Lishe bora tiba ya utapiamlo.
Lishe bora tiba ya utapiamlo
Na Mwandishi Wetu
Hali ya afya na lishe bora kwa mama mjamzito ni muhimu kabla na baada ya ujauzito kwa kuwa husaidia kuwepo kwa matokeo mazuri ya ujauzito na kufanikisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama.
Ndani ya siku 1000 yani tangu mama apate ujauzito hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka miwili ni muhimu akazingatia lishe bora pamoja na mtoto wake ili kuhakikisha mtoto anakua vizuri na kuepuka matatizo ambayo anaweza kuyapata ikiwemo utapiamlo, ugonjwa unaotokana na kupunguza au kuzidisha mahitsaji muhimu katika mwili.
Kuna aina mbalimbali za utapiamlo ambazo mtoto anaweza kuzipata ikiwemo utapiamlo wa kukonda, utapiamlo wa ufupi na hali hiyo huwa hivyo mpaka kwenye maendeleo ya ubongo wake.
Mtoto kuwa na uzito usioendana na umri na utapiamlo wa madini na vitamini ambao unaweza kuwapata hata watoto warefu na kwamba una dumaza ubongo wa mtoto.
“Unaweza kumkuta mtu mrefu lakini amekuwa na shida katika uelewa wake kwakuwa anakuwa na uelewa wa hali ya chini sana”,anasema Mary.
Utapiamlo usababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa chakula, hali ya usafi wa chakula, kutokuwepo kwa uangalizi na kwamba zipo sababu zilizojificha ambazo ni pamoja na umaskini unaobabisha kukosa chakula, uwezo wa mama kufanya maamuzi na mazingira ya njaa na hivyo waathirika wakuu ni watoto walio chini ya umri wa miaka miwili na kina mama.
Mary alieleza kuwa madhara ya utapiamlo kuwa ni pamoja na vifo vya watoto 130 kila siku, huaribu mfumo wa kinga mwili na kusababisha maradhi, watoto waliozaliwa na uzito pungufu hupata kisukari, hupata matatizo ya moyo, kuwa na uwezo mdogo na kukosa uwezo wa kuzalisha na kufanya maamuzi.
Binafsi nimeshuhudia baadhi ya watoto waliopata utapiamlo kutokana na kutozingatia taratibu za lishe ambazo mzazi ama mlezi anatakiwa kuzifuata ikiwa pamoja na wazazi wenyewe kuwa na afya duni, hali inayoweza kusababishwa na mambo mbalimbali yanayomkwamisha mama kupata lishe bora kwake na mtoto wake.
Mary Kabona Mtaalamu wa lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni katika semina ya waandishi wa habari kuhusu Lishe ya watoto na maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji ambayo ufanyika kila mwaka Agosti Mosi hadi Agosti 7, alisema kuwa ikiwa mama mjamzito atakosa lishe bora hata mtoto wake atapata utapiamlo.
“Licha ya mtoto kupata utapiamlo hali hiyo uweza kusababisha kifo kuzorotesha maendeleo ya mtoto, Udhoofisha ubongo wa mtoto na ingawa mtoto anakuwa mtu lakini si mtu bora yaani ni mtu asiye na uwezo’’,anasema Mary.
Mary anaeleza kuwa hali ya lishe na ulishaji watoto wachanga nchini Tanzania si ya kuridhisha kwa kuwa wazazi au walezi wanashindwa kuzingatia taratibu za lishe kwa watoto wao wawapo wa changa hali inayosababisha asilimia kubwa ya wazazi kukiuka taratibu za kiafya kwa kuwapatia watoto chakula cha nyongeza kabla ya wakati unaotakiwa kitalaam.
“Hali ya lishe kwa watoto nchini si nzuri kwani takwimu za mwaka 2010 zinaoonesha 42% ya watoto wanatatizo la udumavu, utapiamlo huku mwaka jana 2014hali hiyo ilionekana kushuka na kufikia 34.7%, na kwamba kitaifa tupo katika hali ya juu ya tatizo ingawa mikoa mingi iliyo na tatizo la utapimlo ina chakula cha kutosha’’,anasema Mary.
Mary anadokeza kuwa kuwepo kwa tatizo la utapiamlo katika mikoa iliyo na chakula cha kutosha kunatokana na aina ya ulishaji watoto isiyozingatia kanuni na taratibu za afya katika suala la ulishaji watoto ikiwa ni pamoja kumpa mtoto chakula cha aina moja, mama aliyejifungua kutomnyonyesha mtoto mapema ndani ya saa moja.
Nyingine ni pamoja na mama kumpa mtoto maziwa ya njano mapema kwa kuwa yana kinga mwili nyingi na vitamin A,kutokumnyonyesha usiku na mchana kila wakati miezi sita bila kumpa kitu kingine kwa kuzingatia taratibu za afya.
Anasema kuwa matumizi ya chupa ya maziwa kwa mtoto mdogo ni hatari kwani hayastahili, aliongeza kuwa na takwimu za mwaka 2010 kwa wazazi wanaozingatia taratibu za ulishaji watoto nchini kuwa ni 49% na hadi kufikia mwaka 2014 imefikia 50.8% na hu8ku nusu ya watoto wakionekana kucheleweshwa.
Taratibu zinazokiukwa kuwa ni pamoja na kuwapa watoto chakula cha nyongeza mapema kabla ya kufikisha miezi sita, hali inayohatarisha afya ya mtoto, kutokana na kumpa vitu vinavyohatarisha afya yake.
Ukiukwaji mwingine unaofanywa na wazazi na walezi ni 5% ya watoto walio chini ya miezi sita wanapewa maziwa yasiyo ya mama na wqengine wakiwapa maziwa ya chupa.
Mary anaeleza kuwa hata wakati wa ulishaji vyakula vya nyongeza asilimia 24ya wazazi ndio wanaowapa watoto wao chakula chenye mchanganyiko unaotakiw, angalau kiwe na maziwa ikiwa pamoja na kuzingatia umri wake ambapo ni asilimia 20ya wazazi ndio wanaozingatia hilo kwa watoto wao.
Aidha Mary alidokeza kuwa ukiukwaji wa taratibu za ulishaji mtoto zinatokana na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na kutokuwepo kwa rasilimali watu na rawsilimali fedha, tafiti zinazofanyika kuhusu suala hilo ni ndogo, Sheria ya mateniti kutotekelezwa lakini pia uuzaji wa chakula cha mtoto kinyume na taratibu za afya.
Nyingine ni mabadiliko ya tabia nchi,majanga ya wakimbizi, mabovu, mafuriko yanayowaathiri mama na mtoto, upungufu wa kinga mwilini HIV ambapo mtoto akipata maaambukizi afya yavke inakuwa mgogoro.
“Lakini hata wakina mama kuwa busy na kazi hali inayosababisha watoto kushindwa kunyonya vizuri ni moja ya changamoto inayochangia wazazi kushindwa kufuata utaratibu wa afyas katika malezi ya watoto na kusababisha changamoto za kiafya kwa watoto wao.
Binafsi naamini hakuna linaloshindikana chini ya jua ni kiasi cha kuamua na kuchukua hatua ili kuwasaidia watoto kukua vizuri kimwili na kiakili ikiwa pamoja na kuhakikisha Taifa linaendelea kwani udumavu kwa watoto unarudisha nyuma maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Ni wakati sasa wa wanawake kuamka na kufuata taratibu za kiafya zinazotolewa na wataalam wa afya ili kuwapa watoto wadogko au wachanga kinachostahili ikiwa ni njia bora ya kuepuka tatizo la udumavu linalowakuta watoto wengi nchini na kusababisha kurudisha nyuma maendeleo yao ya kimwili na kiakili, kumaliza tatizo la udumavu nchini inawezekana.