Menu
RSS

Waanglikana wamkabidhi zawadi Baba Mtakatifu

PICHA YA BABA MT AKIPOKEA ZAWADI PICHA YA BABA MT AKIPOKEA ZAWADI

ROMA, Italia

UONGOZI na waamini wa Kanisa Anglikana la Watakatifu Wote la Roma nchini Italia, wamemkabidhi Baba Mtakatifu Fransisko zawadi mbalimbali baada ya kufanya ziara ya kihisroria kanisani hapo hivi karibuni.

Miongoni mwa zawadi alizokabidhiwa Baba Mtakatifu ni ahadi ya kutoa chakula kwa ajili ya maskini, Biblia Takatifu kwa ajili ya waathirika wa biashara haramu ya binadamu Barani Afrika na Keki ya Kwaresma.

Jumuiya ya Kanisa hilo iliamua kutoa zawadi hizo kwa ajili ya ziara hiyo ya Baba Mtakatifu ya Februari 26, 2017 iliyoenda sanjari na maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 200 tangu kuanzishwa kwake.

Kwanza waamini wa Kanisa Anglikana la Watakatifu Wote la Roma kwa kushirikiana na Parokia Pacha ya Kanisa Katoliki ya Watakatifu Wote, waliahidi kutoa chakula kila Ijumaa jioni kwa ajili ya maskini wanaorandaranda katika Stesheni ya Treni ya Ostiense, kwa heshima ya Baba Mtakatifu.

Pili, waliahidi kuchapisha nakala 200 za Biblia Takatifu kwa Lugha ya Kiingereza kwa ajili ya jubilei ya Kanisa hilo na kati ya hizo, 50 zitatolewa bure kwa makahaba waliopo nchi za Afrika Magharibi walioomba kupewa msaada huo wa kuwaongoa.

Kwa mujibu wa mpango uliopo, nakala hizo za Biblia Takatifu zitasambazwa kupitia mtandao wa Watawa wanaowasaidia waathirika wa biashara haramu ya biandamu wengi wao wakiishia kushinikizwa kutumiwa katika biashara ya umalaya.

Katika ziara hiyo, Askofu Robert Innes wa Kanisa Anglikana, Jimbo la Ulaya, alimshukuru Baba Mtakatifu Fransisko kwa kutembelea Kanisa la Watakatifu Wote la Roma na kuweka historia ya kuwa Baba Mtakatifu wa kwanza kutembelea Kanisa hilo.

Licha ya Baba Mtakatifu kuwa Askofu wa Roma wa kwanza kufanya ziara kanisani hapo, upo uhusiano mwema kati ya viongozi wakuu wa Makanisa hayo mawili yaani Baba Mtakatifu na Askofu Mkuu wa Canterbury aliye Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana kama alivyo Baba Mtakatifu kwa Kanisa Katoliki.

Tangu Baba Mtakatifu alipochaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki mwaka 2013, Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby, ameshakutana mara tatu na kuzungumza na Baba Mtakatifu Fransisko.

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.