Menu
RSS

WAAMINI WAASWA KUTOFURAHIA SHIDA ZA WENGINE

DAR ES SALAAM

Waamini Nchini wametakiwa kuwa na moyo wa huruma na kuacha tabia ya kufurahia mateso na shida ambazo watu wengine wanayapata katika maisha yao.

Wito huo umetolewa na Katibu wa  Utume wa Karsmatiki Katoliki Jimbo la Dar es salaam, ELIUTER MANGE ,katika kipindi cha roho Mtakatifu Kinachorushwa na redio Tumaini.

Amesema kuwa katika safari ya maisha ya kiroho kuna magumu ,wanadamu wanateseka kwa ajili ya imani na mambo mengine yanayowazunguka katika jamii hivyo sio vema kufurahia mateso ambayo wengine wanayapata.

MANGE amesema katika kipindi cha mfungo wa kwa  resma  ni vema kujipatanisha na wengine na kuwaonea huruma kwa kuwasaidia wale walio katika mateso na taabu kwa kuwa kila mmoja hapa duniani ana sehemu ya mahangaiko atakayopitia.

Aidha amewataka waamini kutokuwa na hofu wala mashaka wanapowasaidia wengine kwani kupitia matendo mema wanayofanya wanamtangaza Kristo.

MANGE amewataka waamini kufanya toba kwa kipindi hiki pamoja n a kuzitumia vyema karama mbalimbali walizojaliwa na mwenyezi kwa jamii pasipo kujisifia na kujiona wao ni bora zaidi kuliko wengine bali wanapaswa kutambua kuwa wamekuwa hivyo kwa neema ya Mungu na wala si kwa mapenzi yao.

NA Joyce Sudi.

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.