Menu
RSS

Washindi wa Tuzo za Ratzinger watangazwa

Baba mt.Francisko (kushoto) na mtangulizi wake Baba mt.Francisko (kushoto) na mtangulizi wake

 

VATICAN CITY, Vatican

 

MFUKO wa Joseph Ratzinger, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI, umewatangaza washindi wa Tuzo ya Ratzinger kwa mwaka 2016 nao ni Monsinyori Inos Biffi na Ioannis Kourempeles.

Tangazo lililotolewa na mfuko huo limeeleza kuwa washindi hao, watakabidhiwa tuzo zao Kwnye Jumba la Kitume mjini Vatican, tarehe 26 ya mwezi ujao.

Tuzo hiyo hutolewa ili kuthamini na kuonesha moyo wa shukrani kutoka kwa Mama Kanisa kwa watu wanaojipambanua kwa mchango wao mkubwa katika kazi, maisha, tafiti na machapisho ya kisayansi.

Kazi hizo yaani tafiti na machapisho ya kisayansi ni zile zinazolisaidia Kanisa kuwafunda na kuwaelimisha na kuwajenga watu mbalimbali katika maisha ya kiroho na kijamii.

Lengo la Tuzo hiyo ya ya Ratzinger ni kuwahamasisha wasomi kusaidia mchakato wa Mama Kanisa katika kuwarithisha watu wa kizazi hiki ujuzi na maarifa mbalimbali.

Mshindi wa kwanza Monsinyori Biffi ni profesa, mwanateolojia na mwana liturjia mahiri anayetambulika kimataifa akiwa ameandika vitabu na majarida mbalimbali.

Monsinyori Biffi ametunukiwa tuzo hiyo kutokana na mchango wake wa mkusanyiko wa machapisho yake hasa katika teolojia na falsafa, kati yake 20 yameshachapishwa na kutolewa na kazi zilizobaki zikiwa katika maandalizi.

Mshindi mwingine, Ioannis ni msomi, mwamini wa Kanisa la Orthodox, akiwa profesa katika Kitivo cha Teolojia, Chuo Kikuu cha Aristotle cha Thessaloniki nchini Ugiriki.

 

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.