Menu
RSS

Jinsi nyuki wanavyowasaidia wanamichezo Featured

Jinsi nyuki wanavyowasaidia wanamichezo

MICHEZO ni jambo muhimu kwa afya ya binadamu ambapo kila mmoja anapaswa kushiriki kwa namna moja ama nyingine ili kuuweka mwili na akili yake katika hali nzuri.

Ipo michezo tofauti tofauti ambayo watu hushiriki kadiri ya uwezo wao ilimradi tu kuimarisha afya yao.  

Lakini ndani ya michezo hiyo yapo mambo ama vitu ambayo vinaweza kuchagiza ubora wa kiwango cha mchezaji katika mchezo husika.

Vipo vyakula ambavyo humfanya mchezaji ashiriki vizuri mchezo anaohusika nao, kwa mfano mchezaji hatakiwa kula vyakula vyenye kiwango kikubwa sana cha mafuta kabla ya kucheza mchezo unaotumia nguvu nyingi kama vile soka, kikapu, masumbwi na mingineyo.

Nyuki ni mdudu mbaya sana ambaye hapendwi na binadamu yoyote yule, hata wanyama pia hawampendi hasa kwa tabia zake za kung’ata.

Lakini mdudu huyo anatoa kitu kitamu sana(asali)ambacho watu wengi wanakipenda licha ya kwamba inahitaji ujasiri wa hali ya juu katika kuipata.

Asali ya wadudu hao ina faida nyingi sana katika mwili wa binadamu lakini kupitia kona yangu nitakuletea faida kadhaa kwa wanamichezo na michezo yenyewe.

NGUVU

Asali humpa mchezaji nguvu zaidi kupitia mchezo husika anaoucheza hasa kwa michezo inayohitaji nguvu nyingi kama vile mpira wa kikapu, soka, masumbwi, riadha na mingine mingi.

Kabla ya kufanya mazoezi mchezaji anapaswa kutumia asali kupitia vyakula mbalimbali ikiwemo kupaka kwenye mikate, kuweka kwenye chai ama kulamba mara kwa mara.Zoezi kama hilo pia huweza kufanywa saa chache kabla ya kuingia uwanjani.

Hivyo kama ni mwanariadha hujikuta akipata nguvu za ziada katika kukimbia na kama ni mwanasoka pia hupata nguvu za ziada uwanjani.

TIBA YA JERAHA

Umuhimu wa asali huonekana hasa pale ambapo mchezaji akaumia kwa bahati mbaya kwa kupata mchubuko katika ngozi yake.Majeraha kama hayo hujitokeza mara nyingi katika michezo mbalimbali kama vile soka, kikapu, rugby,baiskeli nk ambapo mchezaji huweza kuanguka na kupata michubuko.

Jinsi ya kufanya ni kwamba mara tu inapotokea mchezaji ameanguka na kupata michubuko katika ngozi yake, kidonda kinapaswa kuoshwa haraka na maji ya uvuguvugu na kisha kupaka asali juu yake.

Kwa kufanya hivyo asali huchukua jukumu la kukausha kidonda baada ya siku chache tu kama ilivyo kwa dawa zingine za vidonda.Kitaalamu inaelezwa kuwa asali ina kiwango fulani cha Antibiotics.

HUDUMISHA MIPIRA YA GOFU

Kama tunavyofahamu kwamba asali ni chakula pekee kisichooza, tofauti navyakula vingine ambavyo ili vidumu lazima vichanganywe na kemikali zingine.

Katika miaka ya zamani kabla ya kuibuka kwa teknolojia za kisasa, viwanda vingi vya kutengeneza mipira ya gofu vilikuwa vinatumia sana asali.

Katika mipira ile ndani yake kulikuwa na kasi fulani cha asali ambacho kazi yake kubwa ilikuwa ni kuhakikisha kwamba mpira wa gofu unadumu kwa muda mrefu zaidi.

HUSAIDIA MABONDIA

Ukiwatazama mabondia wengi utabaini kwamba sura zao hazipo katika muonekano mzuri hasa kutokana na kashikashi za mchezo wenyewe kwasababu ni ngumu sana kuepuka makonde ya usoni.

Kama unavyo fahamu mtu akigongwa na kitu kizito katika ngozi yake, sehemu iliyogongwa hupatwa na alama fulani ambayo wengi hutumia lugha fulani ya ‘kuvilia’.

Kwa kifupi mabondia wengi ngozi zao haziwi katika ulaini kwa kawaida(softy/smooth skin) hivyo dawa pekee ya kulainisha ngozi zao na kuonekana maradufu ni kupaka asali.

Wataalamu wanashauri kwamba watu wa namna hii wanapaswa kupaka asali katika ngozi zao mara kwa mara ili kuzifanya ngozi zao ziwe laini na muonekano mzuri.

HUPUNGUZA UZITO

Wakati mwingine mwili ukiwa na uzito mkubwa humpunguzia mchezaji ufanisi wa mchezo anaohusika nao.

Mchezaji anapaswa kuwa na kiwango cha kawaida kabisa cha uzito wa mwili wake kulingana na urefu alionao, na hiyo itamfanya awe mtu ambaye anafanikiwa kila anachokitaka ndani ya uwanja kwasababu anajiona mwepesi.

Mchezo unaweza kupunguza uzito wa mchezaji lakini kama ikishindikana asali inaweza kuchukua nafasi yake ambapo muhusika anapaswa kuitumia mara kwa mara kwa kuchanganya kwenye maji ya uvuguvugu na kunywa kila anapoamka.

Hiyo huambatana na kusaidia kuondoa sumu mwilini na hata kupunguza kitambi endapo kama mtu atakuwa nacho.

HULAINISHA MISULI

Kuna wakati huwa tunashuhudia wachezaji wakigalagala uwanjani huku wakiugulia maumivu makali bila ya kuchezewa rafu na mtu yoyote.

Hiyo hutokea mara baada ya misuli kukaza ghafla, hutokea hasa miguuni kwenye nyama za paja ama juu ya ‘ankle’.

Asali ni moja ya dawa za kutibu hali hiyo ambapo kama ipo karibu, mtoa huduma anaweza kuichukua na kupaka kwenye sehemu ambayo msuli umekaza.

Kwa kifupi hizo ndiyo faida za asali kwa wanamichezo ambao wanashiriki michezo mbalimbali.

mpanduka@yahoo,com

xxxxxx

 

 

 

 

 

 

Last modified onWednesday, 25 March 2015 16:24
back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.