Menu
RSS

Tamasha Jubilei Huruma ya Mungu kunguruma Dar

 

Na Timothy Kahoho

 

TAMASHA kabambe la Jubilei ya pekee ya Huruma ya Muungu imepangwa kufanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu ya Mtakatifu Joseph Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Dominika ya Oktoba 30, mwaka mwaka huu.

Paroko wa Kanisa Kuu ya Mtakatifu Joseph, Padri Dk. Joseph Matumani alisema hayo wakati akizungumza na gazeti hili, kufuatia maandalizi ya tamasha hilo kufikia asilimia 95 kwa kushirikisha vyama na vikundi vya Kitume mbalimbali na pia kwaya kadhaa pamoja na Kwaya za Kanisa Kuu la Anglikana la Mtakatifu Albano na Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

“Tarehe 30/10/2016 yatafanyika maonyesho ya vyama na vikundi vya kitume kuanzia saa 1 hadi saa 7 mchana eneo la Kanisa la Mtakatifu Joseph. Vyama na vikundi hivyo vitatoka Kila parokia za Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Dar es Salaam. Kwani kufanyika kwa maonyesho hayo ni kudhihisha uhai wa parokia husika kutokana na ushiriki wa viongozi na wanachama wa vyama na vikundi vyenyewe,” alisema Padri Matumaini.

Paroko huyo alidokeza kuwa kila chama na kikundi kitapewa eneo kwa ajili ya kuonyesha shughuli zake ikiwa ni pamoja na mavazi yao katika kuwavutia waamini kujiunga na vyama au vikundi hivyo. Alitolea mfano wa chama cha Kitume cha Moyo Mtakatifu wa Yesu kuwa wataonyesha sala zao na kuwaorodhesha kama wanachama wapya kutokana na kuvutiwa na sala zao.

Padri Matumaini alitaja vyama na vikundi vitavyofanya maonyesho hayo kuwa ni Rejio Maria, Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA), Umoja wa Wanaume Wakatoliki (UWAKA), Karismati, Katoliki, Kwaya ya Mtakatifu Joseph, na pia Kwaya za Walutheri na Anglikana.

“Siku hiyo kuanzia saa 7 hadi saa 12 jioni kutakuwepo na tamasha la kwaya mbalimbali. Kusema kweli, kuimba ni kumtukuza Mwenyezi Mungu na hivyo ni tendo la kusali, kujumuika pamoja na kusherehekea kimaisha,” alisema.

Aidha Padri Matumaini alitaja kwaya zitazotumbuiza kwenye tamasha hilo kuwa ni Familia Takatifu, Kwaya ya Mtakatifu Joseph, Kwaya ya Watoto, Kwaya mbili katika Lugha ya Kiingereza, na pia kwaya za kutoka Azania na Albano.

Kuhusu maudhui ya tamasha lote, Padri Matumaini alisema kuwa hiyo ni Jubilei ya Pekee ya Huruma ya Mungu, ambapo wakristo husali na kukaa pamoja katika kutafakari Neno la Mungu.

“Wito wangu kwa wote ni shime kwa waamini kujumuika na wote wenye mapenzi mema kushiriki  kutokana na kuguswa na Huruma ya Mungu,” alisema.MWISHO

 

 

 

 

 

End

 

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.