa mujibu wa Askofu Nzigilwa katika Historia ya Kanisa ilionekana kuwa wakati wa kuzaliwa kwake Bwana Yesu Kristo watawala wa wakati huo walikuwa hawakukubali  kuwa Kristo aliyezaliwa ni mfalme kutokana na hila ya watawala hao na chuki na ndio maana Herode alipopata  taarifa ya kuzaliwa kwake Kristo alifadhaika na kuamuru  wale wataaalmu wa Nyota wamletee taarifa kuwa huyo aliyezaliwa aanafananaje  ili yeye aweze kufahamu lakini kutokana na ufikiri wake ulikuwa umegawanyika katika sehemu mbili  katika utawala kisiasa na utawala kiuflme hakuweza kufanikiwa hivyo aliweza kuamuru  mauaji  ya watoto wa kiume walio chini ya miaka miwili kuuawa  lakini lego lake halikufanikisha kuuawa kwa Yesu Kristo.

“Hali hiyo iliyoonekana kuwa kuna chuki za kidini katika jamiii na ilizua taharuki kubwa tunaiona hadi leo kuwepo kwa chuki baina  ya dini moja na nyingine  hiyo yote ni hali ya viongozi na wenye mamlaka  kujichukulia maaamuzi bila ya kutafakari kwa kina”,alisema Askofu Nzigilwa.

Askofu Nzigilwa alisema katika kutafakari kwa kina sakata hilo la hila za Herodi ni lazima kutafakari kwa kina zaidi na zaidi  kwa kila Mtanzania katika kipindi cha mwaka huu ambapo taifa linapoelekea katika Uchaguzi Mkuu kwani  hila kama za Herodi zipo kwa viongozi wengi  wa taifa letu ambao hawastahili kuchaguliwa.

Alisema wapo ambao wanatumia nguvu za fedha kwa ajili ya kuwaangamiza wengine  ili waweze kumiliki madaraka pasipo kustahili jambao ambalo linaleta ukakasi kwa wananchi na hata wakati mwingine kutishia machafuko katika jamii kutokana na utawala wa pesa.

“Ni jambo kwa kila mwanasiaasa ana watawala kujiuliza  kama kweli wanatenda haki wanayopaswa kuitenda pasipo kumgandamizi raia yoyote kwa kutumia pesa au madaraka”,alisema Askofu Nzigilwa.

Alisema kuwa awali Mfalme Herodi alifahamu kuwa Kristo alizaliwa kwa ajili ya mpango wa Mungu wa kuwakomboa binadamu na ndio maana alizaliwa katika mazingira Duni  ambayo alishuhudiwa na watu duni wenye dhiki  ambao daima hukesha huko mabondeni kwa ajili ya kulinda mifugo yao.

Askofu Nzigilwa alisema inatupwa kila kiongozi kufikiri kwa umakini juu ya utawala  wake katika sehemu yake kama anaongoza kwa  maslahi yake au ya wengi na sio kufuata nyayo za Mfale Herode.

Alibainisha kuwa hali hiyo imejitokeza haya kwa viongozi wa sasa ambao wanadiriki kuwaaangamiza wengine bila ya hatia ikiwemo kuwatupa gerezani bila kosa lolote kwani Mungu alimuumba mwanadamu akiwa na mpango naye na wala si kumgandamiza.

Akizungumza juu uongozi wa kisiasa Askofu Nzigilwa alisema kuwa  kwana namna nyinginne watawala wa wakati ule walifikiri pia kuzaliwa kwe Kristo kutaweza kuwasaidia kufanikiwa kiuchumi  katika kupandisha thamani ya Dola kwa wakati ule kwani Kristo alizaliwa katika Betrehemu ya Uyahudi wakidhani ataimarisha utawala wa kiyahududi kuwa na nguvu ya kiuchumi zidi ya nchi za Isarael ambazo zilikuwa na nguvu ya kiuchumi jambo lililokwenda kinyume na matarajio yao.

Askofu Nzigilwa alifahamisha kuwa ni vema jamii ikajengwa na hofu ya Mungu hasa katika madaraka  na kuacha kutumia njia haramu za kujipatia madaraka  kama vile rushwa  na wizi wa kura ambao unajitokeza mara nyingi katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika nchini kwani hali hiyo inaweza kuleta machafuko  na kumwaga damu.

Askofu Nzigilwa alisema kazi kubwa kwa viongozi wa Kanisa ni kusisitiza kusali kwa ajili ya kuombea amani ya taifa jambo linalotakiwa kufanywa na kila mwaamini hasa katika kipindi Taifa linapoekekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Aidha Askofu Nzigilwa alitakwa Waamini wanotaka kugombea nafsi mbalimbali za uongozi katika  ngazi  mbalimbali ikiwemo Urais, Ubunge na Udiwani kujitokeza na kuchukua fomu ila wawe waangalifu wasifuate nyayo za Mfalme Herode na wala wasiwe watu wa kugandamiaza na kuwaaangamiza wengine.

 

KARDINALI PENGO ATANGAZA MFUMO MPYA WA VIGANGO

Aidha uwa upande wake Askofu Mkuu wa wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizungumza wakati wa Misa hiyo ya daraja la Upadri na Ushemasi alitangaza mabadiliko na kuwapangia kazi Mashemasi na Mapadri na kukitangaza Kigango cha Ulongoni kuwa Parokia mpya  ya 86 ya jimbo hilo.  

Kardinali Pengo alitangaza pia mfumo mpya wa utambuzi wa Vigango ambapo katika kuanza mfumo huo amevitangza vigango vitatu vya jimbo hilo kuwa Parokia Teule huku kurudisha Historia ya Pugu amewarudishia wamisionari wa Shirika la Wabenedictini  kuendea na utume katika Parokia hiyo na Kituo cha Hija.

Pamja na hayo Kardinali Pengo amefanya mabadiliko madogo baada ya kuhamishia katika Parokia ya Pugu Padri Melkiol Kayombo  kuwa Paroko wa Pugu na Padri Leonardo Amadore kuwa Paroko wa Parokia ya  Ulongoni.

 

AVIPANDISHA HADHI VIGANGO VITATU

Katika kuanza kuutumia mfumo huo mpya wa Kigango ili kiweze kuwa Parokia lazima kipitia ngazi ya Parokia Teule, Kardinali Pengo alikitangza Kigango cha Ununio  kilchopo Parokia ya Boko kuwa Parokia Teule na kitakuwa chini ya Mapadri wa Shirika la Watawa wa Matkatifu Vicenti kutoka Jimbo Katoliki la Mbinga.

Vigango vingine ni pamoja na Kigango cha Mtakatifu Yohane Mtumme ambacho awali kilifahamika kama Mtakatifu Petro kuwa Parokia Teule kikiwa chini ya Wamisionari wa Shirika la Maria  Imakulata na Kigango cha Thomas More kuwa Parokia Teule  kikiwa chini Mapadri wa Jimbo chini ya Padri Girlbert Makuru.

Kardinali Pengo alisema  Mapadri waliopangiwa  katika vigango hivyo wanatakiwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa juhudi ili ifikapo Julai mwaka huu vitangazwe kuwa Parokia kamili.

Kardinal Pengo aliwashukuru waamini kwa moyo wao wa upendo hasa kwa kuwatoa vijana wao kuingia katka miito mitakatifu na kumtaka Padri Joseph Mapunda  kwenda katika kituo chake cha kazi alichopangiwa hapo awali ili kutekeleza kazi ya utume katika Kanisa la Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwani Padri Joseph Mapunda  ni Paroko wa Parokia ya Kibangu nafasi alipangiwa tangu Julai 7, mwaka jana.

Awali Askofu  Msaidizi wa jimbo hilo, Mhashamu Titus Mdoe akitoa humilia yake kwenye Ibada ya Masifu ya jioni aliwaasa walipewa daraja Takarifu ya Ushemasi, Shemasi Mmoja alipewa Daraja Takatifu ya Upadri kuhakikisha wanakiishi kiapo cha useja kwani ni  muhimu sana kwa Yule anaingia katika maisha ya ukasisi kwa sababu Kasisi kujitoa sadaka  na sadaka yenyewe ndiyo hiyo ya kuacha yote na kumfuasa Kristo na kutenda kazi yake.

Aidha Askofu Mdoe aliwataka waamii kutofikiri vibaya kuwa wana mapungufu bali hiyo ni sadaka  na katika kufanya kazi wasiwe watu wa majivuno  wala kufanya kazi kwa sifa bali watende kwa sifa na utukufu wa Mwenyezi Mungu.

Askofu Mdoe alisema ni vema watumishi hao wa Mungu wakaacha ubinafsi na kutokuwa na tabia ya majigambo kwa kuzitumia akili zao na usomi walioupata kueneza Neno la Mungu.

Waliopata Daraja  ya Ushemasi ni Shemasi Raymond Mbaula wa Parokia ya Kigamboni  ambaye kwa sasa amepangiwa kufanya kazi katika Parokia ya Ikwiriri, Shemasi Meinrad BigirwaMungu ambaye amepangiwa kufanya kazi ya kichungaji katika Nyumba ya Askofu Msaidizi Masaki na Parokia ya Mtakatifu Petro Oyesterbay na Shemasi Dainiel  Matungwa anayekwenda kufanya kazi ya uchungaji Parokia ya  Roho Mtakatifu Kitunda.

Na aliyepewa Daraja  takatifu ya  Upadri Padri Tito Rwegoshora  amepangaiwa kufanya kazi ya kichungaji katika Parokia ya  Ukonga akiwa ni wakili Paroko wa Parokia hiyo, Padri Asisi Mendosa aliyekuwa masomoni Roma amepangiwa kufanya utume kwenye Parokia ya Mtakatifu Yosefu kama Paroko Msaidizi na kumfamisha Padri Ladislaus Kapinga aliyekuwa Paroko Msaidizi Parokia ya Mt. Yosefu na kuwa Paroko Msaidizi kwenye Parokia ya Mtakatifu Martha Mikocheni.

Aidha Kardinali Pengo amempangia Padri Theophil kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC}, kuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Yosefu na kufanya Parokia hiyo kuwa na Maparoko wasaidizi wawili.

 

 

Read more...

Gari linaloweza kujiegesha kwa kutumia saa

Hakuna kitu kibaya kama kusahau ulikoegesha gari lako katika jengo la kuegeshea magari lenye goraf nyingi.

Lakini hivi karibuni hautahihajika kupanda gorofa kutafuta gari lako kwani kampuni ya kutengeza magari ya BMW, imetangaza kuzindia kifuaa ambacho kinaweza kuyawezesha magari ya kampuni hio kujiegesha yenyewe kwa kubonyeza tu kifaa hicho.

Hata hivyo dereva wa gari hilo atalazimika kuvaa saa ya Smartphone mkononi ambayo ataibonyeza na kuiamrisha kwa sauti gari hilo kwenda kujiegesha.

Gari hilo kwa amri ya dereva litatoka liliko baada ya dereva kushuka na kwenda lenyewe kwa kuhesabu muda utakalichukua kwenda kutafuta sehemu ya kujiegesha.

Tawi la kampuni ya BMW mjini Munich, Ujerumani limezindua teknolojia hio ambayo inawezesha gari kujiegesha lenyewe.

Gari hilo linatumia miale ya Leser iliyo kujitafutia ramani ya jengo ambalo lipo. Dereva anaweza kuliamrisha gari hilo kwenda kujiegesha kwa kutumia Smartphone.

Teknolojia hio inajulikana kama ' Remote Valet Parking Assistant,' na inafanyiwa majaribio kwenye gari la BMW i3.

Badala ya kutumia GPS, teknolojia hio inatumia miale ya Laser ambayo hutengeza ramani inayolisaidia gari hilo kutafuta sehemu ya kwenda kujiegesha.

Teknolojia hiyo inaiwezesha gari hilo kuona njia na nafasi ya kujiegeshea na pia kuona vizingiti mfano kama magari ambayo hayajaegeshwa vyema.

Kwa mujibi wa waliotengeza gari hilo, linaweza kujitafutia nafasi ya kujiegesha na hata kuweza kutambua sehemu ambako kuna nafasi.

Teknolojia hio inatengezwa sambamba na teknolojia nyinginezo zitakazoweza kuzuia gari hilo kugongana na magari mangeine.

Read more...
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.