Menu
RSS
Tanzania

TANTRADE YAWAPONGEZA WAFANYABIASHARA

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), imewapongeza waafanyabiashara nchini kwa kuchangamkia fursa ya kufanya ushirikiano wa kibiashara na Finland kwa kuwa hilo ndilo lengo la Mamlaka.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Biashara ya Ndani-Tantrade, Edwin Lutageruka, wakati wa Semina iliyoandaliwa na mmlaka hiyo kwa ushirikiano na Serikali ya Finland chini ya ubalozi wa Finland nchini na kushirikisha wafanyabiashara wa ndani mia moja hamsini.

Alisema kuwa Semina hiyo imefanyika wakati maonyeshoa ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yakiendelea ili kuwapata wafanyabiashara wengi zaidi na kwamba wafanyabiashara wa ndani wanayo nafasi ya kushirikiana kibiashara, kuwekeza na kupeleka bidhaa nchini Finland hasa katika sekta ya TEHAMA, mitindo na sanaa za mikono pamoja na zao la Korosho.

Alitoa wito kwa wafanyabiashara walioshiriki Semina hiyo kuwasambazia taarifa hiyo wafanyabiashara wengine ili nao waweze kuitumia fursa hiyo ya kufanya biashara na Finland wakiunganishwa na programme maalum iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo ya Finnpartinership.

Akibainisha fursa zilizopo nchini humo Mkurugenzi wa program hiyo SIV AHLBERG, alisema kuwa program hiyo itasimamia kila kitu na kuhakikisha wanawakutanisha ana kwa ana au kimawasiliano wafanyabiashara wa Tanzania na wale wa Finland  kulingana na kile watakachokuwa wamehitaji.

Alieleza kuwa nchi hiyo yenye viwanda vya chuma, kemikali, mashine, vifaa vya umeme, nguo na vyakula imelenga kuwahamasisha watanzania kushirikiana kibiashara kwa kuwa ina mashirikiano ya asilimia mbili tu na nchi za Afrika.

 

Read more...

Tahariri

Hongera Askofu Mapunda, endeleza utume Singida

HATIMAYE Jimbo Katoliki la Singida limepata Askofu wake mpya atakayeendeleza utume kwenye jimbo hilo.

AskofuEdward   Mapunda Dominika hii anatarajiwa kupewa DarajaTakatifu ya Uaskofu na kusimikwa rasmi kuwa askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Singida.

Sisi waTumaini Letu tunampongeza Askofu Mapunda kwa kukubali utume huo kwani kazi iliyopombele yake katika utekelezaji wa majukumu ya uinjilishaji ni nzito na inayohitaji sala za waamini wajimbo hilo.

Aidha tunaendelea kuwapongeza waamini waJimboKatoliki la Singida kwa kupata Askofu huyo na jambo la msingi wanalopaswa kulifanya ni kumpa ushirikiano katika utekelezaj I wa majukumu yake.

Kama inavyofahamika Askofu n I mtendaji mkuu wa kazi za uinjilishaji kwenye Jimbo, hivyo ni jukumu sasa na wanasingida kuhakikisha kazi aliyopewa askofu huyo ya kuchunga kondoo wa bwana inakuwarahisi kwa kumuombea iliafanikishe vema kazi zake.

Tunajua kazi aliyoitiwa Baba AskofuMapunda na MwenyeziMungu kuwachunga kondoo wake kwenye Jimbo la Singida inahitaji maombi na sala kutoka kwawaamini.

Ni wazi kwamba katika kazi yauinjilishaji zipochangamoto nyingi, zinahitaji kupatiwa ufumbuzi kupitia Askofu waJimbo, lakini kubwa nikwanjia ya  sala na  kupitia msaada wa Mwenyezi Mungu.

TunaaminikwambakwaushirikianobainayaMashirikayaKitawajimboni, waamininawatuwenyemapenzimema,  hakika kazi ya uinjilishaji itakuwa rahisi kwa Baba Askofu.

Tuonavyosisi Askofu Mapunda kwa kukubali kwake kufanya utume huo atakuwa chachu na chumvi ya kuleta matumaini pasipo na matumaini, kuondoa chuki palipo na chuki na kuleta upendo pasipo na upendo na kuongeza kasi ya kulitangaza Neno la Mungu.

Tumuombee Askofu wetu Mapunda ili aweze kuwa chimbuko la neema kwa wote katika Kanisa la Tanzania hasa kwenye Jimbo la Singida na kuwa  fanya waamini wajimbo hilo kuimarika zaidi kiroho na kimwili.

Tunamkaribisha, tunamuombeanakumtakiaherina Baraka zaMungu, AskofuMapundaanayesimikwaJulai 5, mwakahuu.

MunguuwabarikiwaaminiwaJimbo la Singida. Amina.

End

 

Read more...

Unywaji viroba waathiri Watoto Kondoa

Na Mary Yuda, Kondoa

Askofu wa Jimbo Katoliki la Kondoa, Mhashamu Bernadine Mfumbusa amesema kuwa watoto wa Jimbo hilo wanakabiliwa natatizo la unywaji wa pombe aina ya viroba.

Aidha amesema kuwepo kwatabia hiyo ni changamoto kubwa inayowamaliza watoto wa Jimbo la Kondoa na hivyo kushindwa kutimiza ndoto zao.

Askofu Mfumbusa alibainisha hayo hivi karibuni katika Ibada ya MisaTakatifu yaKongamano la UtotoMtakatifuKanda yaMasharikina Kati, lililofanyikakwenyeViwanjavyaKanisa la Kiaskofu la RohoMtakatifuKondoa.

AlisemawatotowaJimbo la Kondoawanashindwakutimizandozozaokutokananakuanzakunywapombewangaliwadogo, haliinayorudishanyumamaendeleoyawatotohao.

KutokananahalihiyoAskofuMfumbusaamewatakawazazi na walezi na watoto wa Utoto Mtakatifu kuwa ombea watoto wa Kondoa ili waweze kuondoka na hali hiyo inayohatarisha maishayao.

Naye Askofu wa Jimbo Katoliki la Mahenge, Mhashamu Agapiti Ndorobo amewataka wazazi na walezi nchini kuhakikisha wanawalea vema watoto wao kwani watoto huchangia kuleta neema na Baraka ndani ya familia.

AskofuNdoroboalisemahayohivikaribuniwakatiakifunguaKongamano la UtotoMtakatifu Kanda yaMasharikina Kati lililofanyikakwenyeJimbo la Kondoa.

Alisemakuwa kuna haja wazazi nawalezi nchini kuwafundisha watoto wao fadhila  mkristo kwa kuwa neemana Baraka zinatokana nafadhila za mkristo.

AskofuNdoroboalizitajafadhilahizokuwanipamojanauvumilivu, upendo, kusameheananakusaidiana.

“Mtotoanapokuwanauvumilivunineemakatikafamilianatunatimizafadhilazakimungukwaniwakatimwinginehaliinawezakuwangumukatikafamiliakutokananamatatizondaniyafamilia”,alisemaAskofuNdorobo.

Alisemakuwakatikakutimizafadhilamambo yoteyanawezekanaendapowazazinawatotohaowatajikabidhimbeleyaMwenyeziMungu.

AidhaAskofuNdoroboaliwatakawatotohaokutambuawajibuwaokatikafamiliaikiwanipamojanakufuatafadhilazakikristokwakuwandiouinjilishajikwasababuukristounaonekanakadiriyamaishawanayoishinakumuombaMungu.

AskofuhuyoaliwatakawazazinawalezikuimarishaupendokwawatotowaoikiwemokuwatimiziamahitajiyaonakuyashiriishakatikaJumuiya, Parokianajamiikwaujumlailikuruhusu Baraka zaMungu.

KongamanohilolilifunguliwanaAskofuNdoroboJulaiMosimwakahuu, likiambatananaseminambalimbalikwawatotopamojanawaleziwaonalinatarajiwakufikiakilelechakeJulai 3, mwakahuu.

Kongamanohilokwamwakahulimebebwanakaulimbiuya ‘Haki ya Mtoto ni Malezi’.

 

Read more...

Mnyika adia ofisi ya waziri Mkuu yawakingia kifua mafisadi

  • Published in Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

 

Mbunge wa Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amedai kuwa ofisi ya Waziri Mkuu inawalinda watendaji wa halmashauri wanaotuhumiwa kuhusika na vitendo vya kifisadi kwenye halmashauri zao.

 

Mnyika alitoa madai hayo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa anauliza swali la nyongeza kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

 

Alidai kuwa hali hiyo ndiyo inawafanya baadhi ya watendaji hususan wa Jiji la Dar es salaam kuwa na viburi pindi wanapoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo zilizoainishwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG.

 

Aliongeza kuwa hata Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa ikiondoa mashauri yanayofikishwa Mahakamani.

 

Hata hivyo akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya TAMISEMI, Kassimu Majaliwa aliliambia Bunge kuwa hakuna mtuhumiwa yeyote anayelindwa na Serikali na badala yake Ofisi hiyo inachukua hatua mara baada ya tuhuma kuchunguzwa na vyombo vinavyohusika.

 

Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju alisema kuwa Ofisi yake ndiyo yenye jukumu la kuondoa mashitaka Mahakamani kwa kuzingatia sababu za msingi za kufanya hivyo.

 

End 

Read more...

SIDO yawapa somo Watanzania

  • Published in Tanzania

Na Mwandishi Wetu

Kutokana na hamasa ndogo iliyopo katika ushiriki wa wananchini kwenye maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, Shirika la Kuendeleza Viwanda Vidogo vidogo (SIDO), limewataka wananchi kuhamasika na kwenda kulitembelea banda lao ili kujionea watanzania wenzao waliothubutu.

 

Akizungumza na Tumaini Media kwenye maonesho hayo Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Mhandisi Omari Bakari alisema kuwa katika banda hilo wapo wajasiriamali wengi waliothubutu kujiendeleza, kutumia teknolojia na ubunifu kwa kutengeneza vitu mbalimbali.

 

Mhandisi Bakari alisema kuwa hiyo ni fursa kwa watanzania wengine hususan vijana waliomaliza vyuo kwenda kujionea ni kwa namna gani na wao wanaweza kujifunza kuzitumia fursa za mafunzo, ushauri wa kibiashara na ushauri wa teknolojia ya kisasa ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali Kutoka SIDO na kwa wajasiriamali wenyewe badala ya kuendelea kusubiri ajira Serikalini au katika Mashirika na taasisi binafsi.

 

Akizungumzia mwamko wa wajasiriamali kushiriki matika maonesho hayo Mhandisi bakari amesema kuwa,umekuwa mkubwa kwani maombi ni mengi kutoka mikoa yote ya Tanzania lakini mwamko wa wananchi kutembelea maonesho hayo kwa mwaka huu ni mdogo.

 

Wakizungumza katika maonesho hayo kwenye Banda la SIDO wajasiriamali kutoka mipakani Noela Gachuma kutoka Boda ya Silari, Edran Mwaku kutoka boda ya Rusumo,

 

Aisha Kisoki kutoka mpaka wa Horohoro na Rose Mlay kutoka mpaka wa Horiri Moshi wamekishukuru Chama cha wafanyabiashara Wanawake (TWCC) kwa kuwawezesha kufanya biashara na kujikwamua na unyanyasaji wa kijinsia kwenye mikoa yao.

 

Wajasiriamali hao wamesema licha ya TWCC kuwawezesha bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kutozwa ushuru mkubwa kwa mizigo wanayoisafirisha kwenye mipaka ya Tanzania na Kenya na Tanzania na Rwanda na hivyo kuwadidimiza kibiashara.

 

 

Read more...

Kanisa lililotumika Zahanati kwenye Vita Kuu ya Dunia lawa kivutio -Tanzania

Na  Mary Yuda

Kondoanimiongoni mwa miji yenye Historia kubwa katika ukanda wa kati nchini Tanznaia.Wilaya ya Kondoa inapatikana mkoani Dodoma ambapo nimakao makuu ya Serikali ya Tanzania.

Wilaya  ya Kondoa iliyo katika mkoa wa Dodoma wakati wa enzi za biashara ya utumwa mji huo ulitumika  kama kituo cha kupumzikia watumwa waliyokuwa wakipelekwa Pwani.

Kwa kipindi hicho eneo hilo lilikuwa likitumika kama njia moja kuwapitisha watumwa hao inayoitwa mtaa wa ubembeni,jina linalotokana na kukaliwa na kabila  laWabemba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambayo zamani ilikuwa ikifahamika kamaZaire ambayo 1900, ilipiga marufuku biashara ya utumwa.

Asili ya neno Kondoa linatokana na Mto unaopita karibu na mji huo ambao watu wa kabira la Warangi waliuita mwairangi Koondo na wakati huo Kondoa ikijulikana kama ula, kikiwa ni soko la biashara  iliyokuwa ya kuuziana  na kununuliana vitu, mahali hapo kwa warangi paliiitwa “wula”ikiwa na maana ya nunua.

Mitaa ya mji wa Kondoa ina majina ya matukio au watu maarufu wa zamanai  ikiwemomtaa wa Bembeni ambapo walikaa kabila la Wabemba kutoka DRC mara baaada ya biashara ya utumwa kufungwa na mabaki ya kabila hilo wapo hadi sasa katika mji huo wa Kondoa.

Mtaa mwingine ni Chemchem ambao unatokana na chemchem isiyokauka inayotoa maji ya moto nyakati za asubuhi, Iboni ni mtaaa mwingine ambao unatokana mtu maaarufu sana na mtawala wa eneo hilo aliyehemishika kwa hekima na busara zake na mtaa wa kwa Pakacha uliotokana na jina la mtawala ambaye alikuwa Mwanangwa wa eneo hilo.

Wakati mtaa wa bomani  unatokana na neno Boma  lilokuwa jengo la watawala wa Kijerumani kwa kuendeshea shughuli  zote za utawala na kwa sasa jengo hilo ni ofisi ya Mkuu wa Wilaya, mtaa wa Mningani umetokana na kuwepo na miti ya mninga na upo karibu na uwanja wa ndege.

Mtaa wa maji ya Shamba, umetokana na kuwepo kwa bwawa linalotumiwa kwa kilimo na kumwagilia mbogamboga na Mnarani, mtaa huu ndipo  mahali palipojengwa  mnara wa kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961. Kondoa ina makabila mengi ikiwemo Warangi,Wasandawe,Waalawi,Wagogo, Wanyaturu na Waberbeig.

Baada ya kuifahamu Kondoa, hebu tuangalie historia ya uinjilishaji katika Jimbo hilo, nikianzia katika Parokia ya Kondoa ya Roho Mtakatifu ambayo ni Parokia mama yenye kiti cha Kiaskofu ambapo ni makao makuu ya Jimbo katoliki la Kondoa.

Kijografia Jimbo Katoliki Kondoa lipo nyanda za kati mwa Tanzania ambapo kwa upande wa Kusini limepakana na Jimbo Kuu la Dodoma, Kaskazini limepakana na Jimbo la Mbulu, kwa upande wa Magharibi limepakana na Jimbo la Singida na  Mashariki limepakana na Jimbo Kuu la Arusha.

Jimbo Katoliki la Kondoa liliundwa Machi mwaka 2011 likiwa Jimbo katoliki la 31 nchini ambalo ni sehemu ya mpango wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania(TEC).

Ukristu ulianza kuingia Kondoa kwa mara ya kwanza mwaka 1907 kupitia Mmisionari wa Shirika la Roho Mtakatifu  Padri Andrea Krieger aliyeitwa “kafefe ambaye alikuwa Mmisionari wa kwanza kupanda mbegu ya Injili katika Jimbo hilo.

Kwa mujibu wa Katibu wa jimbo hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa PMS jimboni humo, Padri Pascal Kilongo, Inasemekana jina la kafefe lilitokana na neno la kirangi “afafa”yaani mgumu au “Kufyefya”  mkali kutokana na kufanya utume wake katika mazingira magumu.

Jimbo hilo lina ukubwa wa kilomita za mraba 13,210, likiwa na idadi ya watu 541,345 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2000 na kwamba ina idadi ya wakatoliki Jimboni humo ni 50,000 wakiwa na Parokia 12 na Mapadri wa Jimbo 18, Mapadri watawa wawili, Mashirika ya Kitawa ya wanawake mawili na Shirika la Mtakatifu Jema wa Dodoma na Shirika la habari njema Babati.

Wakati Mashirika ya watawa wa kiume yanayofanyakazi katika jimbo hilo ni moja ambalo ni Shirika la Mateso la Bwana Yesu Kristo na kwamba lina jumla ya Waseminari wakubwa tisa.

Safari ya Padri Andrea Krieger kuja Kondoa  ilianzia Kibosho Moshi ambapo alifuatana na Bruda Timoteo na makatekista wanne wa kabila la Kichaga  akiwemo Katekista Oktavian (Otto),Albert, Petri na Zefrin, ambaye aliadhimisha Misa ya kwanza kisese Agosti 18  mwaka 1907  na kwamba Ukristu ulipofika Kondoa Uislamu ulikuwepo miaka mingi iliyopita.

Padri Kafefe alihubiri sehemu za Choray, Bubu,Chaangaa na Wisi , hatimaye alipata eneo la ambapo kanisa la Parokia ya Kondoa lipo  hadi sasa.

Ujenzi wa kanisa hilo ulikamilikamwaka 1910na kwamba alifanikiwa kuwabatiza wakristo wa kwanza 60 katika Kanisa la Kondoa katika sikukuuya Krismasi mwaka 1910.

Imani kabla ya vita Kuu ya kwanza yaani kuanzia  mwaka 1907 -1913, mwanzoni Padri Kafefe aliwaandaa Makatekista  11 wenyeji wakuchukua nafasi ya wale aliofuatana nao kutoka Moshi.

Aidha alifanikiwa kuanzisha vigango 13 vya Parokia ya Kondoa ikiwemo Kigango cha Kolo,Tumbelo,Changaa, Loo, Ausia, sega,Dalai,Kwancharai, Bolisa, Muluwa, Baura, Ihalala na Haubi, na baadae Haubi ilikuwa Parokia chini ya Mapadri wa Mateso( Passions Fathers).

Hali ya uinjilishaji wakati wavita Kuu ya kwanza 1914- -1918 haikuwa nzuri kwani shughuli za kichungaji ziliathirika ambapo wakati huo Padri Kafefe alikuwa likizo Ulaya naye Bruda aliyekuwa Parokiani Kondoa alijiunga na Wajerumani wenzake kupigana na Waingereza.

Wakati wa vita hiyo ikiendelea jengo la Kanisa la Kondoa liligeuzwa kuwa zahanati  ya kutunzia na kutibu majeruhi wa vita jambo lililosababisha Kanisa kupigwa mabomu yaliyobomoa paa na kuua majeruhi waliolazwa kwenye kanisa hilo na kwamba iliwalazimu wakristu wa Haubi kwenda kusali Kurhio ambapo ni mbali kutoka Haubi.

Desemba 24, mwaka 1920 Padri Andrea Krieger alirudi na alilazimika kufufua upya imani katoliki  hasa kwa wakristo wachanga waliokosa mchungaji kwa muda mrefu.

Aidha miaka ya 30 Dodoma liligawanywa katika sehemu Kuu tatu  ambapo Kondoa ilikuwa chini ya Vicariate ya Kilimanjaro, Kurio, Bahi na Farakwa  zilikuwa chini ya vicariate ya Bagamoyo na Bihawana  ilikuwa chini ya Vicariate ya Iringa.

Mwaka 1935 Dodoma ilifanywa kuwa Prefecture Apostolic na Padre Disma Giannotti aliyeteuliwa  kuwa Prefect wa kwanza.

 Miaka miwili baadaye Novemba 23 mwaka 1937 Monsinyori StanslaoAmbrozini aliteuliwea kuwa “Prefect Apostolic” wa pili na baada ya kufariki nafasi yake ilichukuliwa na Padre Teodoro Mateo  na Jimbo la Dodoma lilifanywa kuwa Vicario Apostolic Desemba 23 mwaka 1951 chini ya uongozi wake Askofu Jeremia Pesce, Cp alipowekwa wakfu  kuwa Askofu  Desemba 3 mwaka 1951.

Mwaka 1972 Askofu Mathias Isuja Joseph alikuwa Askofu wa Kwanza mzalendo wa Jimbo la Dodoma wakati Mhashamu Yude Thadeus Ru’waichi  alikuwa Askofu wa Jimbo hilo mwaka 2005 – 2011 na Askofu Gervas John Mwasakhabile Nyaisonga kutoka machi 17, 2011.

Jimbo la Kondoa liliundwa Machi 12, mwaka 2011 kwa tamko la Baba Mtakatifu Benedict XVI na Askofu wa kwanza wa Jimbo hilo ni Askofu  Bernadine Mfumbusa ambaye mpaka uteuzi wake alikuwa mkufunzi Mwandamizi katika Idara ya Mawasiliano na makamo Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Mwanza.

Binafsi nimeyafurahia mazingira ya uinjilishaji Kondoa, kwani Kondoa ni Jimbo lililo na Wakristu wachache kuliko Waislamu lakini watu hawa wa imani tofauti wamekuwa wakishirikiana vema bila kujali tofauti zao kama ilivyo katika baadhi ya Majimbo ambayo yana idadi ndogo ya Wakristu.

Jimbo hilo limebarikiwa kupata Maaskofu wazawa watatu akiwemo Askofu Mstaafu Mhashamu Matthias Isuja  wa Jimbo la Dodoma, Askofu Bernadine  Mfumbusa Jimbo la Kondoa na Askofu Agapiti Ndorobo wa Jimbo la Mahenge.

 

 

Read more...

TAHARIRI

 

Serikali iwe makini na uandikishaji Wapigakura

ZOEZI la uandikishaji wapigakura katika daftari la kudumu la wapigakura kwa mfumo wa kieletroniki wa Biometric Registration Voter (BVR), linaendelea nchini.

Hivi karibuni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema katika taarifa yake kwamba inakusudia kuwafikisha mahakamani wananchi zaidi ya 100 wa Mkoa wa Njombe kwa madai ya kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura.

Naibu Katibu wa Tume hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Daftari na Tehama, Dk. Sisti Cariah alisema wananchi hao wamebainika kwa kutumia teknolojia ya BVR na uhakiki huo utaendelea katika maeneo yote nchini.

Alisema picha na majina ya watuhumiwa hao vimepelekwa kwenye idara zinazohusika huku akiwaonya wananchi ambao hawajaandikishwa kuacha kudhani kwamba wanaweza kujiandikisha zaidi ya mara moja bila kubainika.

Haki hii ni jambo la baya ambalo linaweza kuleta shida katika uchaguzi hasa endapo katika baadhi ya maendeleo ikishindikana kubainika kutokana na changamoto mbalimbali.

Lakini pia lipo suala la raia wasio watanzania hasa katika maeneo ya mipakani ambapo bila ya Serikali kuweka udhibiti mkali na kutilia mkazo suala la umakini hakika wataandikishwa watu ambao sio watanzania.

Tuoonavyo sisi ni vema  licha ya kazi hiyo ya uandikishaji kukamilika katika Mikoa mitano nchini ikiwemo ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa na Njombe, bado juhudi za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa na serikali kudhibiti wasio raia kuandikishwa hasa katika mikoa ambayo bado zoezi hilo halijafanyika.

Hali ya wananchi kujiandikisha zaidi ya mara moja na wengine kudai kusahaulika kuandikishwa kwenye daftari hilo hasa katika mikoa ambayo tayari zoezi hilo limekamilika inaweza kuleta shida na kuzusha mijadala ikiwemo kuibua hofu wananchi kuona uwepo wa uchakachuaji kufanyika katika Uchaguzi Mkuu.

Lakini pia jambo lingine ambalo linaonekana kwamba huenda zoezi hilo lisifike kweye mikoa yote ni kutokana na muda unavyozidi kwenda zaidi ikilinganishwa na kasi ya zoezi hilo huku NEC, ikitangza kusogeza mbele uandikishaji wapigakura kwenye mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga na Morogoro kutokana na marekebisho ya mipaka ya kiutawala ya kata, mitaa, vijiji na vitongoji yaliyofanywa na Tamisemi.

Sisi tunawasihi wananchi katika mikoa ambayo zoezi hilo linatarajiwa kuendelea wajitokeze kwa wingi na kujiandikisha, tena mara moja ili waweze kupata haki yao msingi kushiriki Uchaguzi Mkuu badaye mwaka huu na kumchagua kiongozi wanayeona anafaa.

Mungu Ibariki Tanzania.

 

Read more...

Watendaji Wizara zilizotumia vibaya fedha za bajeti wawajibike-Askofu

Na Alex Kachelewa

IMEELEZWA kuwa watendaji wa Serikali na Mawaziri ambayo Wizara zao hazikufanya vizuri katika matumizi ya fedha za bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo wanatakiwa kuwajibika kwani wametumie vibaya fedha za umma.

Kauli hiyo imekuja wakati huu ambapo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilikualikiendelea na vikao vyake vya bajeti mjini Dodoma, ambapo tayari Wizara mbalimbali zimekwisha pitisha bajeti zake.

Kutokana na hali ya kisiasa kuelekea ucuaguzi mkuu bajeti hizo zimepitishwa na  idadi kidogo ya wabunge hasa wa viti maalum huku idadi kubwa ya wabunge wakiwa hawapo kwenye vikao hivyo.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Mhashamu Method Kilaini, wakati akizungumza na Tumaini Letu katika mahojiano maalumu kuhusiana na bajeti ya fedha zinazotolewa kwa Wizara mbalimbali nchini ikiwemo ya mwaka wa fedha 2014/2015 na 2015/2016.

“Bajeti hata kama inapitishwa na wabunge wachache lakini jambo la msingi inatakiwa iwe imetengenezwa vena na hasa wale technical Staff, maana wale ndio wanaoendesha serikali kuanzia Katibu Mkuu wa Wizara”,alisema Askofu Kilaini na kuongeza kuwa:

Lakini kama hao watafanya vibaya katika kutengeneza bajeti hiyo hakika inakuwa shida kubwa kwani Waziri yeye ni kiongozi wa kisiasa na sio mtaalam anaweza kuhamishwa wizara moja kwenda nyingine”,alisema.

“Hivyo kwa Wizara ambazo zilipokea fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo kwa bajeti zilizopita na hakuna utekeleza wowote fedha zile zimeliwa kwa namna moja ama nyingine Mawaziri wanatakiwa kuwajibika na hata kujiuzulu”,alisema Askofu Kilaini.

Alisema kuwa na ndio maana ikapendekezwa kwenye Katiba mpya kupo kwa kipengele kinachoeleza Waziri asiwe mwanasiasa kwa sababu akiwa mtaalam ama wa Maji na nyingine atafanya kazi yake katika wizara husika kama mtaalama na hivyo kuondoa masuala ya kupiga siasa katika mambo ya msingi.

Kwa mujibu wa Askofu Kilaini kwa sasa bajeti nyingi zimepitishwa na idadi ndogo ya wabunge hali inayoweza kutia mashaka kwa wanachi, endapo hazikutengenezwa vema kwani wabunge wengi wa kuchaguliwa wamerudi majimboni kwa ajili ya kujipanga na kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu badaye mwaka huu.

Alisema zipo wizara ambazo kwa namna moja ama nyingine zimeomba fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo lakini zinashindwa kutekelezwa kutokana na ufinyu wa bajeti hasa kwa kutopatiwa fedha zote zilizoombwa huku Wizara zingine zikitumia vibaya fedha hizo za miradi.

Akizungumzia hali ya kisiasa nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu, Askofu Kilaini alisema hatua ya sasa ni ya vyama vya siasa ambapo watu mbalimbali wenye nia wanachukua fomu za kuomba kuteuliwa, lakini bado uhalisia wa nani atakuwa Rais haujafajamika hadi mchujo utakapofanyika ndipo wananchi wataelekezwa namna ya kufanya kumpata kiongozi bora.

“Kwa sasa hii ni inaonesha wazi kwamba demokrasia imekua na kila mtu anaweza kwenda kuchukua fomu hata kama ni darasa la saba ama la pili si kinachotakiwa ni fedha bwana…wakati ukifika itajulikana anayewania Urais ni nani na wananchi wafenye nini ili kumchagua kiongozi bora”,alisem Askofu Kilaini.

Alisema kuwa jambo la msingi kwa wananchi ni kujiandaa na kujipanga ili wapate muda wa kuwauliza maswali watu watakaoteuliwa na vyama vyao jinsi ya kufanikisha ahadi zao baada ya kupata nyadhifa mbalimbali za uongozi.

Kwa sasa Watu wengi waliojitokeza kutangaza nia na kuchukua fomu kwa upande wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaendelea na harakati za kusaka wadhamini katika Mikoa mbalimbali nchini wakisubiri hatua ya mwisho za mchujo ndani ya chama chao.

Hivi karibuni wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walipinga vikali bajeti ya Wizara ya Maji wakidai fedha za miradi ya maji katika kipindi cha mwaka jana ambayo miradi yake haikutekelezwa kama ilivyokusudiwa wakida fedha hizo zimeliwa.

Wabunge hao walisema kuwa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maji haikuweka bayana namna ya utekelezaji wa miradi ya maji vijijini.

Wakichangia bajeti hiyo wabunge hao walidai kuwa hotuba hiyo imetoa taarifa za uwongo kuwa miradi ya maji vijijini imetekelezwa kwa kiwango kibwa jambo walilosema halina ukweli wowote.

Mbunge wa Rungwe Mashariki Profesa David Mwakyusa aliitaka Wizara hiyo kuweka takwimu wazi ni vijiji vingapi vimefikiwa na miradi hiyo ya maji kuliko kutaja kwa jumla ya asilimia.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ether Bulaya aliitaka Wizara hiyo, kutowakumbatia wakandarasi wazembe wanaochelewesha na kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maji vijijini.

Bulaya alisema wakandarasi hao wamekuwa na utendaji mbovu na hawana sifa zinazostahili hivyo wamekuwa wakileta taarifa za uwogo kwa wananchi na kuwalazimisha wananchi kupokea miradi isiyokamilika.

Aidha kwa upande wake David Silinde Mbunge wa Jimbo la Mbozi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEDMA) na Mbunge wa Nkasi, Ally Mohamed Kesi walilalamikia taarifa walizodai ni za uwongo zilizoko kwenye hotuba hiyo kuhusu  utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji vijijini.

Read more...

‘Vyombo vya habari Jimbo Kuu Dar vyenu Waamini’

  • Published in Tanzania

·        Parokia Kipawa yanyakua tena Mbuzi

Na Mwandishi Wetu

Waamini wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wametakiwa kuviona vyombo vya habari vya jimbo hilo vyao na hivyo wanapaswa kuvisaidia kwa hali na mali.

Changamoto hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Tumaini Media, Padri Paul Haule, alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi ya mbuzi kwa washindi wa promosheni ya shinda mbuzi iliyoendeshwa na Gazeti Tumeini Letu.

Alisema kuwa vyombo hivyo ni vya waamini na kwamba watendaji wake wako kwa ajili ya kuwezesha kazi ya uinjilishaji.

Aidha aliwataka mawakala wanaouza gazeti la Tumaini Letu kuendelea kujitolea na kuliwezesha gazeti hilo kuwafikia wasomaji wengi na kurahisisha kazi ya uinjilishaji.

Alisema kazi inayofanywa na mawakala ni ya uingilishaji kwani wanasambaza gazeti lenye kubeba mambo mbalimbali ikiwemo habari za kanisa kwa ajili ya kuwafikishia wengine.

Katika shindano hilo Parokia ya Kipawa imeibuka mshindi kwa mara ya pili mfulululizo ikifuatiwa na Parokia ya Luhanga huku Parokia ya Mbagala ikishika nafasi ya tatu.

Mbali na Parokia hizo tatu Parokia 20 zilizofanya vizuri kwenye promosheni hiyo ni pamoja na Parokia za Mbezi Louis, Yombo Kiwalani, Msewe, Chang’ombe, Salasala, Kimanga, Mbezi Beach, Tabata, Livuvia na Kijichi.

Zingine ni Parokia ya Kizinga, Kilungule, Chanika, Tegeta, Mwananyamala, Oysterbay, Kibaha, Segerea, Hananasifu na Parokia Kuu ya Mtakatifu Yosefu.

Read more...

Mrema akana kutafuna fedha za Jimbo

  • Published in Tanzania

Na Mary Yuda

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) Agustino Mrema amekanusha tuhuma za kutumia vibaya fedha za mfuko wa Jimbo la vunjo na kusema hizo ni hujuma zakutaka kumuondoa katika jimbo hilo.

Hatua hiyo ya Mrema imekuja kufuatia kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulaahman Kinana hivi karibuni katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Jimbo la Vunjo na kusema Mrema anafuja fedha za mfuko wa Jimbo hilo.

“Wanataka kuvuta TLP ili ipoteze Jimbo la Vunjo na kwamba hakuna yeyote atakayeweza kunishinda katika Jimbo la Vunjo”, alisema Mrema.

Akizungumza katika mkutano Mkuu wa Chama hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mrema alidokeza kuwa mfuko huo unakusanya kiasi cha shilingi milioni arobaini na mbili kwa mwaka na si milioni mia kama ilivyosema na Kinana.

Katika hotuba yake iliyojaa malalamiko Mwenyekiti huyo wa TLP amemuomba Rais Jakaya Kikwete  amuagize Kinana  akamuombe radhi katika Jimbo la Vunjo katika mkutano wa hadhara kama alivyofanyawakati akimchafua.

Akizungumzia hali ya usalama nchini, Mrema alieleza kusikitishwa na migogoro mbalimbali inayoendelea nchini  ikiwemo migomo, migogoro ya dini na hivyo kuwaomba viongozi wa Serikali kujitokeza kukemea hali hiyo ili kuiepusha nchi katika hali machafuko.

Katika hatua nyingine mgombea mtarajiwa wa urais kupitia TLP Maximiliani Lyimo alidokeza kuwa uamuzi wake umekuja kufuatia sera za chama hicho na kwamba lengo la TLP ni kuondoa umaskini kwa Watanzania endapo watapata nafasi hiyo.

“Chama chetu ndicho chenye sera nzuri  kushinda vyama vyote na kwama Agenda Yetu Kuu Katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba tutaomba iwe Futa umaskini kwa Tanzania”,alisema Lyimo.

Hata hivyo ameyataja mapendekezo ya TLP kwa uchaguzi Mkuu ujao  kuwa ni pamoja na wagombea watakaopitishwa rasmi na vyama vyao kutafuta muafaaka wa kitaifa wa wa kutazama manmboo mbalimbali ikiwemo suala la katiba .

Suala lingine ni klutafuta Siku maaalum ya kufanya maombi ya kitaifa kumuomba Mungu awavushe salama katika magumu yote ndani ya Taifa la Tanzaniana kwamba maonmbi hayo yashirikishe watu wa dibni zote.

“ Nina muomba Rais wa nchi  kuona umuhimu wa kufanya maombi maaana penye hitaji kubwa na zito kama hali ilivyo kwa sasa ni kiongozi Mkuu wan chi tu ambaye huweza kuita maombi na Mungu akasikia na kujibu kwa haraka  na kwa usahiii”,alisema Lyimo.

End

Read more...
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.