Menu
RSS

SIKU YA MAFUNGO YA KWARESMA WAWATA 16/03/2019 KRISTO MFALME TABATA.DSM TANZANIA

 

DAR ES SALAAM.  uongozi wa wanawake wakatoliki jimbo kuu la Dar es salaam, (wawata) unawakaribisha akina mama wote kushiriki siku ya mafungo ya kwaresma yatakayofanyika tarehe 16/03/2019  katika parokia ya kristo mfalme tabata, Nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi huo katika kituo cha Tumaini Media ,mafungo hayo yataanza saa mbili asubuhi  kwa mafundisho na mada mbalimbali zitatolewa na paroko wa parokia ya maramba mawili, padri  AURELIUS MWINUKA.

Uongozi huo umebainisha kuwa,mafungo hayo yataambatana na zoezi la matendo ya huruma kidekania, kwa wahitaji wa kituo cha mama theresa wa karikuta mburahati,na kituo cha watoto yatima msimbazi center.

Waamini na watu wenye mapenzi mema wametakiwa kuwahi ili wajiweke chini ya  yesu kristo katika kuchota  neema za mungu  hasa katika kipindi hiki cha kwaresma ili kujinyenyekeza na kutafakari maisha ya  kiroho .

Ujumbe wa kwaresma mwaka huu, ni familia kanisa la nyumbani, shule ya imani na maadili.

 

Celina Matuja/Joyce Sudi.

 

 

 

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.