Menu
RSS

Baba Mtakatifu awakumbuka waathirika wa Kimbunga Matthew

 

POT-AU-PRINCE, Haiti

BABA Mtakatifu Fransisko ameungana na watu wote walioguswa na kutikiswa kwa Kimbunga Matthew kilichovikumba Visiwa vya Carribean, lakini kwa namna ya pekee, Haiti.

Baba Mtakatifu alionesha masikitiko yake hayo wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, baada ya maadhimisho ya Jubilei ya Bikira Maria, maalum kwa vyama vya kitume vyenye ibada kwa Bikira Maria Mama wa Mungu na Kanisa iliyofanyika Dominika ya 28 ya Mwaka C wa Kanisa.

Akihutubia mahujaji waliofika kwenye Viwanja vya Mtakatifu Petro, Vatican, Baba Mtakatifu aliwaambia mahujaji hao kwamba alikuwa ameguswa kwa namna ya pekee na maafa makubwa yaliyotokana na kimbunga hicho.

Alisema, angependa kuonesha uwepo wake wa karibu na matumaini makubwa kwa mshikamano unaoendelea kuoneshwa na jumuiya ya kimataifa, taasisi za Kanisa pamoja na watu wote wenye mapenzi mema.

Baba Mtakatifu alisema, anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kuungana naye katika sala kwa ajili ya watu hao walioathirika kwa kiasi kikubwa.

Haiti ilipata athari kubwa kutokana na Kimbunga Matthew kilichoua watu wapatao mia tisa, kuharibu maelfu ya nyumba na kusababisha watu 350,000 kuwa katika hali ya kuhitaji misaada.

Hata hivyo, Serikali ya Haiti ilieleza kuwa idadi rasmi ya watu waliofariki dunia na kuthibitishwa ni 336, ingawa idadi inaweza kuwa kubwa zaidi kwa kuwa wengi katika maeneo ya vijijini hawakuweza kufikiwa kwa sababu ya kukatika kwa barabara na kuvunjika kwa madaraja.

Katika sala hiyo ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu alimkumbuka Padri Gennaro Fueyo Castanon na waamini walei watatu waliotangazwa kuwa Wenyeheri huko Oviedo, Hispania, Jumamosi Oktoba 8, 2016.

Baba Mtakatifu alimshukuru Mungu Mwenyezi kwa mashuhuda hao wa imani wanaoungana sasa na umati mkubwa Mashahidi wa Imani walioyamimina maisha yao kwa ajili ya Kristo na Kanisa lake.

 

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.