Menu
RSS

Walutheri kusherehekea miaka 500 ya mageuzi

LUND, Uswisi

JUBILEI ya miaka 500 ya Mageuzi ya Kiluteri inatarajiwa kuadhimishwa Jumatatu ya Oktoba 31, 2016 huko Lund na Malmo nchini Uswiss.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanywa kwa ushirikiano kati ya Kanisa Katoliki na Shirikisho la Makanisa ya Kiinjili ya Kiluteri Duniani.

Kufuatia maadhimisho hayo, Baba Mtakatifu Fransisko anatarajiwa kufanya hija ya kitume nchini Uswis ili kushiriki maadhimisho hayo ya kihistoria katika maisha na utume wa Kanisa.

Licha ya changamoto kadhaa, makanisa hayo mawili yamefaulu kupita hasa ikizingatiwa kuwa, maadhimisho hayo yanafanyika ndani ya kipindi cha miaka 50 tangu Kanisa lianzishe mchakato wa majadiliano ya kiekumene kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Kilutheri.

Chimbuko la maadhimisho hayo ni Martin Luther ambaye mwaka 1517, alilaani kwa nguvu zake zote vitendo vilivyokuwa vimejitokeza vya kuuza rehema kwa kuzingatia msingi ya maisha ya kiroho na teolojia, hivyo kuleta mageuzi makubwa katika medani za kisiasa, kiuchumi, kiroho na kijamii.

Martin Luther hakuwa na wazo la kuanzisha Kanisa jipya, lakini kutokana na matukio yale, alijikuta analazimika kuanzisha Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Duniani, hivyo kusababisha machafuko na mgogoro ndani ya Kanisa.

Maadhimisho ya kumbukumbu hiyo yaliyofikia miaka 500, kwa muda wa miaka mingi yalikuwa ni sawa na kurasa chungu za misigano kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Duniani.

Lakini kwa mwaka huu, mambo ni tofauti kabisa, kwani Wakristo wanataka kujikita zaidi katika mambo yanayowaunganisha badala ya kuogelea mambo yanayowagawa.

Kwa sababu hiyo, Baba Mtakatifu Fransisko ameamua kushiriki kikamilifu katika tukio hilo la kihistoria litakalofanyika Lund na Malmo nchini Uswiss.

Lengo ni kuiangalia Jubilei ya miaka 500 ya Mageuzi ya Kilutheri kwa jicho la matumaini pamoja na kuendelea kuimarisha mafanikio yaliyokwisha kupatikana kama sehemu ya mchakato wa majadiliano ya kiekumene katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.

Mababa wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican walisisitiza kwa namna ya pekee maridhiano kati ya waamini wa Makanisa hayo mawili na kwamba, Sakramenti ya Ubatizo ni kiini cha imani yao kwa Kristo na Kanisa lake na hivyo wote ni sehemu ya Fumbo la Mwili wa Kristo yaaani Kanisa.

Jubilei ya miaka 500 ya Mageuzi ya Kiluteri ni fursa ya kukuza na kuimarisha mahusiano mazuri yaliyofikiwa baina ya Makanisa hayo mawili katika Uekumene wa huduma unaoshuhudiwa na waamini wa Makanisa hayo mawili sehemu mbalimbali duniani.

Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita kumekuwepo na mafanikio yaliyofikiwa na kutiwa saini kwenye Waraka wa pamoja kuhusu Mafundisho ya “Kuhesabiwa haki ndani ya Kanisa” yaliyotiwa sahihi kati ya Makanisa haya kunako mwaka 1999.

Dhana ya kuhesabiwa haki ilikuwa ni kiini cha mpasuko kati ya Makanisa hayo katika Karne ya XVI.

Jubilei ya miaka 500 ya Mageuzi ya Kiluteri yanaongozwa na kauli mbiu “Kutoka katika kinzani kuelekea kwenye umoja. Tumeungana katika matumaini”. 

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.