Menu
RSS

Matukio ya soka yaliyotikisa ndani ya miezi kumi Ulaya

YAPO matukio mengi makubwa ya michezo yaliyotokea ndani ya miezi kumi tu tangu kuanza kwa mwaka huu.

Hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu tayari zaidi ya matukio 9 makubwa ya mchezo wa soka yametokea na ni matarajio kwamba hadi mwaka huu unamalizika tutauwa tumesikia na kuyashuhudia mengine mengi zaidi.

Fuatilia makala haya kuweza kujua yale tuliyoshuhudia kuanzia mwezi Januari hadi Oktoba.

BALLON D’OR

Tuzo ya mchezaji bora wa Dunia maarufu kama Ballon d’Or kwa mwaka 2016 ni moja kati ya matukio yaliyoukaribisha mwaka huu.

Tuzo hiyo ilitolewa Januari 11 pale Zurich Uswiss na wachezaji waliokuwa wanawania tuzo hiyo ni Messi, Ronaldo na Neymar ambapo hatimaye Ronaldo akatwaa tuzo hiyo.

TEKNOLOJIA YA GOLI NDANI YA UEFA

‘Goal Line Technology’, hii ni teknolojia mpya katika soka ambayo ilianza kutumika mwezi Agosti mwaka 2016, baada ya Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kukubali na kuanza kuitumia katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Goal line technology ni teknolojia mpya ambayo humsaidia mwamuzi kufanya maamuzi sahihi kuhusu mpira kama umeingia golini ama la.

COPA AMERICA KUFIKISHA MIAKA 100, MESSI AJIUZULU

Mashindano ya Copa America yamefikisha miaka mia moja toka kuanzishwa kwake.

Michuano hiyo ilifanyika U.S.A kwa kushirikisha nchi 10 kutoka ukanda wa Conmebol na timu sita kutoka Concacaf ambapo Chile ilitwaa taji hilo baada ya kuichapa Argentina na kumfanya Lionel Messi atangaze kujiuzulu kuchezea timu ya taifa.

BURUDANI ZA EURO 2016

Kuanzia Juni hadi Julai mwaka huu mashindano ya soka ya Mataifa ya Ulaya (EURO 2016) yalianza kutimua vumbi barani Ulaya.

Hiyo ilikuwa ni michuano ya 15 kufanyika na kujumuisha jumla ya timu 24.

Miongoni mwa timu kubwa zilizoshiriki ni Ujerumani, Hispania, Ureno, Ubelgiji, Uingereza, Italia na mwenyeji Ufaransa.

Hatimaye Ureno ambayo ilionekana kama timu chovu tangu mwanzo wa michuano hiyo, ndiyo iliyotwaa taji hilo.

MOURINHO AENDA MANCHESTER UNITED

Hatimaye kocha Jose Mourinho alijiunga na Manchester United baada ya Disemba mwaka jana kutimuliwa na Chelsea kufuatia timu hiyo kuwa na mwenendo mbovu kuwahi kutokea.

Hakuna aliyedhani kama kocha huyo angejiunga na United, lakini hatimaye yakatimia na Mourinho akaanza maisha mapya Old Trafford.

CHELSEA YAPATA KOCHA

Baada ya kufukuzwa kwa Jose Mourinho katika klabu ya Chelsea na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa muda Guus Hiddink, wengi walikuwa na hamu ya kutaka kufahamu nani angekuwa kocha wa kudumu wa timu hiyo.

Makocha Antonio Conte na Diego Simeone walikuwa wanahusishwa kuwa katika mipango ya kuchukuliwa na Chelsea. Jibu la suala hilo lilipatikana baada ya kumalizika kwa msimu wa 2015/16 baada ya Antonie Conte kukabidhiwa mikoba ya timu hiyo.

GUARDIOLA ATUA MAN CITY

Habari nyingi katika mitandao ya soka barani Ulaya mwaka jana ziliwahi kumuandika kocha Pep Guardiola kuwa angejiunga na Manchester City mwezi Mei na kurithi nafasi ya Manuel Pellegrini baada ya msimu kumalizika.

Tetesi hizo hatimaye zilikuwa kweli ambapo kabla ya mwezi Mei mwaka huu, Guardiola alisaini mkataba wa kufundisha timu hiyo miaka mitatu.

MAAJABU YA UBINGWA WA EPL

Mwezi Mei mwaka huu tulishuhudia klabu ndogo ya Leicester City ikitwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza kwa msimu wa 2015/2016.

Leicester City ilitabiriwa ubingwa tangu Disemba mwaka jana, kwasababu siku zote Waingereza kuamini kwamba timu inayokuwa kileleni katika siku ya Disemba 25 ambayo ni sikukuu ya Ksismasi, ndiyo inakuwa bingwa mwishoni mwa msimu.

Kwea kutwaa taji hilo, Leicester iliwalaza vigogo Manchester City, Arsenal, Manchester United, Liverpool na Tottenham.

RAIS MPYA WA FIFA APATIKANA

Baada ya utawala wa miaka 18 wa Sepp Blatter katika nafasi ya Urais wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA, mwezi Februari mwaka huu FIFA ilifanya uchaguzi wake na kumpata mrithi Blatter katika nafasi hiyo.

Gian Infantino ndiye aliyeibuka kuwa rais mpya wa FIFA akikalia kiti kilichoachwa na Blatter.

Blatter alitangaza kujiuzulu mwaka jana kabla ya Kamati ya Maadili ya FIFA kumfungia kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miaka nane baada ya kubainika kufanya ubadhilifu wa fedha kwa kipindi chote alicholiongoza Shirikisho hilo.

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

 

 

 

 

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.