Menu
RSS

Baba Samatta; “Mwanangu Mungu atakuona”

Baba Samatta; “Mwanangu Mungu atakuona”

 

Na Arone Mpanduka

 

BABA mzazi wa mshambuliaji wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars na klabu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta, amesema atajitahidi kuongeza maombi ili mwanae afanikiwe kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka huu.

Baba huyo mzee Ali Samatta aliyasema hayo hivi karibuni baada ya mwanae kuingia katika orodha ya mchujo ya wachezaji wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika.

Akizungumza na Tumaini Letu hivi karibuni, mzee Samatta alisema amefurahishwa na taarifa hizo na kwamba kilichobaki sasa ni kitu kimoja muhimu ambacho ni kuzidisha maombi kwa ajili ya mafanikio ya mwanae.

“Nimefurahishwa sana na taarifa hizo, ama kweli Mungu mkubwa.Namuomba aendelee kumjaalia katika safari yake ya kuwania tuzo na nina imani Mungu atamsaidia na kufanikiwa kutwaa tuzo hiyo”

“Siku zote unapoonyesha juhudi katika kazi yako unatoa fursa ya wengi kuiona, kwa hiyo hata Mbwana juhudi zake zimemsaidia na wengi wameuona uwezo wake na kumjumuisha kwenye tuzo,”alisema mzee Ali Samatta.

Alisema mafanikio mengi aliyopata mwanae yametokana na maombi yake ya mara kwa mara.

“Mara nyingi katika maombi yangu huwa ninamkumbuka sana mwanangu na kumuombea mafanikio mema katika kazi yake.Hata yeye pia huwa ana swali sana huko aliko na anamuogopa sana Mungu, ndiyomaana anafanikiwa”

Mwezi Januari mwaka huu, Samatta alitwaa tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani ya Bara hilo.

Mchezaji huyo alizaliwa Januari 7 mwaka 1992 katika mkoa wa Dar es salam.

Katika maisha yake ya soka alianza kucheza mpira katika klabu ya Kimbangulile FC na kisha African Lyon kwa muda wa miaka miwili kutoka 2008 hadi 2010 na kuhamia katika klabu ya Simba.

Mwaka 2011 alijiunga na klabu ya TP Mazembe ya Congo DR na aliweza kuifungia jumla ya  magoli 60.

Januari mwaka huu alijiunga na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji na sasa ameanza kuaminika kwani mechi kadhaa za Ligi Kuu amekuwa akifunga magoli.

Hadi sasa Samatta anajulikana sana katika mji wa Lubumbashi kwa kuwa alifunga magoli nane katika mashindano ya Ligi ya mabingwa Africa na kuiwezesha Mazembe kutwaa kombe hilo.

Licha ya kucheza soka nchini Ubelgiji, Samatta bado ana ndoto za kusonga mbele zaidi ambapo anatamani kucheza Ligi Kuu soka nchini England ama Ligi ya Ufaransa.

Mara nyingi amekuwa akisikika akisema kwamba Ligi za nchi hiyo zinamtangaza haraka mchezaji katika soko la dunia ikilinganishwa na zingine.

 

Xxxxxxx

 

 

 

 

 

 

 

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.