Menu
RSS

Hawa ndiyo mabingwa wa NBA ‘waliomzuia’ Obama kushuka kwenye ndege

Hawa ndiyo mabingwa wa NBA ‘waliomzuia’ Obama kushuka kwenye ndege

UKIPENDA unaweza kuwaita Cavs ambao kwa kirefu wanaitwa Cleveland Cavaliers.Hawa ni mabingwa wapya wa Ligi ya NBA kwa mwaka huu.

Wamepata ubingwa huo kwa mara ya kwanza kabisa tangu timu ilipoanzishwa mwaka 1970.

Ilikuwa ni alfajiri ya Jumatatu ya Juni 20 mwaka huu ambapo walifanikiwa kuwanyuka Golden State Warriors katika mechi ya saba ya fainali za NBA.

Utamu wa mchezo huo ulimlazimu Rais wa Marekani Barack Obama ashindwe kushuka kwenye ndege yake ya Air Force One hadi mchezo ulipomazilika.Obama alikuwa akitoka safarini na familia yake lakini aliona kuteremka kwenye ndege ni kama kukosa uhondo wa Cavaliers.

JINSI ILIVYOANZA LIGI YA NBA

Cavaliers kwanza kabisa walianza kushiriki Ligi ya NBA mwaka 1970 chini ya umiliki wa Nick Mileti.

Baadae, Jerry Tomko ambaye ni baba  wa aliyekuwa mchezaji wa Baseball Brett Tomko akaipa timu hiyo jina rasmi la Cavaliers kufuatia hapo kabla kuitwa majina tofauti likiwemo Jays, Foresters na Presidents.

Cavaliers walikuwa wanatumia uwanja wa Cleveland Arena chini ya kocha Bill Fitch na wakapata mwanzo mbaya wa ligi kwa rekodi ya 15-67 katika msimu wao wa kwanza.

Mnamo mwaka 1994 timu hiyo ilianza kucheza mechi zake za nyumbani katika uwanja wa Quicken Loans ambao waliutumia pamoja na timu ya Cleveland Gladiators iliyokuwa ikishiriki Ligi ya American Football na Lake Erie Monsters iliyokuwa ikishiriki Ligi ya Hockey.

WAMILIKI WALIOPITA

Wadhamini kadhaa wamepita katika timu hiyo ambapo kuanzia mwaka 1970 hadi 1980 kampuni ya Austin Carr ilijitokeza kudhamini timu hiyo na kusaidia kuleta auheni.

Katika kipindi hicho ilijikuta ikizidi kuongeza wachezaji wenye vipaji kama vile Bobby "Bingo" Smith, Jim Chones, Jim Cleamons na Dick Snyder.

Cavaliers ilijitahidi na kumaliza msimu kwa rekodi ya 23–59 in their na kufuatiwa na ya 32–50 katika msimu wa 1972–73, na ya 29–53 katika msimu wa 1973–74.

Cleveland won 43 games in both of the 1976–77 and 1977–78 seasons, but both seasons resulted in early playoff exits. After a 30–52 season in 1978–79, Fitch resigned as head coach.

Cleveland ikashinda jumla ya michezo 43 katika misimu ya 1976/77 na 1977/78 lakini ulipofika msimu wa 1978/79 Fitch alijiuzulu ukocha.

Kuanzia mwaka 1980–83Ted Stepien akaitwaa timu hiyo baada ya Austin Carr kuachana nayo.

Mileti aliuza hisa zake kwa Louis Mitchell ambaye nae aliuza kwa Joe Zingale na baada ya hapo Zingale aliuza kwa Ted Stepien.

Kuanziamwaka 1983 hadi 1986 familia ya Gunds nayo ikaingia na kuweka hisa zake.Gunds walifanya mabadiliko kadhaa ikiwemo kubadili rangi za jezi kutoka ya mchanganyiko wa mvinyo na dhababu hadi mchanganyiko wa machungwa mbivu na bluu bahari.

Gunds pia waliibua jina la ziada la ‘Cavs’ambalo linatumika hadi sasa kama kifupi cha Cavaliers.Kifupi hicho kimelazimika kutumika kwa sababu za kibiashara.

Mbali na Gunds wapo wengine wengi waliopita kwa nyakati tofauti wakiwemo The Daugherty, Nance na Price

UJIO WA LEBRON JAMES

Cavaliers iliboronga kwa misimu mingi mfululizo na kuifanya msimu wa mwaka 2002/03 ifanye vibaya sana.

Wakati huo ndipo wazo la kumchukua LeBron James lilipowajia ambapo walimchukua kutoka shule ya Sekondari.

Kipindi hichohicho jezi zikabadilishwa tena kutoka rangi ya machungwa, nyeusi na bluu na kisha kurejea tena kwenye rangi ya mvinyo na dhahabu.

James alikuwa akisoma na kucheza mpira wa kikapu katika shule ya St Marry iliyo karibu na Akron.

James ambaye alipewa jina la King James, alianza kung’ara katika msimu wa 2003/04 na kutoa matumaini makubwa ya kufanya vizuri hapo baadae kwa timu hiyo kwani alianza kuwa mchezaji tegemeo.

Msimu huohuo alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa NBA.

Msimu wa 2004/05, uwezo wa James ukazidi kuzaa matunda hasa katika nyanja za pointi, ribaundi na pasi za magoli kwa kila mchezo.

Licha ya kuondoka kwaCarlos Boozer mwishoni mwa msimu huo, James alishirikiana kwa karibu na nguli Žydrūnas Ilgauskas na Drew Gooden ili kupata kikosi imara.

Kwa ujumla tangu mwaka 2003 hadi 2010, James alifanikiwa kutwaa tuzo ya Rookie of the Year(2004), Tuzo ya MVP, yaani mchezaji bora wa Ligi mara mbili(2009 na 2010) pia aliipeleka Cavaliers katika fainali za NBA kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 2007.

Kadhalika amekuwa mfungaji bora wa mara zote ndani ya timu ya Cleveland Cavaliers.

Julai 8,2010 James alitangaza rasmi kuachana na Cavs na kutimkia katika timu ya Miami Heats, jambo ambalo liliwaudhi mashabiki wa Cavs waliohisi kama wamesalitiwa na kufikia maamuzi ya kuchoma moto jezi zake.

CAVALIERS WAHAHA

Baada ya James kuondoka zake mwishoni mwa mwaka 2010, Cavs wakaanza kuhaha huko na kule kusaka wachezaji mbadala kwa lengo la kuimarisha kikosi.

Cavs walitumia kipindi cha mapumziko mwaka 2010 kukisuka kikosi chao ambapo walimsaini Christian Eyenga, Ramon Sessions na Ryan Hollins kutoka katika timu ya Minnesota Timberwolves na kuwatema Delonte West na Sebastian Telfair.

Pia walimsaini Joey Graham na kuwatema Samardo Samuels na Manny Harris. Walifanya zoezi hilo hadi Februarimwaka 2011

Hata hivyo misimu iliyofuata kuanzia 2010/11,Cavs hawakufanya vizuri sana ambapo msimu wa 2012-13 walilazimika kumtimua kocha Byron Scott baada ya rekodi mbovu ya 64–166 ya misimu mitatu ya jumla.

MWAKA 2014 LEBRON AREJEA KUNDINI

Juni 20 mwaka 2014 Cavaliers wakamsajili kocha wa muda mrefu David Blatt na siku tatu baadae wakamsainisha kocha mwingine Tyronn Lue kama kocha msaidizi.Lue akawa kocha msaidizi wa NBA anayelipwa pesa nyingi zaidi.Ikumbukwe kwamba hivi sasa Lue ni kocha mkuu wa timu hiyo aliyeipa taji la kwanza kabisa la NBA  kwa mwaka 2016.

Julai 15 makocha hao walimsainisha James ambaye alirejea tena na kuendeleza rekodi zake za kufunga pointi nyingi na hatimaye kuifikisha Cavs kwenye fainali za NBA kwa mara ya pili tangu afanye hivyo 2007 na kuipatia taji la kwanza kabisa la NBA kwa mwaka huu wa 2016.

Pia kwa msimu wa 2015/16 James ametwaa tena tuzo ya MVP na kufanya iwe ya tatu katika klabu hiyo ukijumlisha na zile za 2009 na 2010.

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.