Menu
RSS
Vatican kushiriki miaka 60 ya Uhuru wa Ghana

VATICAN CITY, Vatican

RAIS wa Serikali ya Mji wa Vatican, Mwadhama Giuseppe Kardinali Bertello, anatarajiwa kumwakilisha Baba Mtakatifu Fransisko katika maadhimisho ya miaka 40 ya Uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Serikali ya Ghana na Vatican.

Idara ya habari ya Vatican ilieleza kuwa maadhimisho hayo yaliyoanza Machi 3 na kufikia kilele chake Machi 6, 2017, yatakwenda sanjari na Kilele cha miaka 60 ya Uhuru wa Ghana.

Ilielezwa katika taarifa hiyo ya Vatican kwamba Ghana iliyojipatia Uhuru wake na kuwekwa wakfu kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu, Machi 6, 1957 iko kwenye Novena iliyoanza Februari 23 na kumalizika Ijumaa Machi 3.

Hatua ya Vatican kumtuma Kardinali Bertello kumwakilisha Baba Mtakatifu katika maadhimisho hayo kulielezwa kuwa ni kuonesha Vatican inavyothamini uhusiano uliopo kati ya Kanisa Katoliki na Serikali za mataifa mengine. 

Akieleza kuhusu maadhimisho hayo, mratibu wake kwa upande wa kiroho, Askofu Mkuu Charles G. Palmer-Buckle, alisema Baraza la Maaskofu Katoliki Ghana linataka kuiweka wakfu nchi hiyo chini ya Ulinzi wa Moyo Mtakatifu wa Yesu.

Askofu Palmer-Buckle alibainisha kuwa tendo hilo la kuiweka Wakfu familia ya Mungu nchini Ghana litafanyika wakati wa maadhimisho hayo katika ibada ya Kiekumene itakayoongozwa na Askofu Mkuu Jean-Marie Speich.

Makamu huyo wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Ghana alisema, Maaskofu waliamua kufikia hatua hiyo kwa kuwa Moyo Mtakatifu wa Yesu ni chemchem ya huruma, neema ya Mungu, msamaha, upendo, unyenyekevu, upole na maisha mapya.

Alisema, Moyo Mtakatifu wa Yesu ni kiini cha Sakramenti za Kanisa uliotobolewa kwa mkuki na kutoka Maji na Damu zilizo alama ya Sakramenti ya Ubatizo na Ekaristi Takatifu.

“Moyo Mtakatifu wa Yesu ni kiini cha Sakramenti za Kanisa uliotobolewa kwa mkuki na kutoka Maji na Damu zilizo alama ya Sakramenti ya Ubatizo na Ekaristi Takatifu” alisema Askofu Palmer-Buckle.

Makamu huyo wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Ghana alisisitiza kuwa Moyo Mtakatifu wa Yesu ni mwanzo na hatima ya maisha na utume wa Kanisa, chemchemi ya utakatifu na ukamilifu wa maisha ya Kikristo.

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.