Menu
RSS

Majeswiti wapata mkuu mpya

 

 ROMA, Italia

Shirika la Wajeswiti limemchagua Padri Arturo Sosa Abascal kutoka Venezuela, kuwa Mkuu wa Shirika mpya wa shirika hilo lenye makao yake Makao Makuu mjini Roma.

Padri Artusro Sosa alichaguliwa katika Mkutano Mkuu wa shirika hilo 30 akichukua nafasi ya Mkuu wa Shirika aliyestaafu, Padri Adolfo Nicolàs aliyestaafu Oktoba 3, mwaka huu kutokana na umri mkubwa.

Padri Artusro Sosa aliyezaliwa mwaka 1948, alijiunga na Shirika la Majeswiti mwaka 1966 na kupewa Daraja Takatifu la Upadri mwaka 1977, anakuwa Mkuu wa Shirika wa 30.

Kabla ya kuchaguliwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika mjini Roma, Padri Arturo Sosa alikuwa mwalikishi wa Wakuu wa Kanda wa Shirika la Majeswiti mjini Roma.

Kati ya mwaka 1996 na mwaka 2004 alikuwa ni Mkuu wa Shirika la Majeswiti, Kanda ya Venezuela na amewahi pia kuwa Mratibu wa Shughuli za Kijamii na Mkuu wa Kituo cha Utafiti cha Majeswiti, Amerika Kusini huko Gumila.

Kwa muda mrefu, Padri Arturo Sosa alitekeleza utume wake kwa kuwalea na kuwafundisha vijana katika masuala ya elimu, kwani kimsingi yeye mtaalamu aliyebobea katika masuala ya elimu na ni mwandishi mahiri wa vitabu hasa kuhusu historia na siasa ya maisha ya familia ya Mungu nchini Venezuela.

Padri Adolfo Nicolàs akiwa Mkuu wa Shirika, mwaka 2008 katika Mkutano Mkuu wa 35, Arturo Sosa aliteuliwa kuwa Mshauri Mkuu na kunako mwaka 2014 akateuliwa kuwa mmoja wa washauri wakuu wa shirika hilo.

 

Katika mkutano Mkuu wa shirika wa Roma mwaka huu, wajumbe 212 kutoka nchi 66 walishiriki.

 

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.