Menu
RSS
Tanzania

Serikali yapongezwa ugawaji vitabu shule za Sekondari

  • Published in Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Pwani.

Serikali nchini imepongezwa kwa kugawa vitabu vya Hisabati na Sayansi kwa Shule za Sekondari nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Abraham Shafuri ambaye ni Mkuu wa Shule ya St. Metthew, wakati akisoma risala kwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita yaliyofanyika shuleni hapo hivi karibuni.

Shafuri amebainisha kuwa, Serikali hivi karibuni ilifanikiwa kugawa vitabu vya masomo manne ambayo ni Fizikia, Kemia, Biolojia na Hisabati, jambo ambalo ni msingi mkubwa katika kuweka motisha kwa suala zima la ufundishaji na usomaji wa masomo ya sayansi ambayo kwa muda mrefu yamekuwa changamoto kubwa kwa wanafunzi wengi nchini.

“ Tunaipongeza Serikali kwa hatua hii ya kimaendeleo  katika sekta ya elimu hapa nchini kwa takwimu tulizozipata ni kwamba, vitabu hivyo vimezifanya shule za Serikali kuwa na vitabu zaidi ya wiano unaotakiwa na vitabu vingine vipo kwenye makabati”,alisema Shafuri.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa shule aliiomba Serikali kuzikumbuka pia Shule za Binafsi katika kuwagawia vitabu na mahitaji mengine kwa kuwa wanaosoma katika shule hizo ni Watanzania tena watoto wa wakulima na wafanyakazi ambao wameamua kujinyima, ili vijana wao wasome.

Alisema ipo haja kwa serikali kuona umuhimu na mchango unaotolewa na shule binafsi na kuziweka shule hizo katika mpango wa kuwapatia vitabu na mahitaji mengine yanayotolewa katika shule za Serikali.

Alisema serikali imekuwa ikizibagua shule zinazomilikiwa na watu binafsi ambapo aliweka bayana juu ya wasiwasi wake kwamba, wanafunzi wanaosoma shule za binafsi wanabaguliwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, kwa sababu tu ya kusoma katika shule za binafsi.

Shafuri aliweka wazi kwamba Serikali huchukulia kwamba wazazi na walezi kama wameweza kumudu gharama za kusoma katika shule binafsi basi wanaweza pia kumudu gharama za masomo ya Elimu ya Juu.

Aliiomba serikali kulitazama upya jambo hilo kwani kuendelela kwake kunawanyima haki watoto wa kitanzania ambao wazazi na walezi wao ndiyo walipa kodi wa kubwa kwa ujenzi wa Taifa lao la Tanzania.

Akizungumzia kuhusu Mchakato wa Katiba Inayopendekezwa, Mkuu huyo wa Shule alisema, jumuiya ya St. Methew inaipongeza Serikali kwa jitihada kubwa wanazozifanya ili kufanikisha mchakato huo muhimu kwa mustakabali wa Taifa.

Aliongeza kuwa, mchakato huo wa katiba Mpya ulikumbwa na vikwazo vingi tangua hatua za awali za zakutengeneza sheria ya mabadiliko ya Katiba, ukusanyaji wamaoni ya wananchi, utengenezaji wa Rasimu ya Katiba, Bunge maalum la Katiba na sasa wakati wa maaadalizi ya upigaji wa kura ya maoni lakini serikali imeendelea kusimama imara.

“ Kama siyo uimara wa Serikali na ujasiri walionao viongozi wetu, zoezi la upatikanaji  wa Katiba Mpya lingekwama katika hatua za awali kabisa”,alisema Shafuri. 

Akizungumzia kuhusu msimamo juu ya kura ya ndiyo au hapana kwa Katiba Inayopendekezwa alisema, Watanzania wana hamu na wako tiari kuipokea.

Aliendelea kusema kuwa, wananchi wanatakiwa kuachwa huru waisome na kuielewa Katiba inayopendekezwa  na wakigundua maoni yao hayamo kwenye katiba hiyo waamue kupiga kura ya ndiyo au hapana.

Aidha ameiomba Serikali iangalie upya namna bora ya kuwatambua wapiga kura kwani  njia ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa kisasa wa kielectroniki wa BVR  tayari imeonesha  ugumu katika kufanikisha jambo hilo.

Aliahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kuandikisha wanafunzi wote waliofikisha umri wa kupiga kura ili waweze  kupata haki yao ya kikatiba.

maendeleo ya Shule

Mkuu wa Shule alibainisha kuwa Shule hiyo imekuwa na mpango kabambe ambao ndiyo unaowaongoza katika utendaji wa kazi za kila siku na kuongeza kuwa mpango huo umewaletea mafanikio makubwa shuleni hapo.

Alibainisha ukuwa ongozi wa shule hiyo uliweka mpango huo ili kwenda sambamba na mpango wa serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Shafuri alibainisha kuwa matakwa ya mpango wa Serikali wa Big Result Now (BRN), unasisitiza juu ya mambo matatu ambayo ni pamoja na mpango wa maendeleo, kuweka vipaumbele na nidhamu ya utekelezaji.

Alifafanua kuwa mpango wa maendeleo wa shule yake ya St. Metthew’s umegawanyika katika maeneo matatu ambayo ni miundo mbinu, malezi na nidhamu na mwisho ni maendeleo ya taaluma.

Akizungumzia  Malezi ya kiroho, alisema shule hiyo imejiwekea utaratibu mzuri wa malezi ya kiroho kwa wanafunzi ambapo kwa kushirikiana na madhehebu mbalimbali ya kidini wanafunzi wote kwa mujibu wa madhehebu yao wanapata huduma mbalimbali za kiroho ikiwa ni pamoja na mafundisho kutoka kwa viongozi wao wa dini.

Pia anasema wanafunzi shuleni hapo hupata huduma za mfungo kulingana na matakwa ya madhehebu yao ikiwemo Kwaresma, Ramadhani na nyinginezo ambapo wanafunzi wakifunga wanapatiwa huduma zote stahili.

Mkuu huyo wa shule alisisitiza kuwa utaratibu huo wa malezi yakiroho umekuwa silaha kuu inayowasaidia kuboresha nidhamu ya wanafunzi  na kuwafanya wapende kusoma na hivyo kufaulu masomo yao.

Maendeleo Kitaaluma  

Mkuu huyo alisisitiza kuwa, Shule imejiwekea malengo mahususi ya kuwafanya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza kupata sifa za kujiunga na kidato cha tano, na wale wa kidato cha tano  wapate sifa ya kujiunga na elimu ya juu.

Pia alitoa baadhi ya takwimu kuonesha jinsi shule ilivyofanikiwa kufanya vizuri kitaaluma akisema kwamba 2014 jumla ya wanafunzi 411 walifanya mtihani wa kuhitimu kidato cha sita ambapo wanafunzi 359 walipata sifa ya kujiunga na Vyuo Vikuu.

Kwa upande wa kidato cha nne kwa mwaka huo huo shule hiyo ilifanikiwa kufaulisha wanafunzi kwa asilimia 89.2 ambao wanatarajiwa kujiunga na shule mbalimbali za serikali na binafsi kwa elimu ya kidato cha tano mwaka huu.

Kwa upande wa maendeleo ya miundombinu, Shafuri alinabinisha kuwa shule hiyo imefanikiwa kwa asilimia 100. Alisema maendeleo ya miundombinu imekuwa ni chachu kwa walimu na wanafunzi wakati wa kufundisha na kujifunza.

Alisema mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia shule imejipanga vizuri kuhakikisha inakuwa na miundo mbinu rafiki inayojumuhisha madarasa, zana mbalimbali za kufundishia na kujifunzia, maabara za sayansi, maktaba na maabara za komputa.

“Nidhamu ni kiungo muhimu katika kuyafikia malengo yoyote. Ili kuyafikia maelengo ya shule hiyo Shafuri anasema tathimini zinaonesha kuwa shule yake imefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 95”,alisema.

Alisema katika mpango wa serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) suala la motisha limepewa kipaumbele ili kufanikisha mpango huo kabambe, shule yake iliona ili kufikia malengo suala la motisha ni moja ya vipaumbele vyake.

Wakati akizungumzia motisha hizo alisema motisha mbalimbali zinatolewa kuanzia ngazi ya wazazi na walezi lengo likiwa ni kuwafanya nao wajisikie kuwa ni sehemu ya taasisi hiyo na wajione kuwa shule inatambua na kuthamini mchango wao katika maendeleo ya shule.

Alisema motisha mbalimbali zitolewazo na Shule kwa wazazi ni pamoja na kutoa punguzo la karo kwa mzazi mwenye mtoto zaidi ya mmoja anayesoma katika Shule hiyo.

Aliongeza kuwa shule hiyo pia inatoa udhamini kwa waafunzi wanaofanya vizuri katika masomo mbalimbali akisema lengo ni  kuwafanya waongeze bidii katika masomo yao.

Aidha shule hiyo imekuwa na utamaduni wa kutoa motisha kwa walimu ili kuwapa hamasa ya kujituma na kufundisha kwa bidii na hivyo wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao.

Motisha hiyo ni pamoja na ziara za mafunzo nje ya nchi, motisha kwenye matokeo ya mitihani ya Taifa pamoja na zawadi mbalimbali ikwemo magari na laptop.

Nasaha kwa wahitimu     

Mkuu huyo aliwataka vijana wanaomaliza kidato cha sita akiwataka wakumbuke walipofika kuwa ni hatua moja na mbele yao kuna hatua kubwa zaidi ya elimu ya juu.

“Nawaombea kila mmoja wenu awe na nia na dhamira ya ya kusoma na kufikia juu kabisa, fikirieni kusoma na kupata shahada kwanza kisha ya pili na tatu”. Alisema Shafuri.

Pia aliwaasa juu ya nidhamu bora walionesha shuleni pindi walipokuwa shuleni hapo waiendeleze huko waendako na wawe chachu ya mabadiliko kwa jamii wanayoenda kuishi nayo sasa.

“Tunawatuma mkawe chachu ya mabadiliko ya tabia ya vijana wenzenu, msijiunge na makundi mabaya yanayoweza kuwaingiza katika utumiaji wa dawa za kulevya au anasa zinazoweza kuwaletea magonjwa ya zinaa ikiwemo UKIMWI”.   

    End

 

         

Read more...

Kura ya maoni ya Katiba Tanzania yaahirishwa

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imetangaza kuahirishwa kwa zoezi la kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa lililokuwa limepangwa kufanyika Aprili thelathini mwaka huu mpaka itakapotangazwa tena.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu DAMIAN LUBUVA amesema kuwa kuahirishwa kwa zoezi hilo kumetokana na kutokamilika kwa zoezi la uandikishaji wapigakura kwa kutumia teknolojia ya BVR Mkoani Njombe na mikoa mingine.

Jaji LUBUVA amesema kuwa pindi zoezi hilo litakapokamilika kwa Mkoa wa Njombe, litahamia mikoa mingine ya Ruvuma, Mtwara, Lindi na Iringa kwa kutumia vifaa vya BVR vilivyopo huku vifaa vingine vilivyoagizwa vikisubiriwa kupokelewa.

Amebainisha kuwa mwitikio wa wananchi waliojitokeza kujiandikisha Mkoani Njombe ni mkubwa na kwamba Tume yake imeongeza muda kwa kata mbili za Mkoa huo kumalizia zoezi la uandikishaji wapigakura.

Jaji LUBUVA amedokeza kuwa endapo vifaa vyote vya BVR vyenye thamani ya dola za kimarekani milioni sabini na mbili vitawasili, zoezi zima la uandikishaji wapigakura linaweza kukamilika mwezi Julai na ndipo mazoezi mengine yatafuatia.

Kwa upande wao, Kamishna wa Tume hiyo Jaji Mstaafu JOHN MKWAWA na Mjumbe wa Tume Profesa AMON CHALIGHA wamesema kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu hautafanyika kwa kufuata miongozo ya Katiba Mpya endapo ingepitishwa kabla ya uchaguzi huo.

                                                         ***

Editha Mayemba

Read more...

Askofu Mkuu Jimbo katoliki Dar es Salaam kuongoza Misa Alhamisi Kuu

  • Published in Tanzania

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam Mwadhama POLYICARP Kardinali PENGO leo anatarajiwa kuongoza ibada ya Misa Takatifu ya Alhamis Kuu kwenye Parokia ya Mtakatifu Petro Oysterbay.

Wakati Kardinali PENGO akiwa Parokia ya Oysterbay, Askofu Msaidizi EUSEBIUS NZIGILWA atakuwa Parokia ya Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu Kawe wakati Askofu mwingine Msaidizi wa Jimbo hilo Mhashamu TITUS MDOE ataongoza ibada hiyo ya Misa Takatifu ya Alhamis Kuu kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Jimbo Padri DENNIS WIGIRA, kesho asubuhi Kardinali PENGO atasali Njia ya Msalaba kwenye Parokia ya Msimbazi kabla ya kushiriki Ibada ya Ijumaa Kuu kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph.

Naye Askofu Msaidizi NZIGILWA atasali ibada ya Ijumaa Kuu kwenye Parokia ya Sinza wakati Askofu MDOE atasali kwenye Parokia ya Msimbazi.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa wakati wa mkesha wa Pasaka, Kardinali PENGO ataongoza ibada ya Misa Takatifu kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph wakati Askofu NZIGILWA akitarajiwa kuwa Parokia ya Oysterbay huku Askofu MDOE akitarajiwa kuongoza Ibada ya Misa Takatifu ya mkesha kwenye Parokia ya Magomeni.

Sikukuu ya Pasaka, Kardinali PENGO ataongoza ibada ya Misa Takatifu kwenye Parokia ya Kurasini wakati Askofu NZIGILWA ataongoza ibada ya Misa kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph huku Askofu MDOE atakuwa mgeni rasmi kwenye ufungaji wa Kongamano la Pasaka kwenye Shule ya Baobab linalowahusisha vijana wakatoliki wanafunzi.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Jumatatu ya Pasaka, Kardinali PENGO na Askofu NZIGILWA watakuwa Parokia ya Kipawa kwenye Ibada ya Misa Takatifu ya Shirikisho la Kwaya Katoliki Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam SHIKWAKA.

 

                                                                    ***

Fred Mosha

Read more...

Chanzo mauaji ya Albino chaanikwa

  • Published in Tanzania

Na Ashura Kishimba

Imeelezwa kuwa kushindwa kwa jamii kutumia ujuzi na maarifa katika upatikanaji wa malighafi zao kunasababisha kujiingiza kwenye dhana potofu ya kuua watu wenye ulemavu wa ngozi na kudhani kuwa ndio suluhisho la kuwapatia utajiri.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mjumbe wa kamati ya uelimishaji wa kupinga mauji na unyanyasaji wa albino nchini Massoud Kipanya alisema ni jambo la kushangaza kuona mwanadamu badala ya kutumia ujuzi na maarifa kuhakikisha anaboresha maisha yake na Taifa anakuwa na fikra potofu ya kudhani kuwa mwili wa binadamu mwenzake ni suluhisho.

Kipanya alisema mfupa wa mwanadamu au nyama ya Albino hauwezi kuwa kisababishi cha wachimbaji kupata madini mengi, wavuvi kupata samaki wengi, wakulima kupata mazao mengi au mfanyabishara kupata wateja wengi bali ni ukosefu wa elimu, maarifa na ujuzi wa kiuchumi.

Kwa upande wake balozi wa kujitegemea wa kamati ya uelimishaji wa kupinga mauji ya albino ambaye pia ni mlemavu wa ngozi Henry Mdimu alisema mauji hayo sasa imetosha tangu mwaka 2,000 lakini hakuna hatua zozote za dhati zilizochukuliwa kukomesha vitendo hivyo.

Mdimua alisema kutokana na hali hiyo wameona njia kuu ya kutatua tatizo hilo ni kutoa elimu kwa jamii kuanzia ngazi ya chini kwasababu imeonekana kuwa watu wa chini ndio wanaofanikisha mikakati hiyo ya mauji.

“Utoaji wetu wa elimu tutaanza kutoa elimu katika Mikoa ya kanda ya ziwa kwasababu imeonekana tatizo hili limeshika kasi sasa tunataka kuhakikisha kuwa wanaondokana na fikra potofu.

Katika hatua nyingine Shirikisho la vyama vya Tiba Asilia Tanzania SHIVYATIATA limelaani vitendo vya kijambazi vya kukatisha maisha ya kuishi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi Albino, vikongwe na kunajisi watoto kinachofanywa na baadhi ya wananchi nchini.

 

Mwenyekiti wa shirikisho hilo Abdulrahman Lutenga alisema utafiti uliofanywa na shirikisho hilo umebaini kuwa mauji hayo yanasababishwa na matapeli kujifanya waganga wa tiba asili kwa madai kuwa wanaweza kutajirisha watu kwa kuwapa dawa.

 

Lutenga alisema waganga hao pindi wanaposhindwa kufikia malengo aliyokusudia waganga hao hutoa masharti magumu ambayo wanadhani kuwa mteja wake hawezi kuyatekeleza kiurahisi  kwa kutuma viungo vya albino kuuwa au kubaka vikongwe na watoto wachanga.

 

Kwa upande wake katibu wa shirikisho hilo Othaman Shem alitoa  wito kwa serikali na wanajamii kushirikiana kufichua na kutokomeza mtandao mzima unaojihusisha na mauji hayo.

 

Naye Hassan Kambangwa mjumbe wa shirikisho hilo amesisitiza kuwa Watanzania wanapaswa kutambua thamani ya binadamu na Afya yake Albino ni binadamu wa kawaida binadamu wengine pamoja na vikongwena watoto.

 

Mwsho.

 

Read more...

Vitendo vya ukatili ni dalili ya amani kutoweka.

  • Published in Tanzania

DAR ES SALAAM

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam Mwadhama POLYKARP KARDINAL PENGO amesema vitendo vya ukatili  vinavyoendelea kutokea nchini ikiwemo kikundi cha panya rodi vinasababishwa na kukosa usalama wa jumuiya ya watu katika familia.

Kadrinal PENGO ametoa kauli hiyo Jimboni humo katika Ibada  ya Misa Takatifu ya Shukrani iliyoandaliwa na Wanawake Wakatoliki wa Jimbo hilo WAWATA Ibada inayokwenda Sanjari na matoleo kwa wagonjwa katika hospitali ya Ocean road.

Kardinal amesema  kama ulimwengu unafikia katika ukatili wa namna hii ni muhimu kujiuliza  kosa liko wapi kwa kuwa usalama wa familia unaanzia kwa mtu mwenye kuhifadhi uhai wa binadamu  ambaye ni mama.

Ameongeza kuwa anashangazwa na makundi mbalimbali yanayoibuka kufanya ukatili huku akishangazwa na kikundi cha panya rodi kilichoibuka na vijana wadogo na kuwafanyia ukatili wazazi wao bila huruma na kuwata WAWATA kuyombea familia.

Mwadhama ameitaka jamii kutambua  kuwa uzalilishaji unaofanywa na mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu ni kukosa kumuheshimu Mwenyezi Mungu, kumuhifadhi na kumtunza mwanadamu hali inayosababisha kuongezeka kwa maovu.

Hata Hivyo Askofu PENGO  amedokeza wataalamu wa  historia ya kanisa  wanasema katika kipindi hiki watu wengi wameuawa kwa jina la kanisa tena kwa ukatili.

 

***  

Mary Yuda

 

 

 

 

Read more...

Dawa za Kulevya ni Shida

  • Published in Tanzania

 

Na Alex Kachelewa

PAMOJA na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuongeza nguvu katika vita dhidi ya dawa za kulevya nchini bado inaonekana kama ni kilio kilichokosa mwenyewe kutokana na ukweli kwamba hakuna hatua madhubuti za kuikabili vita hiyo.

Hali hiyo inajidhihirisha kutokana na kuwepo kwa matukio mengi na makubwa ya usafirishaji wa dawa za kulevya kwenda nje ama kuingizwa ndani ya nchi.

Kama katika siku za hivi karibuni vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikiripoti kuhusiana na kuwepo kwa iadai kubwa ya Vijana wa kitanzania ambao wameswekwa lupango huo nchini China kwa madai ya kukamatwa na dawa za kulevya.

Inabainisha kwamba wengi wa watanzania hao wapo kwenye magereza mbalimbali nchini China wakisubiri hukumu zao ikiwemo ile ya kunyongwa.

Masuala haya ya biashara ya dawa za kulevya yanaweza kuzua maswali mengi miongoni mwa watanzania lakini pia kwa wanaharakati wanaopambana vita dhidi ya dawa hizo na malezi ya vijana.

Mara nyingi jeshi la polisi kupitia idara yake ya kupambana na dawa za kulevya imekuwa ikikamata vijana mbalimbali wanaosafirisha dawa hizo nje na kuzingiza ndani ya nchi.

Kimsingi Jeshi la polisi limejitahidi katika juhudi zake za kupambana na watu wachache wenye nia mbaya na taifa hili kwa kuingiza dawa za kulevya na kuwaathiri vijana nchini ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa.

Mmoja wa wanaharakati wa masuala ya vijana, ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini katika mahojiano yake na Tumaini Letu anasema kuwa, bado jeshi la polisi lina kazi ngumu kwa sababu wahusika wakubwa wa biashara hiyo ni wakubwa.

“Hii ni vita ngumu sana kwa sababu wahusika sio fagaa bali ni mapapa na manguru ambao polisi inahitaji meno makubwa kuwang’ata”,anasema mwanaharakati huyo katika mazungjmzo yake na gazeti hili.

Akasema kwamba pamoja na juhudi zote za polisi kukamata dagagaa wanaotumwa na mapapa hao, lakini jeshi la polisi bado linatakiwa kuhakikisha linaongeza nguvu zaidi dhidi ya dawa hizo kwani inaonekana watu wenye kufanya biashara hiyo wamekuwa na mbinu nyingi.

Hii inaweza kuwa ni sehemu ya dawa ambazo kwa namna moja ama nyingine zimekwisha ingizwa nchini na kuwaathiri vijana wetu ambao ndiyo tegemeo la kesho.

Kama inavyofahamika vijana wengi kwa sasa wameathirika zaidi na matumizi ya dawa hizo ambazo zimekuwa zikiingizwa nchini kila kukicha isipokuwa chache ndizo zinazonaswa.

Lakini wakati kukiwa na idadi kubwa ya vijana ambao wameathirika na matumizi ya dawa hizo, ni jambo la kushangaza na kujiuliza kwamba wanzipata wapi dawa hizo?

Kwa sababu wengi wa vijana wanaotumia dawa hizo wako katika hali duni na isiyotegemewa hata kidogo, lakini utakuta ndiyo wateja wakubwa wa biashara hiyo haramu.

Sasa kwa mantiki hiyo polisi bado wana kibarua kigumu kwani watalazimika kuongeza juhudi zake katika vita dhidi ya dawa hizo kwa sababu ni jambo la kushangaza kuona ongezeko la vijana wanaotumia dawa hizo kama si udhibiti kuwa mdogo.

Kama kungekuwa na udhibiti mkubwa wa uingizwaji wa dawa hizo za kulevya hata matokeo yake yangejulikana kwani, hata idadi ya watu wanaotumia dawa hizo ingepungua. 

Hivi karibuni Waziri Mpya wa Wizara ya Uchukuzi, Samwel Sitta, ambaye amepokea kijiti kutoka kwa Dk. Harison Mwakyembe anasema kuwa atavalia njuga suala hilo hasa kudhibiti kwenye njia kuu za usafirishai ukuwemo uwanja wa ndege.

Hivyo kwa kauli hiyo ya Waziri mwenye dhamana Polisi haina budi kuimarisha ulinzi katika ukaguzi wake hasa katika maeneo ya mipaka ambako ndiko wahalifu kutumia mwanya wa kupita kwenye njia za panya na hivyo kujikuta biashara hiyo ikiendelea kushamiri nchini.

Kimsingi maeneo ya mipakani ndiko kwenye tatizo kubwa tutake tusitake bila ya udhibiti wa maeneo hayo hali itaendelea kuwa mbaya zaidi kwa maisha ya vijana wetu, ambao ndiyo tegemeo hapo badaye.

Suala la msingi ni kujipanga kwani hakuna dawa nyingine, kwa kuweka watu waadilifu kwenye mipaka ya nchi ambao hawatakuwa tayari kupokea rushwa ili kupitisha mizigo ya aina hiyo na hata dawa  na vyakula bandia kwani nazo zinapita kwa njia hizo za panya. 

Hakuna kitu kisicho na mwisho, suala ni polisi kujipanga vizuri kwani upo uwezekano wa kushinda vita hiyo hasa kwa kubaini mbinu zinazotumiwa na wafanyabishara hao wajanja.

Lakini pia vita hiyo inaweza kuwa ngumu kutokana na kuwepo kwa mianya ya rushwa, kwani katika maeneo ya mipakani ambako ndiko kwenye mwanya mkubwa wa kuingiza kwa vitu nchini ikiwemo bidhaa bandia bado hakuna udhibiti wa kutosha hasa kutokana na rushwa.

Ulinzi ukiimarishwa katika maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo mipaka, vituo vya usafiri kama vile uwanja wa ndege, bandari na vituo Vikuu vya Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani na kuishinda rushwa kama ambavyo Waziri Samwel Sitta alivyotamka vita dhidi ya dawa za kulevya tutashinda.

Rushwa ambaye ni adui wa haki anaweza kutokomezwa kwa wafanyakazi kulipwa mishahara mizuri pamoja na posho za kuwafanya wasiwe na tama ya kupokea rushwa hakika vitu hivyo vitabaki historia.

Lakini tabia hii ya kuendelea kuwalipa wafanyakazi fedha kiduchi ambazo hazikidhi mahitaji yao inawafanya waingiwe na tama za kijinga na kujikuta wakipokea rushwa kwa sababu ya shida zinazowakabili. 

Wakati umefika Serikali iboreshe hali ya maisha kwa watumishi wake hasa wa jeshi la polisi ili waweze kutimiza wajibu wao ipasavyo na kuepukana na shetani wa rushwa pindi wanaposhawishiwa na watu wasio waadilifu ama wafanyabiashara wanaosafirisha bidhaa bandia. 

Tukishirikiana pamoja na kila mmoja kwa kuona athari hizo hasa wananchi waishio mipakani kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kuhusu vitendo vya uhalifu kilio hicho tutakimaliza.

 

Vita dhidi ya dawa za kulevya isiwe ya msimu iwe endelevu na kila wakati. 

Read more...

Sera zinazohusu mtoto zitekelezwe - Watoto

  • Published in Tanzania

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imetakiwa kuhakikisha kwamba sera zinazohusu mtoto zinatekelezwa ipasavyo kwa kuweka mifumo ya ufuatiliaji ili watoto waweze kutimiziwa haki zao na kujenga jamii bora ya kuwafanya watoto kuwa na furaha wakati wote.

 Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaama hivi karibunu na watoto wanauonda mabaraza ya watoto kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini wakati wa  maadhimisho ya miaka 25 ya mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto ambapo wamedai kusherekea lakini changomoto zao zitekelezwe ili mkataba huo uweze kuwa na tiaja kwao.

Watoto hao walisema serikali imetunga sera nyingi zinazohusu mtoto, hivyo  ni vyema ikapiga hatua kwa kuhakikisha sera hizo zinatekelezwa mfano sera ya kuunda mabaraza ya watoto na zile haki zote zilizowekwa kwenye sheria ya mtoto zinatekelezwa kuacha kutekeleza ni kufanya huo mkataba uwepo kwenye nyaraka lakini kinachofanyika kwa walengwa hakipo.

Katibu wa Baraza la Watoto mkoani Arusha,Rapahel Dennis, alisema Wilaya zina vyanzo vingi vya mapato mfano kodi, zitumike katika kusaidia masuala ya watoto na pia iweke mfuno mzuri wa ufuatiliaji wa matumizi na mapato ya fedha za watoto  na bajet ya watoto ijulikane isiunganishwe na masuala mengine ambayo inafanya watoto kuishi bila kujua kiasi cha bajeti  yao  .

Naye, Mwenyekiti wa Baraza la Watoto, Wilayani Lindi, Hassan Maingu, alizitaja baadhi ya changamoto kuwa ni pamoja na umaskini katika ngazi ya familia unasababisha wazazi kushindwa kutekeleza haki za watoto  kwa kutopatiwa elimu bora na mahitaji mengine ya msingi ambapo serikili ni wajibu kuinua vipato vya wananchi wake katika kuhakikisha watoto watapata mahitaji muhimu kutoka kwa wazazi wao.

Aliongeza kuwa bado jamii haielewi vizuri haki za mtoto na kuelewa nini hasa kilichopo kwenye mkataba wa hazi za mtoto na pengine ulisainiwa kwa malengo gani na kama kuna siku ya kuihadhimisha haki za watoto.

Pia litokuwa na viongozi waadilifu ambao wanatoa kipaumbele katika masuala ya watoto na pia viongozi hao kutumia vibaya fedha zilizotengwa kwa ajili ya watoto hatua ziweze kuchukuliwa ili kuwa fundisho kwa watu wengine wanaotumia vibaya madaraka kwa fedhaa za watoto.

Aidha katika kuadhimisha maadhimisho hayo Shirika la Kimataifa la Save the Children limetoa zawadi mbalimbali zikiwemo baiskeli mbili kwa washindi walioshiriki mashindano ya kuchora na kuandika insha.

Ofisa Habari wa Shirika hilo, Ellen Okoedion,alisema kuwa Tanzania imeweza kuboiresha huduma katika sekta uya elimu na afya lakini bado kuna changamoto ambazo serikali ina wajibu wa kuzitekeleza.

Alisema bado kuna ukinzania katika baadhi ya sheria ambapo  bado hazimlindi mtoto hususani mtoto wa kike ambapo kwenye sheria ya ndoa inaruhusu mtoto kuolewa chini ya umri wa miaka 18 kwa ridhaa ya wazazi.

Aidha  alisema  baadhi ya mira potofu zimekuwa zikimkandamiza mtoto wa kike ambapo baadhi ya makabila yamekuwa yakiwaingiza  watoto wenye umri wa miaka 9 kwenye unyago na kusababisha mtoto kunyanyasika.

....

Read more...

Ukawa wasusa

  • Published in Tanzania

DAR ES SALAAM

Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA wamesema hawatashiriki katika kura ya Maoni ya Katiba inayopendekezwa kwani kufanya hivyo ni kukubaliana na maudhui ya Katiba hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA FREEMAN MBOWE.

MBOWE amesema hawata shiriki katika  mchakato wa kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa na Bunge maalum la Katiba kwani kufanya hivyo ni kubariki kilichomo katika Katiba hiyo.

Amesema Katiba hiyo inayopendekezwa imekosa uhalali siyo kuanzia kwenye Bunge bali tangu mchakato huo kuanza kwa sheria na kuachwa kwa masuala ya kitaifa na kuzarau maoni ya wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi CUF Profesa IBRAHIM LIPUMBA, amesema watawahamasisha wananchi kutokwenda kupiga kura ya maoni ili kuweza kudhirisha kuwa hawakubaliani na Katiba inayopendekezwa.

Nao Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi JAMES MBATIA na Mwenyekiti wa NLD  EMMANUEL MAKAIDI wamesema vyama vinavyounda UKAWA watafanya mambo mengine na kuacha kura hiyo kwa waliopitisha Katiba hiyo.

Kura ya Maoni ya Katiba inayopendekezwa inatarajiwa kupigwa April 30 mwaka huu baada ya Bunge Maalum kumaliza kazi ya kuandika Katiba hiyo.

 

Modest Msangi

Read more...

Tanzania na mabadiliko ya tabia nchi

Mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa yakileta madhara duniani ,nchini Tanzanian mamlaka ya hali ya hewa imelazimika kutoa taarifa maalumu kwa umma kuhusiana na tahadhali ya mabadiliko ya hali hewa katika ukanda wa Pwani kutokana na kuimarika kwa mgandamizo mdogo wa hewa katika eneo la Bahari ya hindi mashariki mwa kisiwa cha Madagascar hali inayoleta mawimbi makali.

Shughuli ya uvuvi katika bahari ya Hindi ni tegemeo kwa uchumi na huduma ya samaki,lakini kwa sasa mambo yamebadilika samaki wanapatikana kwa tabu kufuatia wavuvi kuogopa kuingia Baharini kuvua,huku hali ya usafiri kwa vyombo vya majini ndani ya Bahari hiyo vikikumbwa na hali mbaya kutokana na mawimbi makali.

Hali hiyo ya kuchafuka kwa bahari na hali ya hewa, pamoja na mawimbi makali bahari ya Hindi, ni kilio kikubwa kwa wavuvi wa mwambao huo wanaoendesha maisha yao kwa kutegemea uvuvi, kwani kwa sasa samaki hawapatikani tena kama hapo awali.

 

Hali ya mabadiliko ya tabia nchi, kwa mwaka huu wa 2015 limekuwa si jambo la kawaida, kwani kwa kawaida nchini Tanzaia majira kama haya ya mwezi wa kwanza mpaka wa pili katikati upepo hukata na kuwapa fursa wavuvi kutafuta riziki zao.

Kutokana na mabadiliko hayo ya hali ya hewa,imeathiri upatikanaji wa mazao ya samaki na sasa bidhaa ya samaki imepanda bei kutoka elfu kumi ama ishirini kwa ndoo ya lita kumi hapo awali sasa inauzwa kwa elfu sabini kwa dagaa mchele, na hivyo kumfanya mjasiriamali mwenye kipato cha chini kutomudu kununua bidhaa hiyo.

Read more...

Polisi wamtafuta mtoto aliyetoweka

  • Published in Tanzania

Polisi wametangaza kutoa dau la shilingi milioni tatu sawa na dola 1,700 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa mtoto albino, Pendo Emmanuel aliyetoweka nyumbani kwake na kupelekwa mahali pasipojulikana mwezi uliopita mkoani Mwanza.

Read more...
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.