Menu
RSS

Jitihada za Zimbabwe katika kuzindua sarafu yake ya dola

  • Published in Africa

Mwaka 2009, Zimbabwe ililaazimika kuachana na dola yake ambayo hakuna alietaka kuitumia, na kuanza kutumia dola ya Marekani ili kuepusha kuanguka kwa uchumi wake na mfumuko wa bei wa kiwango cha juu kabisa.

Na sasa hakuna anaetaka kutumia sarafu zilizoingizwa kwenye mzunguko mwezi uliyopita.

Maamuzi ya kuitumia dola ya Kimarekani, kama sarafu rasmi ya nchi kama ilivyofanya Ecuador yanazusha maswali kuhusu ugavi wa fedha, sera ya fedha na hata uhuru wa taifa.

Kitendawili cha sarafu ya Zimbabwe kinabainisha pia ugumu wa kila siku wanaokabiliana nao wakati uchumi wao unapoelekea kwenye njia kama hiyo.

Noti za Marekani zinapatikana kirahisi, lakini kupata sarafu za dola ya Marekani na kuziweka katika mzunguko ni jambo tofauti

Kwa hiyo Gavana wa Benki kuu ya Zimbabwe John Mangudya alianzisha sarafu zilizopewa jina na 'bond coins' mwezi uliopita. Jina hilo limetokana na dhamana za dola milioni hamsini, zilizotolewa kwa ajili ya kuzichapisha na kuzisafirisha kutoka nchi jirani ya Afrika Kusini

Read more...

Shell kuwafidia Wanigeria dola milioni 84

  • Published in Africa

Kampuni ya Shell italipa fidia ya dola milioni 84 kufuatia kuvuja kwa mabomba ya mafuta nchini Nigeria, hatua inayoweza kufungua njia ya kufidiwa hasara zinazosababishwa na kampuni za mafuta duniani.

Wanavijiji 15,600 kwenye jimbo la Niger Delta watapata dola 3,300 kila mmoja, huku dola milioni 30 zikiingizwa kwenye mfuko wa jamii kwa ajili ya maendeleo ya vijiji vyao.

Hata hivyo, kampuni ya uwakili ya Leigh Day jijini London, Uingereza, ambayo ndiyo iliyofikia makubaliano hayo na Shell kwa niaba ya wakulima hao wa Nigeria, ilisema ni jambo linalokera kwamba imechukuwa miezi sita kwa kampuni tanzu ya SPDC kukubali kwamba ilifanya makosa na kufikia makubaliano ya fidia.

Pamoja na kukiri kwamba makosa kwenye ufungaji wa mabomba ulisababisha kuvuja kwa mafuta, Shell imeendelea kusisitiza kwamba sehemu kubwa ya uharibifu wa mazingira nchini Nigeria husababishwa na hujuma dhidi ya mabomba hayo, uchimbaji haramu wa mafuta na majaribio ya wizi.

Read more...

Jinsi mfumo wa ‘Mti wa Krismasi’ ulivyoleta mafanikio kwenye Soka

KATIKA mchezo wa Mpira wa Miguu kuna mifumo mingi sana ambayo makocha huitumia kwa lengo la kupata mafanikio ndani ya uwanja.

Mifumo hiyo haitumiki tu kama fasheni, bali makocha huzingatia aina ya wachezaji iliyonao.

Ipo mifumo mingi kama vile 4-4-2, 4-3-3, 4-5-1, 3-5-2,4-3-2-1 na hata 9-1 ambao ulikuwa ukitumika miaka ya zamani sana.

Katika soka la kileo tunashuhudia makocha wengi wakitumia mifumo kama 4-4-2, 4-3-3, 3-5-2 na mingineyo mingi, na timu zao zimekuwa zikipata mafanikio pia kupitia mifumo hiyo.

Kupitia mifumo hiyo makocha wengi wanaamini kwamba ndiyo yenye mafanikio makubwa zaidi ikilinganishwa na ile ya miaka ya zamani.

Ikumbukwe kuwa katika miaka ya 1800, mchezo wa soka ulianza kwa kutumia mifumo ambayo leo hii hakuna hata mmoja unaotumika. Mfano mzuri ni Novemba 30 mwaka 1872, timu za taifa za Scotland na Uingereza zilitumia mifumo ya kipekee kabisa.

Uingereza ilitumia mfumo wa 1-1-8 ama unaweza kuuita 1-2-7 wakati Scotland ilitumia mfumo wa 2-2-6.Hadi mechi inamalizika timu zote zilitoka suluhu ya bila kufungana.

 

MFUMO WA ‘CHRISTMAS TREE’

Huu ni mfumo ambao wachezaji hujipanga uwanjani na kutengeneza umbo linalofanana na mti wa Krismasi, ndiyo maana ukaitwa hivyo.

Mfumo huu ni 4-3-2-1 ambao huusisha mabeki wanne, viungo watano na mshambuliaji mmoja. Sifa kuu ya mfumo huu ni kujihami zaidi na mshambuliaji mmoja anapaswa kuwa na nguvu za kupambana na msitu wa mabeki wa timu pinzani.

Mfumo wa mti wa Krismasi unatoa majukumu kwa wachezaji kama ilivyo mingine ambapo katika 4-3-2-1, mabeki wanne kazi yao ni kulinda na mara zote huwa nyuma.

Viungo watatu wanaofuatia, kazi yao ni kuwasaidia mabeki wanne wasipate mashambulizi makali wakati wawili ambao huwa mbele yao, kazi yao ni kumtengenezea mipira mshambuliaji peke(lone striker).

Faida kubwa ya mfumo huo ni kwamba ni mzuri sana kwenye ulinzi na hasara yake kubwa ni kuinyima timu uwezekano wa kupata mabao mengi.

 

MAFANIKIO YAKE KWA MAKOCHA NGULI

Makocha kadhaa nguli walikuwa wakipenda kutumia mfumo huo ambao ni pamoja na Terry Venables, Christian Gross, Carlo Ancelotti, Jose Mourinho na hata Sir Alex Ferguson.

Makocha Terry Venables na Christian Gross waliwahi kuutumia mfumo huo wakati walipokuwa wakifundisha katika klabu ya Tottenham kwa nyakati tofauti. 

Kocha Ancelotti alikuwa akiutumia mfumo huo wakati alipokuwa katika klabu ya AC Milan na Mourinho alikuwa akitumia wakati alipokuwa Chelsea kabla ya kuachana na timu hiyo mwaka 2007.

 

TERRY VENABLES NA CHRISTIAN GROSS

Katika kipindi cha mwaka 1987 hadi 1993, Venables alikuwa akipendelea sana mfumo wa 4-3-2-1.Kwa kutumia mfumo huo aliipatia timu ya Tottenham taji la FA mwaka 1991.

Kabla ya hapo mwaka 1990 Spurs ilimaliza Ligi ya Uingereza katika nafasi ya tatu.Kwa upande wake Gross ambaye alipewa timu ya Spurs mwaka 1997 hadi 1998, aliweza kuinasua kutoka kwenye hatari ya kushuka daraja.

 

CARLO ANCELOTTI

Tangu mwaka 2001 hadi 2009, kocha Carlo Ancelotti alikuwa akiifundisha timu ya AC Milan ya nchini Italia.Aliifundisha timu hiyo akiwa anatumia zaidi mfumo wa mti wa Krismasi wa 4-3-2-1.

Kocha huyo alifanikiwa kuipeleka timu hiyo kwenye michuano ya Ulaya na alianza kwa kuifikisha hatua ya nusu fainali ya Kombe la Ulaya(sasa Klabu Bingwa Barani Ulaya) kwa msimu wa 2001-2002.

Licha ya mfumo wake ulipingwa sana na mmiliki wa klabu hiyo Silvio Berlusconi, Ancelotti aliipatia Milan taji la Klabu Bingwa Ulaya mnamo mwaka 2003 baada ya kuifunga Juventus penati 3-2 kwenye uwanja wa Old Trafford na kisha kushinda taji la Coppa Italia.

Mwaka 2007, Ancelotti aliipatia Milan taji la pili la Klabu Bingwa Brani Ulaya baada ya kuinyuka Liverpool katika dimba la Olympic nchini Ugiriki.Mwaka huohuo kocha huyo aliipatia Milan taji la Klabu Bingwa ya Dunia.

 

JOSE MOURINHO NA SIR FERGUSON

Mourinho alijiunga na Chelsea kwa mara ya kwanza kabiusa mwaka 2004 na kuachana nayo mwaka 2008.Katika kipindi hicho alikuwa akipenda kutumia mfumo wa 4-3-3 na wakati mwingine 4-3-2-1 na kufanikiwa kuipa Chelsea mataji mawili ya Ligi Kuu, matatu ya Kombe la Ligi na moja ya FA.

Sir Alex Ferguson naye wakati akiwa anainoa Manchester United alikuwa akitumia mfumo huo kiujanjaujanja na umemsaidia kwa namna fulani kupata mafanikio makubwa hadi anastaafu.

 

 

 

 

 

Read more...
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.