Menu
RSS

JINSI GANI UWANJA WA TENNIS UTATENGENEZWA

JINSI GANI UWANJA WA TENNIS UTATENGENEZWA

 

Sara Fray ni Mkurugenzi wa huduma za Uhandisi na Ufundi kutoka katika taasisi inayojishunghulisha na masuala hayo jijini London,  anasema kwamba ujenzi wa majengo chini ya bahari daima utabaki kuwa na ugumu.

Alisema uwanja wa tenisi utakuwa ni kitu kikubwa mno kukitengeneza na kisha kukizamisha chini ya bahari.

“Unazungumzia uwekezaji wa hali ya juu hata kama utaujenga nchi kavu na kuuzamisha baharini.Huu ni ujenzi wenye gharama mno,”alisema.

Alisema kuna vigezo vingi vya kuangalia wakati wa ujenzi huo ikiwemo kuhakikisha kwamba kiwanja kinajengwa chini zaidi kutoka usawa wa bahari ili kuepuka muingiliano wa vyombo vya usafiri kama vile boti na meli.

Alisema ndani ya bahari kuna vitu vingi kinzani kwa sababu hata boti haziruhusiwi kushusha hovyo nanga zake hata kama kuna dharula imetokea.

“Pia haitakiwi boti nzito kuweka nanga juu ya dali la kioo la uwanja, vinginevyo kiwanja kizamishwe chini ya maji ya bahari yenye ujazo mdogo,”alisema mhandisi huyo.

Alisema kuna njia mbili za ujenzi ikiwemo ya kujenga uwanja nchi kavu na kisha kuuzamisha baharini, ama kutumia kifaa maalumu cha kuyapa msukumo maji kuondoka eneo husika na kisha kujenga uwanja chini ya lile eneo.

“Ninafikiri projekti hii ya chini ya bahari ni ghali sana.Lakini kuna msemo kwamba kila kitu kinawezekana ikiwa una pesa za kutosha,”alihitimisha Fray.

Uwanja huo ukikamilika utaweka rekodi ya kuwa uwanja wa kipekee wa michezo duniani kujengwa chini ya bahari.

VIWANJA VINAVYOTAMBA SASA

Kwa sasa vipo viwanja vya tenisi vya nchi kavu vingi vinavyotesa kwa ubora duniani lakini kwa viwango tofauti tofauti.

ARTHUR ASHE

Uwanja huu umejengwa kwa heshima ya mchezaji mkongwe wa Kimarekani na kutambulika kama moja kati ya viwanja vikubwa kabisa vya tenisi duniani.

 

Uwanja huu upo pale New York City nchini Marekani na unaingiza jumla ya watazamaji 23,000.Ulijengwa kwa gharama ya dola milioni 250.

 

Uwanja huo umeibuka baada ya maboresho ya uwanja wa Louis Armstrong ambao ulitumika kwa mashindano ya wazi ya US mwaka 1997.

 

COURT PHILIPPE

Ni uwanja mkongwe ambao umetengenezwa kwa heshima ya mkuu wa Shirikisho la Tenisi ya Ufaransa.

 

Uwanja huo upo nchini Ufaransa na ulijengwa mwaka 1928 na tangu wakati huo umekuwa ukitumika katika mashindano ya French Open.

 

Unaingiza watazamaji wapatao 15,000 na unabaki kuwa uwanja mkongwe wa tenisi duniani.Rafael Nadal anaukumbuka uwanja huu kwa sababu alishinda taji la French Open mara nane.

 

INDIAN WELLS TENNIS GARDEN

Uwanja unapatikana Califonia nchini Marekani. Ni uwa nja unaotumika kwa fainali za Indian Wells Masters ambayo kwa sasa inafahamika kama BNP Paribas Open.

Unaingiza jumla ya watazamaji 16,100 na umejengwa kwa gharama ya dola milioni 77.

Imeandaliwa na Arone Mpanduka. This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.