Menu
RSS

Kanisa lataka amani Ghana kuelekea uchaguzi

Kanisa lataka amani Ghana kuelekea uchaguzi

 

TAMALE, Ghana

 

BARAZA la Maaskofu Katoliki Ghana (GCBC) limetoa wito kwa waamini na wananchi wote wa nchi hiyo kudumisha amani wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye Desemba 7 mwaka huu.

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Ghana na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Konongo-Mampong, Mhashamu Joseph Osei-Bonsu, alitoa wito huo kupitia Mkutano Mkuu wa GCBC uliofanyika hivi karibuni katika mji wa Kaskazini wa Tamale.

Askofu Osei-Bonsu alisema, Ghana imekuwa katika wakati mzuri wa amani na utulivu iliyopo hadi sasa aliyosema inatakiwa kulindwa na kila mwananchi wa Ghana mwenye mapenzi mema.

Alisema, wananchi wote wa Ghana wanatakiwa kukumbuka kuwa wana nchi moja tu nayo ni Ghana nayo ndiyo nyumba ya kila mwananchi wa Ghana inayotakiwa kulindwa kwani ndimo wanamoishi.

“Wananchi wote wa Ghana tunatakiwa kukumbuka kuwa tuna nchi moja tu nayo ni Ghana nayo ndiyo nyumba ya kila mwananchi wa Ghana inayotakiwa kulindwa kwani ndimo tunamoishi” alisema, Askofu  Osei-Bonsu.

Osei-Bonsu alaisema, wananchi wa Ghana wasingetaka kuoma machafuko yakitokea kabla, wakati au baada ya uchaguzi kwani wamezoea kuishi kwa amani na upendo.

Aliwakumbusha wananchi wa Ghana kwamba matokeo ya machafuko yanajulikana kwa kila mtu ikiwemo kupotea kwa maisha ya binadamu, majeruhi na uharibifu wa mali, hofu na hatimaye kuibuka kwa wimbi la wakimbizi.

Askofu Osei-Bonsu alisema, wananchi wa Ghana hawataki kuwa wakimbizi katika nchi jirani kwa sababu ya machafuko yatakayotokana na uchaguzi.

“Wananchi wa Ghana hawataki kuwa wakimbizi katika nchi jirani kwa sababu ya machafuko yatakayotokana na uchaguzi” alisisitiza Askofu Osei-Bonsu.

Maaskofu 20 wa Baraza la Maaskofu Katoliki Ghana wameshiriki Mkutano Mkuu huo wa siku 10 wa GCBC ulioongozwa na kauli mbiu ‘Upatanisho na Mungu, Utu na Asili katika Mwaka wa Huruma ya Mungu’

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.