Menu
RSS

Viwanja 10 vinavyoongoza kwa ubora Afrika

Viwanja 10 vinavyoongoza kwa ubora Afrika

 

AFRIKA ina viwanja vingi vya mpira wa miguu katika nchi mbalimbali isipokuwa vimezidiana thamani, ukubwa na ubora.

Vipo viwanja ambavyo vimejengwa kwa lengo pekee la kuhakikisha soka linachezwa na vingine vimeanzishwa kuhakikisha si soka linachezwa tu, bali uvutie watu wanaoingia kuutazama mchezo husika.

Vifuatavyo ni viwanja kumi vyenye ubora barani Afrika ambavyo vimejengwa kwa kiasi kikubwa cha pesa na kukidhi haja ya michuano mikubwa ya kimataifa hasa mpira wa miguu.

 

10 UWANJA WA TAIFA, TANZANIA

 

Uwanja wa Taifa ulijengwa kwa gharama ya dola milioni 53 ambapo nusu ya hela za ujenzi huo zilitolewa na Serikali ya China. Uwanja ulifunguliwa mwaka 2007 na una uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000.

Kulingana na ubora wake, mwaka 2010 timu ya taifa ya Brazil ilishawishika kuja nchini kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars ambapo wenyeji walifungwa mabao 5-1.

 

9 STADE OLYMPIQUE DE RADES, TUNISIA

 

Stade Olympique de Radès ni uwanja uliopo nchini Tunisia katika mji wa Rades, uwezo wake wa kuchukua mashabiki ni sawa na uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ila gharama yake inatajwa kufikia dola milioni 110. Ulijengwa mwaka 2001.

 

8 MBOMBELA STADIUM, A. KUSINI

 

Ni moja kati ya viwanja vilivyotumika katika fainali za michuano ya Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika ya Kusini. Una thamani ya dola milioni 140 na una uwezo wa kuchukua mashabiki 40,929.

 

7 PETER MOKABA STADIUM, A. KUSINI

 

Ni uwanja ambao ulijengwa kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini.Ulijengwa kwa dola milioni 150 na una uwezo wa kuchukua mashabiki 41,733, kwa sasa unatumiwa na klabu ya Black Leopards FC kama uwanja wa nyumbani.

 

6 ESTADIO 11 DE NOVEMBRO, ANGOLA

 

Estádio 11 de Novembro upo Angola lakini ulitumika kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2010.Umejengwa kwa dola milioni 227 na una uwezo wa kuchukua mashabiki 50,000.

 

5 NELSON MANDELA BAY, A. KUSINI

 

Huu ni uwanja ambao ulijengwa kwa dola milioni 270.Upo katika mji wa Port Elizabeth na una uwezo wa kubeba mashabiki 48,459. Jina lake limetokana na Rais wa kwanza wa Afrika Kusini hayati Nelson Mandela.

 

4 ABUJA STADIUM, NIGERIA

 

Hiki ni moja kati ya viwanja vilivyojengwa kwa gharama zaidi barani Afrika.Dola milioni 360 ndio zilitumika kujenga uwanja huu wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,491.Upo  kwenye mji mkuu wa Nigeria Abuja.

 

3 FNB STADIUM, AFRIKA KUSINI

 

Ni uwanja ambao ulijengwa kwa dola milioni 440 na kutumika katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.

Jina lake lilizoeleka na wengi ni Soccer City. Huu ndio uwanja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki wengi zaidi barani Afrika, una uwezo wa kubeba watu 94,736.

 

2 MOSES MABHIDA STADIUM

 

Moses Mabhida ulijengwa kwa dola milioni 450.Uwanja huu upo Durban Afrika Kusini na ulitumika kwa baadhi ya mechi za fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010.

Ulikuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 62,760 lakini wakati wa fainali za Kombe la Dunia ulipunguzwa na kuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 54,000.

 

1 CAPE TOWN STADIUM

 

Cape Town Stadium ndio uwanja wenye thamani kuliko vyote barani Afrika, kwani zimetumika dola milioni 600 katika ujenzi na una uwezo wa kuingiza mashabiki 64,100.

 

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

 

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.