Menu
RSS

Kanisa lataka mshikamano DRC

Kanisa lataka mshikamano DRC

KINSHASA, DRC

BARAZA la Maaskofu Katoliki Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), limesema makubaliano yaliyofikiwa na vyama vya kisiasa nchini humo kuhusu uchaguzi mkuu, hayana budi kujikita zaidi katika ustawi, maendeleo na maslahi ya wananchi wengi.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Vatican, Maaskofu hao walitoa tamko lao na kutaka makubaliano hayo yasiangalie faida zinazoweza kupatikana kwa vyama vya siasa husika pekee na viongozi wake.

Maaskofu hao walikubaliana kimsingi katika tamko hilo kwamba, wakati wa kipindi cha mpito kutaundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayokuwa kweli na sura ya kitaaifa.

Mapendekezo yao ni kuona Serikali hiyo inakuwa na Waziri Mkuu atakayetoka vyama vya upinzani wakati Rais Joseph Kabila anayemaliza muda wake, akiendelea kuwa kiongoza wa DRC.

Kabla ya kutoa tamko hilo wakati wajumbe kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki DRC walijitoa katika majadiliano kati ya Serikali na vyama vya upinzani, kwa sababu ya kukosekana kwa uwakilishi mpana wa vyama vyote vya upinzani.

Maaskofu hao walisema, mmbo ya msingi yanayotakiwa kupewa kipaumbele ni maandalizi ya uchaguzi mkuu, haki za msingi za binadamu, kuyafanya maisha ya wananchi kuwa bora zaidi kwa njia ya huduma za jamii hasa afya, elimu na uchumi.

Katika tamko lao, Maaskofu walieleza kuwa Baraza la Maaskofu Katoliki DRC linataka kujielekeza zaidi katika kukuza na kudumisha misingi ya haki, amani, maridhiano, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Last modified onWednesday, 02 November 2016 13:08
back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.