Menu
RSS

Wakimbizi na wahamiaji wasiachwe

GENEVA, Uswisi

KATIBU Mkuu wa Baraza la Makanisa Duniani (WCC), Dk. Olav Fykse Tveit, ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kuwa wakimbizi na wahamiaji wanakuwa katika mikono salama.

Dk. Olav alitoa wito huo wakati akichangia mada kwenye mkutano uliojadili changamoto ya wakimbizi ulioitishwa na WCC kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa, uliofanyika mjini Geneva, Uswisi.

Alisema, jibu makini linaloweza kudhibiti wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji kutoka sehemu mbalimbali duniani ni kuhakikisha, mizozo, migogoro na mipasuko ya kijamii inamalizika kwa njia za amani.

Dk. Olav alisema, iwapo migogoro inayoendelea katika nchi mbalaimbali ikiwemo Libya, Iraq, Somalia, Afghanstan na Eritrea, haitapatiwa ufumbuzi, wakimbizi na wahamiaji wataendelea kuwepo.

Alisema, makundi ya namna hiyo yataendelea kuwepo kwa sababu yanatafuta hifadhi na usalama hasa katika Bara la Ulaya kunakoelekea kuna amani na utulivu.

“Makundi ya namna hii yataendelea kuwepo kwa sababu yanatafuta hifadhi na usalama hasa katika Bara la Ulaya kunakoelekea kuna amani na utulivu” alibainisha Dk. Olav.

Dk. Olav alisema, ni jukumu la jumuiya ya kimataifa kutowaacha wahamiaji na wakimbizi kwa kuhakikisha kuwa mizozo, vita na machafuko vinapatiwa ufumbuzi wa kudumu, huku haki, amani na usalama vinakuzwa na kudumishwa.

Alisema, WCC inawataka wakuu wa jumuiya ya kimataifa kushikamana na kushirikiana zaidi ili kuratibu na kuwasaidia wakimbizi na wahamiaji wanaotafuta hifadhi, usalama na maisha bora zaidi.

Alisema, katika siku za hivi karibuni, Umoja wa Ulaya (EU) unaonekana umeshindwa kutekeleza dhamana na wajibu wake katika kuratibu huduma kwa wakimbizi na wahamiaji jambo alilosema siyo zuri.

“Katika siku za hivi karibuni, Umoja wa Ulaya (EU) unaonekana umeshindwa kutekeleza dhamana na wajibu wake katika kuratibu huduma kwa wakimbizi na wahamiaji na kwa kweli jambo hili siyo zuri” alisema Dk. Olav.

Dk. Olav alisema, suala la wakimbizi na wahamiaji linahitaji mshikamano wa upendo wa jumuiya ya kimataifa ikiongozwa na nchi za EU zinazotakiwa kulinda na kudumisha haki za msingi za binadamu pamoja na kushirikiana rasilimali watu na nguvu kazi.

Katibu Mkuu huyo wa WCC alisema,  jambo lililojitokeza kwa sasa na kuwa changamoto kubwa ni kwa baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya kuwaona wakimbizi na wahamiaji kuwa ni mzigo hivyo kuamua kufunga mipaka yake kwa muda.

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.