Menu
RSS

HAYA NDIO MAMBO YA SOKO

HAYA NDIO MAMBO YA SOKO

Unajua kwamba mchezaji anapopiga mpira nao unampiga?

MICHEZO yoyote ambayo inachezwa na kushindaniwa na binadamu huwa inahitaji vipaji kutoka kwa wachezaji.

Vipaji ambavyo vinatumiwa na wachezaji husika huweza kutofautiana na hapo ndipo watazamaji na mashabiki tunapoweza kuwatofautisha kwa kuwaweka katika madaraja tofauti tofauti.

Hata hivyo katika michezo si vipaji pekee ambavyo hutumiwa na mchezaji ili kupata mafanikio uwanjani bali pia mbinu za kisayansi kuweza kutumika katika kupata mafanikio husika.

Yafuatayo ni matukio mbalimbali yanayotokea michezoni pamoja na uhusiano wake wa kisayansi na tafiti zingine.

MPIRA KUPIGWA JUU NA KURUDI CHINI

Tafiti za kisayansi zinasema kuwa mwanasoka anapopiga mpira angani, mpira ule hukumbana na msuguano mkali kadiri unavyozidi kuambaa.

Msuguano huo ambao hauonekani kirahisi husababishwa na hewa ya anga ambayo kisayansi inatambulika kama maada(maada ni kitu chochote chenye uzito na kinachochukua nafasi).

Kadiri mpira unavyozidi kusafiri angani ndipo unavyozidi kuathiriwa na msuguano wa hewa(frictional force), na hapo ndipo utauona taratibu unaanza kupungua mwendo na kurudi tena chini.

Unapokuwa unarudi chini, mpira huo huanza kuathiriwa na nguvu ya mvutano kutoka ardhini ambayo kitaalamu inaitwa Gravitational Force.

Wakati mpira unapotua ardhini huenda katika tendo linguine la kisayansi lijulikanalo kama ineshia(inertia), Ineshia ni hali ya kitu chenye uzito kutaka kuendelea na mwendo kasi ama kutaka kubaki katika hali yake ya utulivu.

Mpira wa kuchezea nao upo katika hali hiyo ambapo mtu anapoupiga utasogea na mtu asipoupiga utabaki katika utulivu wake.Kwa maana nyingine tunasema kwamba hiyo ipo ndani ya sharia ya kwanza ya mwanasayansi Isaac Newton.

MCHEZAJI ANAPIGA MPIRA BILA KUJUA UNAMPIGA

Leo hii tumekuwa tukiona wanasoka kadhaa wakisifika kwa kupiga mashuti golini na hata kuwatesa magolikipa.

Wapo wachezaji wanaopiga mipira na kufunga magoli mazuri na si kufunga tu bali hata kushuhudia mipira ikichana nyavu.

Kisayansi tunaambiwa kwamba mchezaji yoyote anayepiga mpira, mpira huohuo ndiyo unaompiga bila kujijua.

Dhana hiyo imechukuliwa kutoka katika sheria ya tatu ya mwanasayansi Isaac Newton(Law of action and reaction).

Sheria hii inaeleza kwamba nguvu unayoweka kwenye kufanya kitendo ndio nguvu hiyo hiyo unayoipata kutoka kwenye kitendo hicho. Yaani kama unasukuma ukuta na ukuta nao unakusukuma kwa nguvu sawa na unayoiweka.

Hivyo hata kwenye mpira, mchezaji anapojikamua na kupiga shuti kali, ule mpira anaopiga nao unaupiga mguu wake bila yeye na watu wengine kugundua.

Katika kudhihirisha ukweli wa hilo ni kwamba kwanini unapopiga shuti kwa kutumia mguu ulio peku, baada ya muda unahisi mguu una maumivu?

KWANINI MBIO ZA MAGARI KWENYE NJIA ZA VUMBI?

Kama ni mfuatiliaji sana wa michezo utagundua kwamba mara nyingi mashindano ya mbio za magari hufanyika kwenye barabara za vumbi badala ya lami.

Hata nchi za Ulaya nako huwa wanatafuta barabara za vumbi na kufanya mashindano hayo.

Kwa mujibu wa tafiti za kisayansi, gari huwa na mwendokasi mkubwa zaidi kwenye barabara ya vumbi ikilinganishwa na barabara ya lami.

Hiyo ni kwa sababu kiwango cha msuguano kati ya gurudumu la gari na ardhi tupu huwa ni kikubwa sana(msuguano mkubwa ndiyo unaochochea mwendokasi na ndiyo maana gurudumu za gari huchakaa)

Kwenye barabara ya lami ni tofauti kidogo kwa sababu kiwango cha msuguano kati ya gurudumu na lami ni kidogo sana(msuguano mdogo unafanya mwendokasi kuwa hafifu pia).

KUOGELEA NA NYWELE NDEFU

Utafiti wa kisayansi unaeleza kwamba katika mchezo wa kuogelea, mchezaji mwenye nywele ndefu ana uwezekano mdogo wa kupata ushindi katika mchezo huo.

Hiyo ni kwa sababu nywele ndefu zinapopambana na maji huzalisha kiwango kikubwa cha msuguano kinachopunguza kasi ya kuogeleaji.

Hivyo endapo muogelaji atakuwa na kawaida ya kunyoa nywele basi atafanya kiwango cha msuguano kuwa kidogo zaidi na kumpa kasi kubwa ya kuogelea.

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Last modified onWednesday, 29 April 2015 13:00
back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.