Menu
RSS

Lishe bora bado mwiba kwa watoto Tanzania

Lishe bora bado mwiba kwa watoto Tanzania

Na Celina Joseph                   

Imeelezwakuwawatoto 42 katika ya 100 nchini Tanzania wanaudumavukutokananakukosalishe bora. 

Hayoyalielezwa hivi karibuni na  Lediana Mngong’o, Mwenyekitikikundi cha Wabunge wa masualayalishe uhakikawachakulanahakizawatoto,katikauzinduziwaripotiyaKimataifayalishe iliyofanyikakatika Hotel yaProteajijini Dar esSalaam. 

Alisema hali ya duni ya lishe inaathari kubwa  hasa katika siku 1000 za mtoto tangu kutungwa mimba,kuzaliwa hadi anapofikisha miaka miwili na kwamba tatizo hilo endapo litaendelea mtoto anaweza kudumaa kiakili na humuathiri mtoto katika maisha yake yote.

Alisema lishe bora ni muhimu kwa mtoto hivyo elimu inatakiwa kutolewa kwa akinamama kuwanyonyesha watoto wao maziwa ya mama pekee bila kuwapa vyakula hadi wanapofikisha umri wa miezi sita.

Alisema licha ya kuwa suala hilonchininimtambuka linahitaji  juhudinauwajibikaji  kwakilammojaikiwemoserikali, sekta binafsi kuwekeza katika lishenavyombovyahabariambaowanawezakutoaelimukwajamii. 

Kwa upande wake MratibuwaLisheOfisiyaWaziriMkuu Saraha Mshiu, alisema Tanzania kwakiasifulani imepigahatuakatikakupunguzatatizo la lishekutokaasilimia 42 hadi 37.5 ndani ya  miaka mitano iliyopita.

Alisema bado tatizo la lishe bora linatakiwa kupewa kipaumbele na kuongeza kuwa Serikali imejipanga kutoa elimu zaidi ya suala hilo na madhara ya ukosefu wa lishe bora na udumavu.

Alisema Serikali pia imejipanga kushirikisha sekta binafsi kuwekeza katika suala la lishe bora na kutoa nafasi kwa taasisi hizo kuwaruhusu akinamama waliojifungua kuwanyonyesha watoto wao kwa kipindi cha miezi sita mfululizo ndipo arejee kazini kwani kufanya hivyo watapunguza utapia mlo na udumavu.

Alisema kwa kuwa serikali inalitambua suala la lishe kuwa ni mtambuka  mwakajanailizinduampangowakuongezaviinilishekatikavyakulaikiwanipamojanaungawanganonamafutayakulaambayo yanatumiwa na kila hadi vijijini. 

Naye Lyidia Bendera KatibuMkuu  waChamaChaADC  alisemaSerikaliitakayoingiamadarakanikwadhamanayamiakamitanoijayoiweke  jitihadazamakusudikatikasuala la lisheilikuondoatatizo la udumavunautapiamlonchini. 

Aliomba Wizara ya Kilimo na Mifugo kuhakikisha suala la lishe kwa watanzania linaangaliwa kwa undani ili watu wapate lishe nzuri badala ya kuishia kuzungumza bila vitendo na uwepo umoja kwa kila mmoja.

Naye GraceGitauMratibuwaKitaifawamasualayalishenchiniKenyaalielezeamalengoyaliyofikiwakatikauzinduzihuonamipangoyabaadayekuhakikishanchihizozinatengabajetiyalishe 

Gitau alisema kwa Kenya imepiga hatua kwa kuangalia watoto waliodumaa kutokana na ukosefu wa lishe kwa mwaka 2008 na hivyo kupunguza utapia mlo kwa watoto waliochini ya miaka mitano kutoka asilimia 35% hadi 20% kwa sasa.

Alisema moja ya mambo waliyozungumzia ni kutenga kiwago cha fedha ili kukabiliana na tatizo la utapia mlo, katika miradi ya  Afya,kilimo, elimu na maji.

Aliongeza kuwa kupitia miradi hiyona nchi husika zikizingatia kutenga bajeti katika suala la lishe zitaweza kupambana na utapia mlo.

Aidha alisema waluzungumzia suala la kuangali Bajeti za kila mwaka kwa masuala ya lishe iwapo zinakidhi kupambana na utapia mlo.

Kulingana na utafiti ulifanyika mwaka ulipita nchi zote za Afrika Mashariki ni nchi mbili tu ambazo zilifanikiwa kutenga bajeti ya lishe ambayo kwa kiasi fulani ingesaidia.

Alisema kuwa kati ya nchi inazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiangalia utagundua  kwamba Ethiopia walikuwa na asilimia 67%kulingana na lengo la nne ambalo wanapaswa kutimiza kupunguza hali ya lishe.

Burudi ina asilimia 5% ambayo imekuwa chini kati ya malengo waliyojiwekea,Rwanda ni ya pili ambayo imefikisha kiwango kwa kuwa na asilimia 56%,  Kenya asilimia 44% Uganda asilimia 43% Tanzania asilimia 40%  ambapo awali ilikuwa na asilia 42%.Utafiti huo ni kwa miaka miaka mitano iliyopita.

Naye Mkurugenzi wa Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) alisema hali ya lishe katika ukanda wa Afrika ni mbaya, kwa kuwa ni nchi chache zenye nafuu kupambana na lishe, Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi hizo.

Alisema ingawa Tanzania ina malengo ya kuondoa tatizo la lishe ifikapo mwaka 2025 juhudi za kutokomeza hali hiyo zinahitajika si tu kwa serikali bali mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi.  

Ripoti ya lishe Kimataifa kwa mara ya kwanza ilizinduliwa mwaka 2014 ikiwa na kauli mbiu "Kuulisha Ulimwengu, Kuilea Dunia" ambayo ilichaguliwa kwa lengo la kuongeza hamasa kuimarisha kilimo cha familia na wakulima wadogo wadogo.

Aliongeza kuwa maadhimisho hayo pia yalilenga kuuzindua ulimwengu kuhusu jukumu la kutokomeza njaa na umaskini, kuhakikisha kuna usalama wa upatikanaji wa chakula na lishe bora, kuboresha kipato, kusimamia vyema raslimali, kuyalinda mazingira na kufanikisha maendeleo endelevu, hususan katika maeneo ya mikoani.

Nchizilizoshirikiuzinduzihuonipamoja na Kenya, wenyeji Tanzania, Uganda, Ethiopia,Burudi, Rwanda na Malawi ambaowalishirikikamawasikilizaji. 

 End 

back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.