Menu
RSS
Michezo

Jeptoo kufika mbele ya tume ya riadha Kenya

  • Published in Michezo

Shirikisho la Riadha nchini Kenya AK litaisikiliza kesi inayomkabili Rita Jeptoo Alhamisi wiki ijayo, huku mkimbiaji huyo wa marathon akiamriwa kuhudhuria kikao hicho pamoja na makocha wawili na wakala wake.

AK imesema katika taarifa kuwa tume yake ya matibabu na kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu itaendesha kikao hicho katika makao makuu ya shirikisho hilo mjini Nairobi.

Jeptoo, mshindi mara tatu wa Boston Marathon na bingwa mara mbili wa Chicago Marathon, aligundulika kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini nchini Kenya mwezi Septemba. Wiki chache baadaye akashinda taji lake la pili mfulilizo la Chicago.

Alitarajiwa kutangazwa mshindo wa mashindano makuu ya Marathon Ulimwenguni na kupata kitita cha dola 500,000 wakati ilipofichuliwa kuwa vipimo vimeonyesha alitumia dawa zilizopigwa marufuku. Vipimo vya pili vilivyofanywa mwezi uliopita mjini Lausanne katika maabara ya Shirika la Kupambana na Dawa zilizopigwa marufuku Ulimwenguni – WADA viligundua kuwa alitumia dawa hizo.

Jeptoo anakabiliwa na adhabu ya kupigwa marufuku miaka miwili. AK imesema pia imewaita makocha Claudio Berardelli na Noah Busienei, na wakala wa Jeptoo Federico Rosa katika kikao hicho cha Januari 15. Maafisa wa riadha Kenya wanawalaumu makocha wa kigeni na maejenti kwa kuhusika na visa hivyo.

Read more...

Stars maboresho kuivaa Rwanda

  • Published in Michezo

Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kitacheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda itakayofanyika Januari 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza

Mechi hiyo ni sehemu ya programu ya Kocha Mart Nooij kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya mechi za mchujo michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN).

Mechi za mchujo za michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Rwanda zinaanza Mei mwaka huu.

Kocha Nooij anatarajia wakati wowote kutangaza kikosi cha timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambacho kitakusanyika Januari 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam, na siku moja baadaye kwenda jijini Mwanza.

Read more...

Timu zaendelea na maandalizi ya AFCON

  • Published in Michezo

Maandalizi katika kombe la mataifa ya Afrika yanaendelea, ambapo timu mbali mbali zinazoshiriki mashindano hayo ya timu 16 nchini Guinea ya Ikweta yatakayoanza tarehe 17 mwezi huu zinatangaza vikosi vyake

Algeria imethibitisha leo kuwa imemuita kikosini Ahmed Kashi kwa mara ya kwanza katika kikosi hicho na mlinzi Liassine Cadamuro kuchukua nafasi za Essaid Belkalem na Mehdi Abeid ambao ni majeruhi.

Kashi , mzaliwa wa Ufaransa kutoka Metz hajawahi kuitwa katika kikosi cha Algeria, lakini Cadamuro , ambaye anaichezea klabu ya Osasuna nchini Uhispania, alikuwamo katika kikosi cha Algeria kilichoshiriki katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwaka jana pamoja na fainali ya kombe la mataifa ya Afrika nchini Afrika kusini miaka miwili iliyopita.

Mchezaji soka bora wa mwaka katika bara la Afrika atajulikana siku ya Alhamis wiki hii , wakati atakapotangazwa katika sherehe kubwa iliyoandaliwa mjini Lagos nchini Nigeria. Baadhi ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na mchezaji wa kati wa Manchester City na timu ya taifa ya Cote D'Ivoire Yaya Toure ambaye ni mchezaji bora wa sasa, Pierre Emerick Aubamiyang wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Gabon na Sofiane Feghouli wa Valencia ya Uhispania na timu ya taifa ya Algeria.

Read more...

CR7 ashinda Ballon d'Or 2014

  • Published in Michezo

Cristiano Ronaldo aliwapiku Manuel Neuer na Lionel Messi na kushinda tuzo ya Ballon d'Or, lakini kocha wa timu ya taufa Joachim Löw na kiungo wa Wolfsburg Nadine Kessler walikuwa washindi wa Ujerumani

 FIFA Ballon d'Or Gala Cristiano Ronaldo Weltfußballer 2014 12.01.15

Cristiano Ronaldo alishinda tuzo yake ya tatu ya mchezaji bora wa mwaka ulimwenguni - FIFA Ballon d'Or 2014 na kumshinda mlinda lango wa Ujerumani Manuel Neuer na Muargentina Lionel Messi.

Neuer aliibuka katika nafasi ya tatu nyuma ya mshindi mara nne wa tuzo hiyo Lionel Messi katika kura zilizopigwa na manahodha na makocha wa timu za taifa kutoka nchi 209 wanachama wa FIFA, pamoja na waandishi habari kadhaa walioteuliwa.

 Joachim Löw FIFA Ballon d'Or Welttrainer 2014 12.01.15

Joachim Löw kocha bora wa mwaka wa 2014

Ujerumani hata hivyo haikuondoka Zurich bila ya tuzo yoyote. Katika kitengo cha wanawake, Kiungo wa Wolfsburg Mjerumani Nadine Kessler aliwapoku Marta wa Brazil na Mshambuliaji wa Marekani Abby Wambach kwa kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora mwanamke ulimwenguni. Kocha wa Wolfsburg Ralf Kellermann alichaguliwa kuwa kocha bora wa kandanda la wanawake.

Kellermann aliiongoza timu ya Wolfsburg akiwemo Kessler kushinda mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili mfululizo.

Kocha wa timu ya Ujerumani Joachim Löw alishinda tuzo ya kocha bora wa mwaka, mbele ya Carlo Ancelloti wa Real Madrid na Diego Simeone wa Atletico Madrid.

James Rodriguez alishinda tuzo ya Puskas ya goli bora la mwaka, kutokana na kombora alilofyatua langoni wakati akiichezea Colombia dhidi ya Uruguay katika Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.

Timu ya bora ya mwaka ya FIFA ni kama ifuatavyo: Manuel Neuer (Ujerumani, Bayern Munich) - Sergio Ramos (Uhispania, Real Madrid), Thiago Silva (Brazil, PSG), David Luiz (Brazil, PSG), Philipp Lahm (Ujerumani, Bayern Munich) - Andres Iniesta (Uhispania, Barcelona), Toni Kroos (Ujerumani, Real Madrid), Angel Di Maria (Argentina, Manchester United) - Arjen Robben (Uholanzi, Bayern Munich), Lionel Messi (Argentina, Barcelona), Cristiano Ronaldo (Ureno, Real Madrid)

Read more...

Maandalizi:Kombe la Mataifa ya Afrika

  • Published in Michezo

Mlinzi wa Orlando Pirates Ayanda Gcaba ameitwa kwenye timu ya taifa ya Afrika Kusini Bafanabafana ili kuziba nafasi ya Patrick Phungwayo.

Bafanabafana inashiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika michuano itakayoanza Januari 17 mwaka huu.

Phungwayo ambaye naye ni mchezaji wa Orlando Pirates alilazimika kurudi nyumbani baada ya kupata majeruhi ambayo hayatamwezesha kuitumikia timu yake ya taifa.

Kocha wa Bafana bafana Epharaim Shakes Mashaba amesema amesikitishwa kwa kumkosa Phungwayo lakini ameonyesha kuwa na matumaini na mbadala wa mchezaji huyo Ayanda Gcaba

wakati huo huo mashabiki wa timu ya taifa ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo nayo itashiriki mashindano hayo wamekuwa na matumaini ya timu yao kufanya vizuri na hata kunyakua kombe hilo.

Read more...

Birthday’,Krismasi ya Okwi vyavurugwa

  • Published in Michezo

Na Arone Mpanduka

TIMU ya soka ya Kagera Sugar imeonekana kuvuruga mipango ya mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi ambaye hupendelea kutumia muda mwingi kusheherekea siku yake ya kuzaliwa pamoja na sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.

Okwi ambaye alizaliwa Disemba 25 mwaka 1992 huko nchini Uganda, kila mwaka amekuwa na mazoea ya kusheherekea sikukuu za Krismasi na mwaka mpya akiwa kwao nchini Uganda lakini safari hii analazimika kuitumikia timu yake ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Disemba 26 mwaka huu.

Hiyo inamaanisha kwamba Okwi hatoweza kusheherekea vizuri siku yake ya kuzaliwa ambayo huwa ni Disemba 25 kila mwaka.

Akizungumza na Tumaini Letu kwa njia ya simu hivi karibuni wakati timu ilipoweka kambi Zanzibar, Kocha mkuu wa timu ya Simba Patrick Phiri alisema walitarajia mchezaji huyo kujiunga na wenzake siku moja kabla ya Krismasi akitokea Uganda ambako alifunga ndoa ya kimila.

 

“Ni kweli, Okwi hayupo kambini lakini atakuja kesho(Disemba 24),”alithibitisha kocha huyo mwenye uraia wa Zambia.

Kwa mara ya mwisho Okwi aliadhimisha siku hiyo akiwa nchini Uganda, siku ya Disemba 25 mwaka 2013 ambapo alitumia muda mwingi kusherehekea hadi kufikia mwaka mpya wa 2014.

Mara nyingi Okwi alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya Habari akidai kwamba anaiheshimu sana siku yake ya kuzaliwa na ndiyo maana hupenda tarehe hiyo imkute nyumbani kwake Uganda pamoja na sikukuu ya mwaka mpya.

 

Namba za jezi zake

Kwa kudhihirisha kwamba anathamini sana siku yake ya kuzaliwa, Okwi hupenda kuvaa jezi yenye namba 25 mgongoni katika klabu anazochezea, ambayo pia ni namba ya tarehe ya kuzaliwa kwake.

Mfano mzuri ni pale alipojiunga na Simba kwa mara ya kwanza na kuchagua jezi namba 25 na kisha kuchagua namba hiyohiyo wakati alipojiunga na Yanga hivi karibuni, kabla ya kurejea tena Simba na kudai namba yake 25.

Mwezi Oktoba mwaka huu, Okwi alirejea Simba akitokea Yanga na kukuta jezi yake namba 25 ikiwa inavaliwa na beki Issa Rashid ‘Baba Ubaya’lakini baadae ukafanyika utaratibu na akarejeshewa jezi yake.

 

Hali hiyo pia ipo kwenye timu yake ya taifa ya Uganda The Cranes ambapo hivi sasa Okwi anavaa jezi namba 25 kutoka katika namba saba aliyokuwa akiivaa hapo awali.

Pia Okwi ameijengea imani kubwa namba hiyo ambapo mara zote huamini kwamba jezi hiyo ndiyo inampa mafanikio pindi anapokuwa uwanjani.

 

‘Birthday’ yake huzisumbua timu

Mara nyingi Okwi amekuwa na desturi ya kutorejea klabuni kwake kipindi cha sikukuu za Krismasi na mwaka mpya, hasa Sikukuu yaKrismasi ambayo huadhimisha pia tarehe ya kuzaliwa kwake.

Tabia hiyo imekuwa sugu kwa mshambuliaji huyo tangu alipojiunga nayo kwa mara ya kwanza mwaka 2010 hadi kufikia mwaka 2013.

Wakati mwingine uongozi umekuwa ukimtishia kumkata mshahara wake, jambo ambalo pia lilikuwa sugu kwake.

Hata alipojiunga na Yanga mwishoni mwa mwaka jana, Okwi alikuwa bado akiisumbua timu hiyo, mfano mzuri ni mapumziko ya mwezi Disemba mwaka jana baada ya mechi ya Nani Mtani Jembe ambayo Yanga ilifungwa 3-1 ambapo yeye alifunga goli moja la kufuta machozi.

Mbali na sherehe, Okwi pia amekuwa akichelewa kurejea nchini hata siku za kawaida huku uongozi ukishindwa kumchukuliwa hatua za kinidhamu.

Akiwa na Simba hivi karibuni, Okwi aliahidi kucheza soka kwa bidii akiwa na kuachana na tabia zake sizizofaa, lakini inaonekana tabia yake imeota kutu.

 

Maisha yake ya soka

Okwi amecheza mpira wa ushindani kwa miaka mitano tu tangu aliposajiliwa kwa mara ya kwanza na SC Villa akiwa kinda wa miaka 17 na kufunga mabao 16 katika ligi kuu ya Uganda mwaka 2009. 

Alinunuliwa na Simba na akaitumikia kwa muda wa miaka mitatu na nusu akitwaa mataji mawili ya ligi kuu Tanzania Bara, msimu wa 2009/10 na 2011/12 kabla ya kupigwa bei katika klabu ya Etoile du Sahel ya nchini Tunisia.

Mwishoni mwa mwaka 2013, alinyakuliwa na Yanga ambayo hata hivyo hakufanya vizuri akiwa na timu hiyo, ndipo Simba walipoamua kumrejesha tena kundini kufuatia kutofautiana na uongozi wa Yanga hasa katika malipo yake.

Kwa upande wa timu ya Taifa, Okwi aliitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Uganda ‘The Cranes’ mnamo mwaka 2009.

 

Read more...

Mchezaji bora Fifa duniani kutangazwa

  • Published in Michezo

Tuzo ya mchezaji Bora wa dunia wa Fifa kwa mwaka 2014 inatarajiwa kutangazwa leo ambapo tayari wachezaji watatu wamechujwa ili kuania tuzo hiyo inayojulikana kwa jina la FIFA Ballon d'Or 2014.

 

Lionel Messi na Cristiano Ronaldo

Wachezaji watatu waliobaki kwenye fainali ni pamoja na Christiano Ronaldo ambaye ni mchezaji wa timu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno.

Mwingine ni Lionel Messi mshambuliaji wa Barcelona na mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina.

Na wa tatu ni Manuel Neuer Mlinda mlango wa Bayern Munich ambaye pia hudakia timu yake ya taifa ya Ujerumani.

Read more...

Jinsi mfumo wa ‘Mti wa Krismasi’ ulivyoleta mafanikio kwenye Soka

  • Published in Michezo

KATIKA mchezo wa Mpira wa Miguu kuna mifumo mingi sana ambayo makocha huitumia kwa lengo la kupata mafanikio ndani ya uwanja.

Mifumo hiyo haitumiki tu kama fasheni, bali makocha huzingatia aina ya wachezaji iliyonao.

Ipo mifumo mingi kama vile 4-4-2, 4-3-3, 4-5-1, 3-5-2,4-3-2-1 na hata 9-1 ambao ulikuwa ukitumika miaka ya zamani sana.

Katika soka la kileo tunashuhudia makocha wengi wakitumia mifumo kama 4-4-2, 4-3-3, 3-5-2 na mingineyo mingi, na timu zao zimekuwa zikipata mafanikio pia kupitia mifumo hiyo.

Kupitia mifumo hiyo makocha wengi wanaamini kwamba ndiyo yenye mafanikio makubwa zaidi ikilinganishwa na ile ya miaka ya zamani.

Ikumbukwe kuwa katika miaka ya 1800, mchezo wa soka ulianza kwa kutumia mifumo ambayo leo hii hakuna hata mmoja unaotumika. Mfano mzuri ni Novemba 30 mwaka 1872, timu za taifa za Scotland na Uingereza zilitumia mifumo ya kipekee kabisa.

Uingereza ilitumia mfumo wa 1-1-8 ama unaweza kuuita 1-2-7 wakati Scotland ilitumia mfumo wa 2-2-6.Hadi mechi inamalizika timu zote zilitoka suluhu ya bila kufungana.

 

MFUMO WA ‘CHRISTMAS TREE’

Huu ni mfumo ambao wachezaji hujipanga uwanjani na kutengeneza umbo linalofanana na mti wa Krismasi, ndiyo maana ukaitwa hivyo.

Mfumo huu ni 4-3-2-1 ambao huusisha mabeki wanne, viungo watano na mshambuliaji mmoja. Sifa kuu ya mfumo huu ni kujihami zaidi na mshambuliaji mmoja anapaswa kuwa na nguvu za kupambana na msitu wa mabeki wa timu pinzani.

Mfumo wa mti wa Krismasi unatoa majukumu kwa wachezaji kama ilivyo mingine ambapo katika 4-3-2-1, mabeki wanne kazi yao ni kulinda na mara zote huwa nyuma.

Viungo watatu wanaofuatia, kazi yao ni kuwasaidia mabeki wanne wasipate mashambulizi makali wakati wawili ambao huwa mbele yao, kazi yao ni kumtengenezea mipira mshambuliaji peke(lone striker).

Faida kubwa ya mfumo huo ni kwamba ni mzuri sana kwenye ulinzi na hasara yake kubwa ni kuinyima timu uwezekano wa kupata mabao mengi.

 

MAFANIKIO YAKE KWA MAKOCHA NGULI

Makocha kadhaa nguli walikuwa wakipenda kutumia mfumo huo ambao ni pamoja na Terry Venables, Christian Gross, Carlo Ancelotti, Jose Mourinho na hata Sir Alex Ferguson.

Makocha Terry Venables na Christian Gross waliwahi kuutumia mfumo huo wakati walipokuwa wakifundisha katika klabu ya Tottenham kwa nyakati tofauti. 

Kocha Ancelotti alikuwa akiutumia mfumo huo wakati alipokuwa katika klabu ya AC Milan na Mourinho alikuwa akitumia wakati alipokuwa Chelsea kabla ya kuachana na timu hiyo mwaka 2007.

 

TERRY VENABLES NA CHRISTIAN GROSS

Katika kipindi cha mwaka 1987 hadi 1993, Venables alikuwa akipendelea sana mfumo wa 4-3-2-1.Kwa kutumia mfumo huo aliipatia timu ya Tottenham taji la FA mwaka 1991.

Kabla ya hapo mwaka 1990 Spurs ilimaliza Ligi ya Uingereza katika nafasi ya tatu.Kwa upande wake Gross ambaye alipewa timu ya Spurs mwaka 1997 hadi 1998, aliweza kuinasua kutoka kwenye hatari ya kushuka daraja.

 

CARLO ANCELOTTI

Tangu mwaka 2001 hadi 2009, kocha Carlo Ancelotti alikuwa akiifundisha timu ya AC Milan ya nchini Italia.Aliifundisha timu hiyo akiwa anatumia zaidi mfumo wa mti wa Krismasi wa 4-3-2-1.

Kocha huyo alifanikiwa kuipeleka timu hiyo kwenye michuano ya Ulaya na alianza kwa kuifikisha hatua ya nusu fainali ya Kombe la Ulaya(sasa Klabu Bingwa Barani Ulaya) kwa msimu wa 2001-2002.

Licha ya mfumo wake ulipingwa sana na mmiliki wa klabu hiyo Silvio Berlusconi, Ancelotti aliipatia Milan taji la Klabu Bingwa Ulaya mnamo mwaka 2003 baada ya kuifunga Juventus penati 3-2 kwenye uwanja wa Old Trafford na kisha kushinda taji la Coppa Italia.

Mwaka 2007, Ancelotti aliipatia Milan taji la pili la Klabu Bingwa Brani Ulaya baada ya kuinyuka Liverpool katika dimba la Olympic nchini Ugiriki.Mwaka huohuo kocha huyo aliipatia Milan taji la Klabu Bingwa ya Dunia.

 

JOSE MOURINHO NA SIR FERGUSON

Mourinho alijiunga na Chelsea kwa mara ya kwanza kabiusa mwaka 2004 na kuachana nayo mwaka 2008.Katika kipindi hicho alikuwa akipenda kutumia mfumo wa 4-3-3 na wakati mwingine 4-3-2-1 na kufanikiwa kuipa Chelsea mataji mawili ya Ligi Kuu, matatu ya Kombe la Ligi na moja ya FA.

Sir Alex Ferguson naye wakati akiwa anainoa Manchester United alikuwa akitumia mfumo huo kiujanjaujanja na umemsaidia kwa namna fulani kupata mafanikio makubwa hadi anastaafu.

 

 

 

 

 

Read more...
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.